Una miaka kuanzia 25 na bado upo kwenu huna hata godoro

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,631
Inawezekanaje kijana ashatimiza miaka 25 na kuendelea do yupo kwao?

Miaka 25 huna hata godoro ndugu?Hata kitanda huna?Miaka 25 hata kujitegemea bado? Bado upo kwenu unagombea dawa ya meno na watoto wa ndugu zako kweli?

Vitu vingine ni vya ajabu sana na aibu siwakandii ila ndio kweli haiwezekani una miaka hiyo bado upo kwenu.

Kuanzia miaka 20 sio miaka ya kukaa nyumbani na kula ugali wa bure ni miaka ya kuanza kujitegemea na kujituma

Maana ukishafikisha miaka 25 bado upo kwenu na huna hata godoro kutimiza ndoto zako huko baadae ni ngumu kinoma.

Ni bora kuambiana ukweli, siwasemi wala siwafokei,na msijitie moyo kwa kuambiwa umri bado, sasa kama ndugu yangu wewe unajiona umri bado?Jee hao wenye miaka 14-18 years wasemeje?

Ni jambo la kijinga na udhaifu wa hali ya juu mtu ana miaka 25 bado hajajitegemea na hana chochote cha maana cha kujivunia.

Tunatengeneza taifa lenye vijana wa hovyo sana.
.
.
.
.
TANBIHI

Kwahiyo mnaona ni sawa above 25 waendelee kukaa majumbani wakila vya bure?

Nilileta uzi humu nikisema kwamba mtu wa kuanzia miaka 25 hatakiwi kuwa nyumbani akitegemea wazazi na ndo ukweli huo

Hapa niliwalenga wale ambao kwao wamekaa tu na hawafanyi shughuli yoyote ile ya kipato, wapo ambao kwa mazingira inawalazimu kubaki makwao lakini wana kazi wanafanya inawaingizia kipato

Sio unakaa nyumbani unakula bure, unalala bure, huchangii chochote, wazazi wamekuzaa wamekulea kwa shida hadi umekua, badala ya ujishughulishe upate kipato, bado unaendelea kuwatia wazazi mzigo wa kukulea jibaba zima la miaka 25 una ndevu hadi za huko chini, una msitu wa equatorial kabisa you are continue to stay at home without nothing you earn than to exploit your parents.

Upo tu, huna kazi yoyote unalala na kuamka tu, na kula na kugombea juisi kwenye friji, ni aibu, kwa mtoto wa kike ni sawa akibaki nyumbani,lakini dume zima aibu kabisa

Haijalishi kwenu mmendelea sana, ni wa kishua toka umezaliwa hujui shida lakini ukifikisha 25 years walau uanze kujishughulisha walau upate chochote kitu kwa maisha haya walau ucontribute chochote au uwe unaingiza chochote hata kama kwenu ni mambo safi.

Kuna mwingine alinijibu kuwa labda sio wote wametokea familia za tia maji tia maji, kwahiyo vijana maskini ndo wasikae majumbani akanirefer mimi kuwa huenda nimetokea familia ya shida ndo maana nasema hivyo

Personally mimi wala sio hivyo,kwanza nijieleze kuwa mimi ni nani kwetu tumezaliwa watatu, wasichana wawili na mvulana mmoja ambaye ndo mimi.

My sister wa kwanza kasoma ana masters yake ana kazi nzuri tu, na kaolewa na mtu ambaye yupo vizuri sana kiujumla wana maisha mazuri sana.

Wa pili ana degree kabahatika kupata kazi kwenye NGO's huko mshahara mnono, ana maisha yake ana mali zake hajaolewa hajazaa ila anamiliki nyumba,biashara na viwanja kadhaa.

Na home sio watu wa njaa wala nini,mimi ndo mtoto pekee wa kurithi mali, mzee na mama wana nyumba tatu, wana biashara ya duka, nyumbani mambo ni swafi, hawana shida, ishu niliamua kutoka home nikajipinde, kitu ambacho kilimuudhi sana mama na baba, na dada zangu, maana huwa wananiambia kwanini ninahangaika wakati mimi ndo mtoto pekee wa kiume?Kwanini nasumbuka?kwanini nisirudi nyumbani kila kitu kipo?Kwanini nisikae tu nyumbani nisubiri ajira au nikae tu na wazazi?kwanini naumiza kichwa wakati nyumbani nyumba zipo za kutosha hakuna walobaki nyumbani zaidi ya mzee na maza?

Wananiuliza kwanini niwe na mawazo ya kununua kiwanja changu mwenyewe na kujenga nyumba yangu mwenyewe wakati hayo majumba yote matatu wanayomiliki wazazi mwishowe ni yangu?

Kwanini nisirudi tu nyumbani nioe maisha yaendelee?kwanini najisumbua?

Hayo yote wananiuliza!Lakini mimi nataka nipambane niwe na vya kwangu mwenyewe ambacho nitakua nimekitolea jasho, hivyo vya wazazi nitapewa ndio, lakini lazima na mimi kwenye maisha yangu niseme kwamba pamoja na yote na mimi nilifanya jambo hili na lile

Haiwezekani una miaka 25 hadi 40 umekaa tu kwenu huna hata godoro, huchangii chochote upo tu unalala na kuamka unawatia wazazi wake gharama za kulitunza dume zima!Wazazi wako wamekulea tokea utotoni huko bado tena sahiv badala ya kuwaacha wapumzike kidogo we bado unawabebesha mizigo ya kukulea wewe dume zima!

Kuna mmoja kasema kwamba eti si wanilizaa wao?Haya ni mawazo ya kijinga sana, uendelee kuwaza hivyo hivyo kama hitazeekea kwenu nala maana hujafanya, hebu jishughulishe huko mwanaume nzima dume zima ni wa kumsumbua bi mkubwa wako kuomba hadi bando?ni aibu ya mwaka

Tatzo hampendi kuambiwa ukweli na ukweli ndo huo una miaka 25 na kuendelea hadi 40 umekaa kwenu unakula bure, kulala bure na huna mishe ya maana wewe ni mzigo kwa wazazi na hustahili kabisa wewe ni mnyonyaji,mvivu, na mtu usiyefaa wala kustahili kabisa
 
Inawezekanaje kijana ashatimiza miaka 25 na kuendelea do yupo kwao?

Miaka 25 huna hata godoro ndugu?Hata kitanda huna?Miaka 25 hata kujitegemea bado? Bado upo kwenu unagombea dawa ya meno na watoto wa ndugu zako kweli?

Vitu vingine ni vya ajabu sana na aibu siwakandii ila ndio kweli haiwezekani una miaka hiyo bado upo kwenu.

Kuanzia miaka 20 sio miaka ya kukaa nyumbani na kula ugali wa bure ni miaka ya kuanza kujitegemea na kujituma

Maana ukishafikisha miaka 25 bado upo kwenu na huna hata godoro kutimiza ndoto zako huko baadae ni ngumu kinoma.

Ni bora kuambiana ukweli, siwasemi wala siwafokei,na msijitie moyo kwa kuambiwa umri bado, sasa kama ndugu yangu wewe unajiona umri bado?Jee hao wenye miaka 14-18 years wasemeje?

Ni jambo la kijinga na udhaifu wa hali ya juu mtu ana miaka 25 bado hajajitegemea na hana chochote cha maana cha kujivunia.

Tunatengeneza taifa lenye vijana wa hovyo sana.
Hao watoto wadogo wa miaka 25 unataka waende wapi mkuu wakati kaka zao wa miaka 38 bado wapo hapo hapo home. Wengine wanadiriki kuolea hapo hapo na maisha yanasonga.
 
Ukiwa mzazi masikini sawa lazima umfukuze mwanao maana hata urithi tu wa kumpa huna.....chakula kupata tu shida yaani hata ukiona mwanao anatumia dawa ya mswaki ya buku mbili unaona Kama anafaidi au anakutia umasikini.....ukiwa masikini lazima uwe na roho mbaya......ILA KWA TAJIRI HATAKI MWANAE AONDOKE AKAKAE MBALI MAANA ATAKUTANA NA MASIKINI MTAFUNDISHA TABIA ZA HOVYO NA HATA AKIPATA URITHI ATASHINDWA KUUUENDELEZA MAANA ATAJIFUNZAJE BIASHARA ZA BABA YAKE ZINAENDESHWAJE WAKATI HAKAI NYUMBANI?......

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kijana anae chezea Ligi ya Uingereza (English premier league) ambae anaitwa Trent Alexander-Arnold ana utajiri wa euro milioni 3 kufikia 2022.
Kijana huyo mpaka leo muda huu anaishi kwa wazazi wake pindi tu apatapo mapumziko kutoka kutumikia ajira yake,na akiwa nyumbani anafanya shughuri zote za nyumbani kama kufua,kuosha vyombo usafi,wa bustani nk.
Dogo anaingiza mpunga mrefu na bado ana stay kwao iweje uje kuwasema vijana wa sa 100 ambao vipato vyao vinaisha kwa TOZOER eti watoke makwao wakapange yani wajitegemee,hivi unafahamu ya kuwa kuna TOZO anzilishwi juu ya wapangaji,acha mapepe wewe kama umetoka kwenu usilazimishe vijana wengine watoke makwao ikiwa wana jukumu la kujenga Taifa lao

NAOMBA NIWEKEE NUKTA
 
Acha kuwafokea watoto mbona mi nina miaka 48 na bado naish kwa baba na mama nina mpango nikifikisha miaka 50 nihamie kwa sista.
Kama ni kweli ulichoandika basi utakuwa na mtindio wa ubongo. Ila naamini siyo kweli. Umeamua kutuchekesha tu. Hata hivyo wengine tunashindwa kucheka, kwa kuwa tozo imetuondolea vicheko vyetu, tumebaki tunagugumia kwa maumivu
 
me naona kukaa nyumbani au kutokukaa ni swala la uwezo wa familia fulani na je unakaa kwa misingi ipi yupo mtu anakaa nyumbani kwao kwakua kuna biashara na familia inahitaji aziendeleze mwingine anakaa nyumbani kwakua yupo mwenyewe na wazazi wanaweza kumsupport kibiashara ila wanahitaji awepo kuongeza namba ya watubwenye familia wasiwe wapweke. Mwingine anakaa nyumbani kwakua kuna kipato na anajipanga kufanya mambo yake.
hivyo bas kukaa nyumbani sio tatizo na huwez kaa kwenu ukasema unanunua godoro wakati lipo sjui jiko wakati lipo home hivyo ni mipango na uwezo wa familia.
wengi wetu tumetokea familia za kifukara sana hivyo ukishaweza kutafta hela lazima utoke ukatafute tofaut na wakishua akatafute nn wakati biashara zipo mali zipo ni yy kuziendeleza.
tukumbuke sisi ni waafrika sio wazungu tuna ule utamaduni wa kulea mtoto mpka akiwa mtu mzima tofaut na wenzetu ukifikisha 18 nenda kajiftaftie ndio maana afrika bado tuna utamaduni wa kurithisha mali kwa watt wetu
 
Inawezekanaje kijana ashatimiza miaka 25 na kuendelea do yupo kwao?

Miaka 25 huna hata godoro ndugu?Hata kitanda huna?Miaka 25 hata kujitegemea bado? Bado upo kwenu unagombea dawa ya meno na watoto wa ndugu zako kweli?

Vitu vingine ni vya ajabu sana na aibu siwakandii ila ndio kweli haiwezekani una miaka hiyo bado upo kwenu.

Kuanzia miaka 20 sio miaka ya kukaa nyumbani na kula ugali wa bure ni miaka ya kuanza kujitegemea na kujituma

Maana ukishafikisha miaka 25 bado upo kwenu na huna hata godoro kutimiza ndoto zako huko baadae ni ngumu kinoma.

Ni bora kuambiana ukweli, siwasemi wala siwafokei,na msijitie moyo kwa kuambiwa umri bado, sasa kama ndugu yangu wewe unajiona umri bado?Jee hao wenye miaka 14-18 years wasemeje?

Ni jambo la kijinga na udhaifu wa hali ya juu mtu ana miaka 25 bado hajajitegemea na hana chochote cha maana cha kujivunia.

Tunatengeneza taifa lenye vijana wa hovyo sana.
MKUU,
KITENDO CHA WEWE KUNUNUA GODORO LA FUTI 2 NA NUSU ND'O KINAKUPA UHURU WA KUTUKANA MALEJENDARI HUMU?!

HUU UHURU UMEPITILIZA SANA NCHI HII!!!
 
Ni kweli kwa mtu uliezaliwa familia masikini ni mzigo kuendelea kuwa kwenu na una zaidi ya miaka 18+ unainyonya familia,

Ila upande wa pili tunaona raha sana ndg tunapojumuika pamoja, ni furaha sana aiseee maana kama ni kazi tunafanya pamoja uchumi tunakuza pamoja

Hebu ngoja nkupe tofauti kidogo iko hiviii mimi kipato changu ni 20k kwa siku kuna mda napita wiki nzima sijatoa chochote kwenye pesa yangu nakula kwa mzee nalala kwa mzee, hapa nafanya kazi kwenye miradi ya mzee na nina vimiradi vyangu ambavyo ndio hivyo vinaniingizia hiyo 20k per day

Ninaweza kulingana na wewe ambaye unaingiza 20k hiyo hiyo kama mimi ulipe kodi, ununue chakula, usafiri nk?

Hata biashara zenu zinakufa sana kwa sababu unaifungua leo na unaanza kuitegemea leo leo unatokaje nyumbani ukiwa huna misingi? Achen ulimbukeni jipange vzr mambo yakiwa sawa toka nhumbani sio utoke tu na hauna kitu kisa umri!
 
Izo Mila za kipumbavu mtoto umemzaa bila ya ridhaa yake leo unataka akajitegemee!! Una akili timamu kweli?

Waarabu wanazaa watoto mpaka wanawaozesha wanakaa kwao mpaka wafanye maamuzi ya kuondoka ....leo mwanao anajifanya kapata bodaboda eti anajiweza anaenda kukaa mageto uchwara kuendekeza Uzinzi tu, wengine wanaume kwa wanaume wanapakauna tope huko magetoni sio salama!!

Usiforce life liwe vile unataka pambana na kwenu hakuna tajiri anapenda mwanae ateseke sema ngozi nyeusi akili hatuna.
 
Back
Top Bottom