Ukishafikisha miaka 20 na kuendelea na bado unawategemea wazazi kwa asilimia 100, umekwisha

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
3,086
2,000
Una miaka kuanzia 20 na kuendelea na bado unategemea wazazi kwa asilimia 100 jitafakari sana wewe bila hivyo utaishia pabaya.

Nimesema asilimia 100 wapo wanaopambana wanategemea asilimia kadhaa tu na asilimia kadhaa wanajimudu hawa wana muelekeo nzuri.

Wapo wanaojimudu 100% kila kitu hawa ndo wanaoelekea pazuri.

Lakini una miaka kuanzia 20 mpk 35 unategemea kwenu nenda ukaombewe na ni aibu na kinyaa kukuta mtu nzima kijana una nguvu lakini unakula kwenu bure, kulala bure, kila kitu kwenu na huzalishi hata hamsini ujitafakari sana maana utaishia pabaya sana na maisha yako yatakua ya shida tu.

Kujitegemea kuanzia miaka 20 ni lazima kwa kila kijana hususan vijana kiume.
 

October man

JF-Expert Member
Nov 23, 2017
3,702
2,000
Ungesahau kuweka iyo asilimia (%) ningekuona hauna akiri timamu, once umeweka asilimia naungana na andiko lako.

Na nahisi hakuna kijana wa aina huyo aliyekaa tu anategemea wazazi 100% labda awe hana akiri timamu au mgonjwa wengi hasa waliocheleweahwa na elimu wanamaliza miaka 26..27 wanategemea wazazi kwa asilimia chache sana maana ndio wako kwenye kuchomoka bado hawajawa stable sana.
 

MENISON

JF-Expert Member
Apr 26, 2013
674
1,000
Mwanangu akishafikisha 23 na anajielewa..nitamtoa kwangu hata kwa tarumbeta.
Mwanangu wa kiume na miaka 6, akimaliza shule popota atakapoishia ntamtoa nyumbani akapambane huko akapata akili. Akikaa nyumbani hapati changamoto, nampa kahela kidogo kakuanzia. Ila wa kike kama hana muelekeo na hapati mume bora nizeekee nae nyumbani kwangu na sio nimfukuze akajiuze huko kwenye mabaa.
 

GODZILLA

JF-Expert Member
Dec 26, 2014
4,894
2,000
Usiwa-frustrate vijana. Kila mtu ana wakati wake wa kupata mafanikio ya kimaisha.

Vibwana mdogo kama wewe vikishapata tumia mia na tuhela twa mkopo mnakuwa na majigambo sana kwa wenzenu.

Ndio maana suicide rates zimeongezeka kwa sababu ya mgandamizo wa jamii dhidi ya vijana na expectations zisizo na uhalisia juu yao.

Tunapopambana na suicide cases lazima tuanze na ninyi motivesheno spika uchwara mnaowajaza vijana illusions na hofu za kufeli.

Stay low key!

Bado sana wewe! Bado mno!
 

October man

JF-Expert Member
Nov 23, 2017
3,702
2,000
Mwanangu akishafikisha 23 na anajielewa, nitamtoa kwangu hata kwa tarumbeta.
Unaandika kwa kutumia ubongo wa kichwani, miaka 23 ni kijana wa mwaka wa 2 au wakwanza chuoni endapo anasoma unamfukuza nyumbani kwamaana gani pia naweza kukuunga mkono endapo umemuandalia Mtaji au network za ajira za kueleweka, mbali na hapo ni baba wa hovyo.

Pia tusikariri kuwai kujitegemea hai guarantee kufanikiwa mapema anaweza mtu ukamtangulia ana akakutoa knock out vizuri tu.
 

yna2

JF-Expert Member
Aug 18, 2018
16,554
2,000
unaandika kwa kutumia ubongo wa kichwani, miaka 23 ni kijana wa mwaka wa 2 au wakwanza chuoni endapo anasoma unamfukuza nyumbani kwamaana gani pia naweza kujiunga mkono endapo umemandalia Mtaji au network za ajira za kueleweka, mbali na hapo ni baba wa hovyo.

Pia tusukariri kuwai kututegemea hai guarantee kufanikiwa mapema anaweza mtu ukamtangulia ana akakutoa knock out vizuri tu.
Miaka 23 mtoto wangu atakuwa ameshamaliza chuo..na kwa muda huo nitakuwa nimemuandalia mazingira mazuri.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom