NMB ni Benki nzuri iliyoenea Tanzania na kwa maana hiyo ni kimbilio la wananchi wa kawaida na wenye kipato cha chini. Pamoja na hayo kuna baadhi ya kero ambazo si za lazima lakini baadhi ya watumishi wa NMB wanazifanya kuwa za lazima na hivyo kutufanya wateja wake kupoteza muda mwingi kutatua matatizo ambayo hayatokani na wateja.
Ikiwa January 2013 nilikerwa na Customer care Manager wa Tawi la Kenyatta na nikalazimika kuachana nae na kupanda First Floor kumtafuta Branch Manager ndo nikakutana na mtumishi mmoja wa Bank ambaye alionesha kugushwa na tatizo langu na akanielekeza chumba cha Branch Manager pale Kenyatta. Nikashuka kuonana na Branch Manager lakini juhudi zangu hazikufanikiwa kwa maana muda wangu ulikuwa limited na tayari kulikuwa na mtu ndani ambaye kwa haraka haraka alichukua takiribani 1hrs akiongea na Manager hivyo nikaamua kuondoka. Tatizo langu lilitatuliwa kwa urahisi sana na Customer Care Manager wa Branch nyingine.
Nilidhani ni mimi tu lakini kumbe tupo wengi..kuna ndugu yangu ambaye kwa mujibu wa kazi yake lazima mshahara wake upitie NMB lakini ajabu ni kwamba juzi amekuta salio la Akaunti yake lina -650,000Tsh. Katika harakati za kufatialia akaambiwa pesa imetolewa pale Kenyatta road branch. Sasa badala ya Bank kumsaidia, amezungushwa mara Misungwi Branch, mara kachukue PF3 Polisi lakini baada ya kupata PF3 anaambiwa hawezi kusaidia mpaka Polisi mwenye faili lake ndo aende ili aonyeshwe picha za yule aliye withdraw pesa yake...lakini kama tunavyowajua Polisi wetu nadhani ndugu yangu hajaelewa nini Polisi anataka maana anapigwa danadana hadi amechoka lakini tukumbuke hiyo ndiyo akaunti yake ambayo mshahara wa Serikali unapitia, sasa sijui kama mshahara wa mwezi huu utasalimika.
Kesi kama ya huyu ndugu yangu pia imewahi kumkuta rafiki yangu ambaye pesa yake 200,000/= pia ililambwa pale Mlimani City lakini kwa staili ile ile ya kuelezwa aende polisi, ni kweli alienda Majumba Sita lakini kwa kuwa Polisi aliyepewa kufuatilia hiyo kesi nae alitaka kupewa kitu kidogo, basi huyu rafiki yangu alilazimika kusamehe mpaka leo.
Lakini kama siyo double standard ni nini? maana kuna jamaa aliibiwa pesa pale pale NMB Kenyatta ATM lakini hakuambiwa kuliport Polisi bali yeye aliambiwa kwenda kwenye Tawi lake la NMB ili akapate Bank Statment na aipeleke kwa Branch Manager na ndani ya siku tatu akapigiwa simu kuwa pesa yake imerudi.
Jamani binafisi hii connection na Polisi wetu inakera sana na mwisho wa siku tunapoteza zaidi. ni bora Bank ikaangalia namna zingine sahihi za kutatua kesi zao bila kuwatumia hawa watu wanaitwa Polisi au kuwe na mawasiliano kati ya Benki na Polisi na isiwe Polisi na Mteja.