Ukipendwa kweli thamini muda na upendo wa mwenzio

Ukipendwa kweli thamini muda na upendo wa mwenzio

Nazidi kuyaona matokeo ya walioshika pesa Ukubwani. Utakula ulikopeleka mboga.
 
Sijaji victimize mkuu nimejaribu kuwa muwazi hapa. Ilifikia maamuzi ya kumwambia tuachane baada ya kuona kuwa ni kama namtesa na mimi lazima kazi nifanye na kila nilipokuwa namweleza ukweli ni kama hakuridhika kuwa mvumilivu.
Mhmh! Kazi...! Kazi ipi hiyo ambayo ilikuafanya usipate hata muda wa kumjulia hali umpendae
Inaonesha huna hofu na Mungu na pia baado ujana unakusumbua
 
Waliosema 'Bahati hairudi mara mbili' hawakukosea. Umelikoroga, sasa itabidi ulinywe. Kila kinachoendelea unastahili kukipata kwani ulichomfanyia mwenzio ni ukatili na unyama wa hali ya juu. You deserve it. Yawezekana unastahili msamaha lakini haina maana kwamba unastahili kurudiana naye. Binti amejilipua maisha yake kwa ajili yako!! Amekupa moyo wake wote na wewe unaufinyanga kisa uko busy!!??? Yaani uko busy kiasi cha kukosa hata dakika tano kwa siku kumjulia hali mtu aliyekuwa tayari kuacha imani yake kwa ajili yako?? Unajua maana ya mtu kubadili dini kwa ajili yako wewe!!?? Ina maana alikuwa tayari kuikana na kuisaliti familia yake kwa ajili yako wewe!? Ningemfahamu ningempa kumi zake, anastahili pongezi kwa kuwa na msimamo thabiti, atakuwa mjinga kukurudia wewe, baada ya ujinga wote uliomfanyia. Habari njema ni kwamba tayari ameshapata mwingine kuziba pengo lako. Yawezekana mateso uliyompa yamemsaidia kujifunza na anaweza kuishi kwa amani sasas kuliko alivyokuwa na wewe. Kama ameshakuambia kwamba ana mtu, nawe bado unaendelea kumng'ang'ania maana yake humheshimu, pamoja na kumkosea kote huko bado unajiona wewe ndiye unayestahili kuonewa huruma na mapenzi yarudi kama kawaida - Just like that!!

Ushauri
Kama unampenda kweli maana yake unapaswa kuheshimu uamuzi wake. The best thing you can is to LEAVE HER ALONE.
 
Distance nayo ni chanzo dada sio issue ya kazi na pombe tu. Tungekuwa tunaishi pamoja wala tusingefika huku kote.

Kuhusu pesa wala hajawahi kuomba hata mia na sio kwamba anashida sana no kwao wapo vizuri tu na ndio maana kuna kipindi akawa ananitumia yeye hela.
Kwahiyo kijana kumpa mpenzi waako hela hadi akuombe!!
Mi nilidhani baaada ya wewe kupata kazi nzuuri angefrahia matunda ya kazi yaako badala yaake inaishia kupata maumivu!!!?
Just think ungelikua ni wewe!.
 
Kubali kataa mkuu hawezi kurudi maana hata mimi nilikuwa na mpenzi aina hiyo nikaleta ujinga nimeombewa msamaha hadi na mama yangu mtoto kakataa so nimekubali yaishe na wewe kubali yaishe
 
Yes iyo hutokea na faudhia kasha move on na ata akikuludia hatakua real....
 
wewe ukumpenda huyo mwanamke kwa maana nijuavyo mtu unayempenda kazi haiwezi ikafanya umsahau na pia kazi haina nguvu kwenye mapenzi ya kweli

alaf unadai et ni wife material kwako na wakati ulisema humfai we jamaa wewe mh
 
Ukipata kazi nyingine ya kuwa busy je? Na yeye muda huu yuko busy. Zamu yako sasa kuisoma namba, malipo ni hapahapa duniani.
Siwezi kuipata hiyo kazi kwasababu sitafuti kwa sasa. Hivyo nina uhakika kuwa kwa sasa nipo free sana
 
Humfai huyo binti na kama kashakuambia ana mtu mwingine mwache aendelee n maisha yake...ulipendwa sana ila hukupendeka...sasa umeachwa kubali kuachika ebooh!
Basi nipe hiyo nafasi mkuu maana hapa nilipo nipo kwenye hali mbaya sina mtu wa kuwa karibu nae sina nimpendae wakuniliwaza
 
Kupenda ni rahisi mno kama ilivyo kupendwa. Challenge ni kupendana regardless kipato,lifestyle na kadhalika.
Kupendana kupo ila kuna changamoto za kimaisha zinazoweza kufanya upendo usipaliliwe na kukua zaidi
 
Umeitimisha vizuri,siku zote husipokuwa makini na umaarufu,pesa,elimu mwisho wake si mzuri,kwani utajithamini sana kuliko upande wako wa pili na hatimae Mungu huwa anafungua macho yako yaliyokuwa yamefungwa na shetani ili ujifunze vizuri kuishi maisha ya upendo na imani kwa badae
Asante kwa maneno yako mkuu
 
Basi nipe hiyo nafasi mkuu maana hapa nilipo nipo kwenye hali mbaya sina mtu wa kuwa karibu nae sina nimpendae wakuniliwaza
Mimi nshapendwa na nikathamini upendo hadi nkafunga ndoa na sijawahi juta . .pole sana jipe muda na ufanye ibada pia omba msamaha wa dhati kwa huyo bibie ili uwe huru ..kama ni wako atarudi na asiporudi utampata unaestahili
 
Nazidi kuyaona matokeo ya walioshika pesa Ukubwani. Utakula ulikopeleka mboga.
Sio ukubwani mkuu labda useme utotoni maana umri nilionao na hela niliokuwa napata na majukumu niliyokuwa nayo wala vilikuwa haviendani kabisa.. <23 ila kwa mwezi nilikua namake hela nyingi na sina mtegemezi sio mzazi wala mpenzi ni vile vizinga vya marafiki na ndugu tu vya elfu tano au kumi.
 
Mhmh! Kazi...! Kazi ipi hiyo ambayo ilikuafanya usipate hata muda wa kumjulia hali umpendae
Inaonesha huna hofu na Mungu na pia baado ujana unakusumbua
nimeeleza hapo mkuu, kuna kazi nyingine nature yake inakufanya unakuwa mchovu kutwa nzima upo site jua kali japo unapata hela ila unachoka sana. Ndio maana nilikuwa narudi nakunywa zangu nalala ili kesho niwahi tena job
 
Waliosema 'Bahati hairudi mara mbili' hawakukosea. Umelikoroga, sasa itabidi ulinywe. Kila kinachoendelea unastahili kukipata kwani ulichomfanyia mwenzio ni ukatili na unyama wa hali ya juu. You deserve it. Yawezekana unastahili msamaha lakini haina maana kwamba unastahili kurudiana naye. Binti amejilipua maisha yake kwa ajili yako!! Amekupa moyo wake wote na wewe unaufinyanga kisa uko busy!!??? Yaani uko busy kiasi cha kukosa hata dakika tano kwa siku kumjulia hali mtu aliyekuwa tayari kuacha imani yake kwa ajili yako?? Unajua maana ya mtu kubadili dini kwa ajili yako wewe!!?? Ina maana alikuwa tayari kuikana na kuisaliti familia yake kwa ajili yako wewe!? Ningemfahamu ningempa kumi zake, anastahili pongezi kwa kuwa na msimamo thabiti, atakuwa mjinga kukurudia wewe, baada ya ujinga wote uliomfanyia. Habari njema ni kwamba tayari ameshapata mwingine kuziba pengo lako. Yawezekana mateso uliyompa yamemsaidia kujifunza na anaweza kuishi kwa amani sasas kuliko alivyokuwa na wewe. Kama ameshakuambia kwamba ana mtu, nawe bado unaendelea kumng'ang'ania maana yake humheshimu, pamoja na kumkosea kote huko bado unajiona wewe ndiye unayestahili kuonewa huruma na mapenzi yarudi kama kawaida - Just like that!!

Ushauri
Kama unampenda kweli maana yake unapaswa kuheshimu uamuzi wake. The best thing you can is to LEAVE HER ALONE.
Asante mkuu kwa ushauri nitaongea nae tena mara ya mwisho kama kweli amepata huyo mtu basi nitafanyia kazi ushauri wako
 
Kubali kataa mkuu hawezi kurudi maana hata mimi nilikuwa na mpenzi aina hiyo nikaleta ujinga nimeombewa msamaha hadi na mama yangu mtoto kakataa so nimekubali yaishe na wewe kubali yaishe
Dah
 
Back
Top Bottom