Sio ukali.. Sijaamua kuremba maneno maana inaonekana unajiendekeza na kutafuta sababu mfu za kuhalalisha ulichokifanya ...hata Mimi nishaharibu sana na kuvunja mioyo ya watu lakini sikuwahi kujitoa ufahamu hata kudharau MTU aliye tayari kujitoa uhai , Huyo binti yupo sahihi kukusumbua na akikutaa pia anastahili. Hivi unahisi hao ndugu zake wanamuonaje kwa alivyoyaona maisha magumu bila ya wewe au hiyo attempt ya kujiua
Ngoja tu nikuambie ukweli.. Aidha ni kweli kakuacha mazima au bado anakupenda lakini hayupo tayari kuchukua risk kubwa kwa mtu asiye na moyo kama wewe.. Jaribu kuvaa viatu vyake na uone kama ni rahisi kumrejea MTU aliyekutesa kiasi hicho
Narudia..cha kwanza kubali makosa na uache hivyo visingizio vya kitoto, kama vilikufanya uharibu its fine lakini kwake ni kama unamkumbusha kuwa yeye ni kitu extra tu katika maisha yako yaani ukipata pesa tu utamzingua.. Acha visingizio and take full responsibility.hapo ndo pakuanzia