Ukipendwa kweli thamini muda na upendo wa mwenzio

Ukipendwa kweli thamini muda na upendo wa mwenzio

Kwa uzi huu tegemea kuona warembo pm huko shida yao hela tu hizo mupombe na dharau zako watakuachia mwenyewe
 
We jamaa ni selfish kama wabunge wa ccm! She deserve some one better than.mwache a enjoy wewe karuke na pombe na malaya.
Wanaume wengine aisee hawafai
 
Pambana na hali yako. Muache mwenzio na maisha yake ewe kivuruge.
Mkuu naomba nipe ushauri nimpe maneno gani ili niweze kumrudisha ili nimpe upendo wa dhati
 
Kwa uzi huu tegemea kuona warembo pm huko shida yao hela tu hizo mupombe na dharau zako watakuachia mwenyewe
Hapana mkuu sio lengo la huu uzi. Hapa nilipo hata usingizi sipati namuwaza Faudhia
 
Safi sana umevuna ulichopanda

Ila kuna me wanaringa jamani, unajitahidi kumthamini na kumjali lkn anajikuta nani sijui mxiew
Haikuwa nia yangu mkuu. Ni hali ya maisha tu
 
Hehehehee,......mazoea tu ndiyo yanakutesa.....
Kwa kuwa ushakikoroga,move on na maisha tu....
 
Usihukumu haraka hivyo mkuu. Sio kwamba nilimziria bali ukweli nikuwa kazi iliniweka busy sana hivyo nikawa nakunywa ili nilale nisiweze kwenda kuhangaika na wanawake wengine kwakuwa ninampenda na ndio maana sikukaa bar nikawa nakunywa zangu ghetto.
Ukipata kazi nyingine ya kuwa busy je? Na yeye muda huu yuko busy. Zamu yako sasa kuisoma namba, malipo ni hapahapa duniani.
 
Humfai huyo binti na kama kashakuambia ana mtu mwingine mwache aendelee n maisha yake...ulipendwa sana ila hukupendeka...sasa umeachwa kubali kuachika ebooh!
 
Habari za asubuhi wakuu, natumaini wote mmepata usingizi mzuri tofauti na mimi ambaye sijaupata takribani siku mbili sasa.

Mkasa wangu unahusiana na huyu binti ni jirani yangu, tulitokea kupendana sana mwaka 2016 mwanzoni ndio ilikuwa mwanzo wa safari yangu mimi na yeye.

Kusema kweli mtoto ni mzuri sana mweupe peeee alafu kimo cha wastani na umbo la kibantu. Japo yeye ni muislam na mimi ni mkristo nilifanikiwa kumshawishi hadi akaanza mafundisho yasiyo ramsi kwaajili ya kubadili dini. Alijifunza sana kwa bidii kwa nia ya kutimiza ndoto zake za kuolewa na mimi mseminary niliekatiwa jina la paroko mtaani kwa sifa za upole na heshima.

Changamoto zilianza pale nilipomaliza chuo nikapata tempo kwenye shirika moja la umma na nikahama mkoa (Arusha) nikahamia Dar, hapo nikawa napewa kazi ( kazi za site) kila siku hakuna kupumzika, hakuna sikukuu hakuna weekend. Kwa mnaojua nikisema hivyo sio kwamba unakua unateseka hapana ni raha maana unapata OT zakufa mtu na mkwanja unaushika sana.

Nilipata mkwanja sana mpaka nikaanza kunywa pombe na matumizi yasiyo na tija yani ukija kwangu nina viatu karibia pair 50 vingine hata sijawahi kuvivaa tokea nimevinunua, vikorokoro ya electronics vingine hata sijui kuvitumia.

Yule mpenzi wangu alikua akinipigia kila siku nakuwa busy sana sipati hata muda wa kujibu simu zake wala sms. Alikuwa ananipigia kila siku na text mpaka wakati mwingine anawatumia ndugu zangu kunitafuta ila kazi na pesa zilinilevya kiasi sikuwa na muda nae kabisa na hata nilipoongea nae nilikua mkali sana nikisingizia kazi na uchovu. Huyu mtoto alinivumilia ila bado akawa ananisumbua ikafikia hatua nikaona kama namtesa ikabidi nimwambie tuachane atafute mtu mwingine mimi simfai.

Kitendo hiki kilimfanya huyu mtoto anywe sumu na aliokolewa na ndugu zake, siku hiyo nilipigiwa sana simu mpaka nikapokea nikaongea nao yakaisha ila baadae hali ilijirudia nikamkatia mawasiliano nikimwambia sitaki kuwa nae tena.

Wakati huo sio kwamba nilikua na wanawake wengine hapana nilikua busy na hela na kazi huku kila nikitoka kazini nanunua mizinga nikifika ghetto nalewa tu wala simu siwezi kutumia nazima tu kila saa moja usiku. Hela nikawa nagawa hovyo kwa kila alieomba na ubaya huyu mtoto hajawahi kuniomba hata vocha ya jero sana sana mimi nilikua nampima kuwa sijala sina hela akawa ananitumia hela ambayo hata kabla sijaitoa nilikua natumia waliokuwa wananipiga vizinga.

Sasa shida imekuja kuwa hivi karibuni nimeacha ile kazi na nimeamua kufanya mambo yangu mwenyewe hivyo nina muda wa kutosha. Nimemtafuta yule binti ili nikoleze upendo ila niliyokutana nayo yameniumiza mpaka sasa siamimi. Anasema ana mtu na wala hataki kunisikia kwakuwa nilimuumiza sana. Nimemlilia kila kilio mpaka kumtisha kuwa nitakufa ila amesema "sawa kufa tu hutakuwa wakwanza kufa" [emoji174]

Kiukweli nimejieleza kuwa ilikuwa hali ya maisha tu iliyonifanya nifanye vile ila hataki kabisa kunielewa kiasi imepelekea ametupa line yake ya mwanzo ila nimeipata namba yake mpya nayo hali imekuwa tete mpaka nimekata tamaa. Kinachouma huyu mtoto ni wife material na sijawahi kuona mwanamke ambae ananifaa zaidi yake. [emoji174][emoji174] kwakweli majibu anayonijibu ni dhahiri hana hata chembe ya upendo kwangu tena. Nimemsumbua kila siku karibu mwezi sasa lakini bado ni unbreakable.

Imefikia hatua nimechukia hata wale walionipa hii kazi na hela nilizokuwa nazipata maana saizi zimefanya naishi kama shetani kwenye ghetto langu. Nifanye nini wakuu ili niweze kuurudisha moyo wa huyu binti kwangu maana nampenda sana ila ni hali ya maisha na wenge la hela lilinishika.

USHAURI

Ukipendwa jitahidi ku reciprocate (hata kinafki tu kama huwezi kuwa real). Jitahidi kujali upendo na muda wa anayekupenda. Wengi wetu tunajikuta tunashikwa sana na mambo mengine na kushindwa ku balance masuala muhimu maishani..

Trust me hata uwe na hela kiasi gani huwezi kuwa na furaha kama moyo wako unapata tabu sana.



Nisamehe Faudhia, ni hali ya maisha tu ilosababisha sio kuwa sikuwa nakupenda. Nipe nafasi ya mwisho.
Kupenda ni rahisi mno kama ilivyo kupendwa. Challenge ni kupendana regardless kipato,lifestyle na kadhalika.
 
Sio ukali.. Sijaamua kuremba maneno maana inaonekana unajiendekeza na kutafuta sababu mfu za kuhalalisha ulichokifanya ...hata Mimi nishaharibu sana na kuvunja mioyo ya watu lakini sikuwahi kujitoa ufahamu hata kudharau MTU aliye tayari kujitoa uhai , Huyo binti yupo sahihi kukusumbua na akikutaa pia anastahili. Hivi unahisi hao ndugu zake wanamuonaje kwa alivyoyaona maisha magumu bila ya wewe au hiyo attempt ya kujiua

Ngoja tu nikuambie ukweli.. Aidha ni kweli kakuacha mazima au bado anakupenda lakini hayupo tayari kuchukua risk kubwa kwa mtu asiye na moyo kama wewe.. Jaribu kuvaa viatu vyake na uone kama ni rahisi kumrejea MTU aliyekutesa kiasi hicho

Narudia..cha kwanza kubali makosa na uache hivyo visingizio vya kitoto, kama vilikufanya uharibu its fine lakini kwake ni kama unamkumbusha kuwa yeye ni kitu extra tu katika maisha yako yaani ukipata pesa tu utamzingua.. Acha visingizio and take full responsibility.hapo ndo pakuanzia
Sahihi kabisa
 
Umeitimisha vizuri,siku zote husipokuwa makini na umaarufu,pesa,elimu mwisho wake si mzuri,kwani utajithamini sana kuliko upande wako wa pili na hatimae Mungu huwa anafungua macho yako yaliyokuwa yamefungwa na shetani ili ujifunze vizuri kuishi maisha ya upendo na imani kwa badae
 
Back
Top Bottom