Ukipata taarifa za mshahara mpya usikose kutujuza wenzako....

Ukipata taarifa za mshahara mpya usikose kutujuza wenzako....

mpasta

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2011
Posts
920
Reaction score
2,009
Wadau ambao ni watumishi wenzangu wa umma, tuna kumbukumbu nzuri tu ya kusugua miaka 6 mfululizo bila ongezeko la mshahara hata thumni. Lakini Rais wetu mpendwa wa Awamu ya sita Mama Samia Suluhu Hassan kaupiga mwingi sana. Kasikia kilio chetu katika nyongeza ya mshahara ya asilimia 23.3 kwa kina cha chini kwenye bajeti ya 2022/2023.

Wanasheria wana msemo wao wanasema "Justice delayed is justice denied"(Haki iliyocheleweshwa ni kama haki iliyonyimwa) lakini si haba, bora tu alivyotukumbuka sisi Watumishi wa umma ambao maisha yetu kwa ujumla kuanzia kula, kuvaa, kujenga, kusomesha, n.k kwa zaidi ya asilimia 85 yanategemea mishahara tunayolipwa na muajiri wetu serikali.

Sasa kujiandaa kupokea mshahara mpya, tayari asubuhi hii kabla hawajaenda shule, nimewasomea risala watoto wangu. Nimewapiga marufuku kuchezea simu yangu nikirudi kazini jioni. Maana naogopa watamaliza chaji nishindwe kupata taarifa za mshahara mpya kwa wakati, niliousotea kwa miaka 6 mfululizo [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Hivyo mdau na wewe ukipata taarifa za mshahara kusoma kwenye akaunti usikose kutujuza hapa jamvini.

NB;Naomba MOTIVATION SPEAKERS, na wale wazee wa NJE YA BOX sijui kufanya nini mpite wima kwenye huu uzi wa mkesha wa mshahara mpya haiwahusu kabisa. Mahubiri yenu mazuri sana ila hapa sio sehemu yake[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Wadau ambao ni watumishi wenzangu wa umma, tuna kumbukumbu nzuri tu ya kusugua miaka 6 mfululizo bila ongezeko la mshahara hata thumni. Lakini Rais wetu mpendwa wa Awamu ya sita Mama Samia Suluhu Hassan kaupiga mwingi sana. Kasikia kilio chetu katika nyongeza ya mshahara ya asilimia 23.3 kwa kina cha chini kwenye bajeti ya 2022/2023. Wanasheria wana msemo wao wanasema "Justice delayed is justice denied"(Haki iliyocheleweshwa ni kama haki iliyonyimwa) lakini si haba, bora tu alivyotukumbuka sisi Watumishi wa umma ambao maisha yetu kwa ujumla kuanzia kula, kuvaa, kujenga, kusomesha, n.k kwa zaidi ya asilimia 85 yanategemea mishahara tunayolipwa na muajiri wetu serikali.

Sasa kujiandaa kupokea mshahara mpya, tayari asubuhi hii kabla hawajaenda shule, nimewasomea risala watoto wangu. Nimewapiga marufuku kuchezea simu yangu nikirudi kazini jioni. Maana naogopa watamaliza chaji nishindwe kupata taarifa za mshahara mpya kwa wakati, niliousotea kwa miaka 6 mfululizo [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hivyo mdau na wewe ukipata taarifa za mshahara kusoma kwenye akaunti usikose kutujuza hapa jamvini.
NB;Naomba MOTIVATION SPEAKERS, na wale wazee wa NJE YA BOX sijui kufanya nini mpite wima kwenye huu uzi wa mkesha wa mshahara mpya haiwahusu kabisa. Mahubiri yenu mazuri sana ila hapa sio sehemu yake[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nyongeza not based kwenye 23.3%, Nyongeza ni 10,000-50,000 pekee!!
 
Wiki ngumu sana hii. Maafisa utumishi wametingwa kweli kweli kupeleka check za malipo benki.

Huenda kesho Ijumaa mzigo ukaingia kwenye akaunti. Hivyo team mshahara, muwe na imani. Kwa wale wenzangu wa viti virefu, ikiwezekana nendeni tu mkaweke bill kwa ajili ya kumwagilia moyo.
 
Back
Top Bottom