Ukipata milioni unaila siku tatu, ikibaki elfu kumi unaishi nayo week. Hii kitaalam mnaiitaje?

If the money you have can’t solve the probs you have eat that money 😂😂
No, it is not true. Eating money will not solve any problems you may have. Money is a form of currency that is used for transactions and as a medium of exchange. It has value because people agree to accept it in exchange for goods and services. Eating money will not address the underlying issues or challenges you may be facing. Instead, it is important to seek appropriate solutions and strategies to tackle your problems. This may involve seeking advice, support, or taking practical steps towards resolving the issues you are facing.
 
Tumia pesa ikuzoee Mnyampaa.

Pesa Ina kanuni na taratibu zake, haijalishi una Elimu Gani ukizifuata, haitakuangusha.

Kama hauna mipango na malengo, utafanya chochote unachomudu Kwa pesa uliyonayo Kwa wakati huo.

Mwisho wa siku, pesa hua haitoshi, ni wewe kuamua ukipata, ifanye vitu gani vya muhimu.

Kuna mtu akiwa na 1M haujui, akiwa na 10k haujui, Yuko vilevile. Lakini mwingine alipata 50k siku hiyo hamnywi maji, ni fujo za hatari. Mtu wa aina hiyo hata umpatie pesa kiasi Gani, atatapanya tu.

Kutafuta na kupata pesa ni jambo Moja, kuitunza ikaongezeka ni kitu kingine kabisa na sio Kila mtu anaweza.
 
Mchoro umetiki umepata kazi ukalipwa million hela haichukui siku mbili ya tatu chali umebaki na hewa hamna kitu ila ka elfu ulichobakiza kanadumu hata siku nne bila shida, unakabembeleza leo 2000, kesho umetumia 3000 keshokutwa 3000 na nyumbani hutoki siku nzima.

Kwanini hatuna ile roho ya kwamba hela imeingia Tayari ni yangu kwa sasa niachane nayo hiyo millioni nianze kusuka michongo mingine ya kupata nyingine.Hata kama kazi na bata ila million nyingi ukiwekeza kula nyama Choma na vya kunoga noga walahu ufaidi hata week tatu basi ila Duuh sio poa yaani siku tatu unabakia lofa.
Dawa ya hii ni kuwa na mkopo ukiwa Na mkopo kamwe hutatumia pesa ovyo
 
Dawa ya hii ni kuwa na mkopo ukiwa Na mkopo kamwe hutatumia pesa ovyo
Madeni mabaya yanaweza kukusababisha ukapoteza hata ulivyo navyo. Nidhamu ya fedha ni muhimu sana binafsi nilikuwa mwepesi sana kutoa fedha hata kwa mtu nisiemjua (kama msaada) ila nikafika mahali nikaona natumika vibaya na nikiwa nacho kumnyima mtu siwezi. Nikaja na mbinu nikafungua fixed a/c kila nikipata hela 75% naweka hiyo 25% inabaki kwa matumizi mengine, kuna muda napigika ila sina stress kwa sababu najua yajayo.
Mikopo sio sahihi sana kuna kipindi nilikopa alafu rejesho nategemea biashara, biashara nayo ikayumba acha kabisa omba yasikukute, nilivyomaliza lile rejesho kwa hali ilivyokuwa sikuamini.
 
ukiona ivo ujue hujazoea kushika iyo milioni, tuelfu kadhaa ndo level zako.

mtu yeyote ambae hajawahi kumiliki kiwango fulani kikubwa cha pesa akikipata atakitumia hovyo mpaka kibaki kile kiasi ambacho kazoea kukishika.

mfano mzuri ni wanaokopa Benki
 
Back
Top Bottom