Ukipata milioni unaila siku tatu, ikibaki elfu kumi unaishi nayo week. Hii kitaalam mnaiitaje?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,583
44,828
Mchoro umetiki umepata kazi ukalipwa million hela haichukui siku mbili ya tatu chali umebaki na hewa hamna kitu ila ka elfu ulichobakiza kanadumu hata siku nne bila shida, unakabembeleza leo 2000, kesho umetumia 3000 keshokutwa 3000 na nyumbani hutoki siku nzima.

Kwanini hatuna ile roho ya kwamba hela imeingia Tayari ni yangu kwa sasa niachane nayo hiyo millioni nianze kusuka michongo mingine ya kupata nyingine.Hata kama kazi na bata ila million nyingi ukiwekeza kula nyama Choma na vya kunoga noga walahu ufaidi hata week tatu basi ila Duuh sio poa yaani siku tatu unabakia lofa.
 
Hapo unakuta hakuna hata cha maana alichofanya zaidi ya kuhonga wanawake, kwa sababu hakuna kingine kikubwa kinachomaliza pesa ya mwanaume wa kiafrika haraka kama hicho, nilichogundua vijana wengi pesa wanapata ila wanafanyia mambo ya kijinga halafu wanalialia mishahara au faida haitoshi
 
Ingawa milioni huwezi kuila siku 3 labda kama umelipa madeni sawa. Ila kama hujalipa madeni ukala milioni moja ndani ya siku 3 unataka maombi, ni matumizi mabaya ya pesa.

N.b mbinguni hakuna hotel tule tushibe hapa duniani, kitu pekee unaenda nacho kaburini ni tumbo lako. Magari na majumba vitabaki duniani vikigombaniwa so kula as much as you can.
 
Back
Top Bottom