Ukipanga sherehe yako hakikisha una hela

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Hii tabia ya kupanga sherehe kwa kutegemea michango ya watu Ife mtakuja kununia watu bure

Mtu unapanga sendoff ya milioni kumi wakati wewe mwenyewe huna hata uwezo wa kutoa milioni mbili, unapanga ndoa ya milioni 20 wakati wewe mwenyewe hata hela ya suti unategemea uchangiwe acheni huu ujinga.

Ukipanga shughuli angalia na mfuko wako acha mambo ya kuiga iga kisa umeona rafiki zako wamefanya sherehe ya kifahari. Ishi maisha Yako na sio kuigaiga ndio maana wengi wenu hamuoi/hamuolewi.

Unakaa na binti wa watu anakuambia anataka kwenye ndoa yake apande Range Rover wakati kwao uwani wamepaki ndala mbovu zilizotoboka, Shela unataka litoke Italy, Viatu vya Uturuki, Manukato ya Dubai, Suti ya Uingereza, wakati hata passport huna, umekazana kabisa mimi bila sherehe ya bajeti ya milioni 30 siolewi nyau wewe ungekuwa na misimamo hiyo si angekukuta na bikira yako.

Acheni kuwatesa vijana kihisia mnawalazimisha wafanye vitu vilivyo nje ya uwezo wao mwisho mnajikuta mnazalishwa na kuachwa. Sio kila unachokiona kwenye vipindi vya CHEREKO CHEREKO na Ndoa Yako na wewe uviige. Chukua Bwana/Bibi Yako nenda kwa Pastor/ Shehe/ Mfungisha ndoa ukiwa na mashahidi wako na watu wachache maliza shughuli. Unaalika watu 400 umekuwa serikali wewe kwamba umeitisha bunge?

Kadi unapanga mchango laki unaijua laki ni asilimia ngapi ya mshahara wa mtu?Ukipanga jambo lako hakikisha asilimia 60 kwenda juu unaitoa kwenye mfuko wako vinginevyo utakuja kulaumu watu bure.

Nimeandika hapa kuna mtu kapanga sendoff ya milioni kumi kabakiza vikao vitano na michango mpaka sasa kapata laki nane anaishia kulaumu watu na ndugu tu
 
Wachungaji, mapadri na masheikh wakemee upuuzi huo, hizo harusi za bajeti kubwa ipo siku wachangiaji wataona maajabu, watachanga halafu bwana na bibi harusi wanaoana kimyakimya michango inageuzwa mtaji wa kufungua biashara maisha yaendelee
 
Harusi za bajiti ya chini inaonekana ni ya kinyonge na hafifu, kijana na binti wanataka harusi ya kifahari wakichagizwa na wazazi wao. Unakuta mahari tu imetolewa milioni moja au zaidi, sasa harusi itatakiwa iizidi mahari mara tatu au zaidi.

Cha ajabu kijana hana ajira wala genge la nyanya anabebwa na wazazi tu, anapata mke maisha yanaanza, muda mfupi tu hali inakuwa siyo aliyoitumainia binti, mahitaji yanatoka kwa wazazi, binti anaamua kurudi kwao, ndoa inavunjika huku imefungwa kwa gharama kubwa
 
Harusi za bejiti ya chini inaonekana ni ya kinyonge na hafifu, kijana na binti wanataka harusi ya kifahari wakichagizwa na wazazi wao. Unakuta mahari tu imetolewa milioni moja au zaidi, sasa harusi itatakiwa iizidi mahari mara tatu au zaidi, cha ajabu kijana hana ajira wala genge la nyanya anabebwa na wazazi tu, anapata mke maisha yanaanza, muda mfupi tu hali inakua siyo aliyoitumainia binti, mahitaji yanatoka kwa wazazi, binti anaamua kurudi kwao, ndoa inavunjika huku imefungwa kwa gharama kubwa
 
Hahahahaaa
Hii tabia ya kupanga sherehe kwa kutegemea michango ya watu Ife mtakuja kununia watu bure

Mtu unapanga sendoff ya milioni kumi wakati wewe mwenyewe huna hata uwezo wa kutoa milioni mbili, unapanga ndoa ya milioni 20 wakati wewe mwenyewe hata hela ya suti unategemea uchangiwe acheni huu ujinga...
 
Back
Top Bottom