Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
Nashangaa kumwona kijana mtanashati akimfukuzia binti hata hamjui......
Kisa binti kapendeza, nguo zimemkaa huku akimeremeta.......
Kijana damu humchemka na kujipiga moyo konde.......
Bila hata ya kujiuliza hivi ni yeye tu mwenye macho ya kuangaza-angaza?
Lakini ukiona vyaelea ujue fika vimeundwa.
hapa mkuu umegonga penyewe kabisa, na hii imeshatukuta vijana wengi sana, unamkuta binti unaanza kumbabakia kumbe hujui background yake na hujui kwanini umemkuta katika hali uliyomkuta nayo, na baadae ukija kugundua hali halisi tunaanza kulia lia tu, naikumbuka thread moja ilikuja last week inasema I will never trust any woman may be my Mom, mshikaji alifunguka vizuri na kweli alipenda mtoto wa chuo na alikutana nae katikati ya jiji...
akatoa simu na pesa kumbe alikua hajui kuna msemo unasema Ukiona vyaelea ujue vimeundwa
hahha.....nyie si mnadhani vyote vinavyoelea ni vyepesi
mara nyingi huwa tunajisahau.........tukifikiri ni sisi tu wenye meno kumbe wenye nayo tuko wengi na vingine vilikwishatafunwa na wengine..................kwa hiyo tunatakiwa twenda polepole...tukisoma khali ya upepo.... Manyanza
huenda kweli vimeundwa ila aliyeviunda labda hajui kuvitumia..au havitumii ipasavyo
basi, huenda ikawa ndiyo bahati yako hapo kwamba wewe ndiye uliyekuwa ukingojewa to make a full utilization of kile kilichokuwa chaelea mtoni ilhali kilitakiwa kuwa chaelea baharini!
never give up dat easily..ukiona vyaelea jua fika vimeundwa, ila je VYAELEA PANAPOSTAHILI!??
na sijui kama nini wanaume tumekua dhaifu sana mbele ya wanawake? mkuu kwenda pole pole haiwezekani bana ukiona totozi lazima uanze kujipanga ili kuing'oa
mara nyingi huwa tunajisahau.........tukifikiri ni sisi tu wenye meno kumbe wenye nayo tuko wengi na vingine vilikwishatafunwa na wengine..................kwa hiyo tunatakiwa twenda polepole...tukisoma khali ya upepo.... Manyanza
sijui bwana...
Mkuu siku hizi nani anafanya hii kazi ya kukufundisha haya mambo
Naomba unipe no ya huyo mtaalam uliyempata maana aise naona vtu vinashuka tuu bila hata mgogoro
Asante sana mkuu kwa hii useful post
Vipi kuhusu kina kaka? Unamuona kaka mtanashati.......... usafiri mzuri...... anapendeza, tunaanza kumrembulia macho na kutikisa makalio...... kumbe ana mkewe ambaye wamesota naye sana tu. Na pengine ungemuona kipindi anachapa lapa na bahasha ya kazi yenye CV na vyeti, kikwapa kwa mbali ......wala usingemuangalia mara mbili.....
My point is ni pande zote!