Ukiona unasisitiziwa jambo kuwa makini

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Habari zenu Wakuu,

Kwenye maisha ukiona kuna jambo unaambiwa na watu wengi ulifanye basi fanya uchunguzi kwanza huenda hao watu wanataka kukuingiza KING ili nawewe upate cha mtema kuni kama wao.

Siku zote jambo zuri huwa halihitaji mpambe/wapambe.

-Ukiona watu wanakwambia uoe basi chunguza kwanza hizo ndoa zao, anzia mtaani kwako kuwachunguza wanandoa halafu ndio ufanye maamuzi.

-Ukiona watu wanakwambia Lima Matikiti maji utakuwa tajiri, basi chunguza kwanza hilo zao maana huenda wanaokwambia ulime ni wauza pembejeo za matikiti (wanataka uwaungishe pembejeo).

CHUNGUZA KWANZA MKUU, USIJE KUINGIA KINGI.

OVA!
 
Back
Top Bottom