Ukiona unashangiliwa na adui, rudi nyuma ujiulize umekosea wapi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
"Ukiona unashangiliwa na adui, rudi nyuma
ujiulize umekosea wapi? na ukiona unasemwa
semwa na adui ujue umewatwanga." Rais JPM.
MY TAKE;
1. "Kikulacho ki nguoni mwako, na adui
mkubwa wa nchi hii unalala naye, unaamka
naye na unakwenda kumpokea rasmi
Dodoma". NOTE, adui mkubwa wa nchi hii ni
kile chama anachoenda kukabidhiwa.
2. Maadui wakuu wasaidizi wa nchi hii ni
Ujinga, Maradhi na Umasikini. Sijasikia
malalamiko ya mabwana hawa (Ujinga,
Maradhi na Umasikini) kwamba
wanatwangwa sana. Sijui hadi sasa Rais
anaongelea maadui wepi?
3. Na kama anamanisha maadui ni wapinzani
asisahau kua upinzani huo ni zao la katiba
hivyo kwa maana nyingine katiba na sheria
za jamhuri ndio iliyoweka adui huyo.
4. Na kama kwake upinzani (uliopo kisheria)
ni uadui basi atakua ni hatari sana kwa
kiongozi huyu kwa msatakabali wa
democrasia (uadui kwa mtazamo wake) hapa
nchini.
Just wait and watch the show my dear brother
and Mr. President.
Mtatiro J
 
MAADUI ujinga,maradhi na umasikini mtazamo wake uko tofauti sana na kuutazama upinzani.Ni vitu viwili visivyofanana kabisa.Hata mikakati ya kupambana iko tofauti.Hakuna uhusiano wala ulinganifu.
 
MAADUI ujinga,maradhi na umasikini mtazamo wake uko tofauti sana na kuutazama upinzani.Ni vitu viwili visivyofanana kabisa.Hata mikakati ya kupambana iko tofauti.Hakuna uhusiano wala ulinganifu.
Mtatiro kavurugwa. Anatafuta madaraka kwa nguvu
 
Sijawai kuona mwanaume mwanasiasa muoga kama mtatiro, mtatiro siku zote anaogopa kushindwa.. Muoga kushindwa, kipindi cha Uchaguzi alikua analia sana, ili Anatropia ajitoe... Mbona mnyika akulia..

Wenzake wanamwambia chukua form ya Uenyekiti CUF anaogopa kushindwa anasema achukui.. Alafu anamkataza Lipumba asichukue..
 
Inaonyesha hujui jimbo la segerea kati ya mtatilo na anatropia nani alistahiri kuachiwa
 
Kinachofurahisha au kusikitisha ni kuwa na viongozi wa aina ya Mtatiro ambao wanacheza ngoma inayopigwa na Rais Magufuli.

Rais Magufuli akikaa kimya, hata wao wanakaa kimya kwa sababu hawana hoja.

Kazi waliyobaki wanaifanya ni kusikiliza anachokisema Rais Magufuli halafu baadaye wanachukua megaphone kwa haraka na kuanza kupiga kelele ambazo hazina nguvu za hoja.
 
"Ukiona unashangiliwa na adui, rudi nyuma
ujiulize umekosea wapi? na ukiona unasemwa
semwa na adui ujue umewatwanga." Rais JPM.
MY TAKE;
1. "Kikulacho ki nguoni mwako, na adui
mkubwa wa nchi hii unalala naye, unaamka
naye na unakwenda kumpokea rasmi
Dodoma". NOTE, adui mkubwa wa nchi hii ni
kile chama anachoenda kukabidhiwa.

Nadhani leo hii Nyerere angekuwapo akasikia wanasiasa wa Kitanzania wanakuwa referred to kama "adui" angejilaumu sana kuupigia debe mfumo wa vyama vingi nchini.
 
Je huyu adui anaezungumzwa hapa ni nani? Hakika kuna sababu ya kutafakari maneno ya mkuu wa nchini. Yamekaa kivijembe sana na hayafai kutolewa na kiongozi wa nchi.
 
Hhhhh... Inanikumbusha awamu ile wakati ccm wanamsifia ZZK kila kukicha...
Hivi siku hizi mbona wamemtenga ZZK?
 
siasa chafu zinadumaza sana maendeleo ya sub saharan..wazungu,wamarekan na wachina wanacheza tu na siasa zetu za kinafiki kutunyonya....cjui ni lini tutatoka kwe hili giza
 
Huyu mtatiro badala apambane kukunusuru chama chake cha ndoa za jinsia moja(according to wenje) yeye anamuwaza jom tu
 
Dawa ya kufukuza mdudu UKAWA ni Dr Tulia.

Popote ukiona mdudu ukawa pulizia Dr Tulia. Wote watakimbia

HAHAHAHAHAHA ... Huyo Mwanamama ni kiboko yao...... Alewanyoosha hawana hamu kabisa. Walizoea kubembelezwa NA "Bibi" Makinda........!
 
...na ukiona unasemwa
semwa na adui ujue umewatwanga." Rais JPM

Na ukiona unawasemasema sana maadui wajue kwamba wamekutwanga...?

Muhimu: Kiongozi Mkuu mwenye dhamana ya kuliongoza taifa anatakiwa kuwa na lugha ya kuunganisha taifa na si kuwagawanya watu kutokana na tofauti zao ama kisiasa au kidini,kabila, jinsia rangi, elimu zao nk.

Taifa lina majeraha baada ya uchaguzi mkuu kupiga. Huu ulifaa kuwa muda wa kulileta taifa pamoja kwa faida wa waTanzania wote.
 
Back
Top Bottom