Kingmairo
JF-Expert Member
- Apr 7, 2012
- 4,936
- 3,548
Ukiona una hivi vijitabia au alama ujue una element za kichawi chawi, na utakuwa mtu wa shida tu milele- "Not personal and no Offence intended pls"
- Ukiona rafiki, jirani au mfanyakazi mwenzio kapata kadeal kadogo roho inakuuma- wivu wa kinyongo
- Ukiona mtu ana mafanikio hata kama humjui unasema -" hawa si ndo mafisadi, wezi, wauza unga etc"
- Ukiwa na vijisenti unaona hakuna mwingine kama wewe, in fact wewe ndo mtu wengine wote nyani tu.
- Upo radhi kufanya kila lililo ndani ya uwezo wako ili rafiki, jirani au jamaa yako akose fursa inayompa kwende msalani
- Ukisikia deal la hela unataka ni wewe tu ulikamue hata kama halikuhusu na unatengeneza zengwe ili aliyekusudiwa asilipate.
- Ukiamka asubuhi kitu cha kwanza unawaza nani umpige mzinga halafu utamdhulumu
- Una mashaka mashaka kila wakati na unamuona kila mtu anayekukaribia ni mmbaya na anataka kukudhuru
- Ukimuona mke/mume/boyfriend/girlfriend wa mshakaji wako unamvua nguo kwa fikra. Yaan hadi unalala naye kimawazo
- Kama una chale za aina yoyote mgongoni, tumboni, kifuani, kiunoni, kwenye makalio au sehemu zozote za mwili zinazofunikwa
- Una kipato (japo cha wastani) lakini watu wako wa karibu kama mke/watoto/baba/mama/ndugu etc wana shida hakuna maelezo
- Unapenda kumpongeza mtu kwa mafanikio yake, yaani kila siku wa kwanza kutoa pongezi lakini kimoyo moyo unaumia hadi moyo umepondeka.
- Unapenda sana kukopa lakini kulipa ni issue mpaka unapelekwa kwa mjumbe au polisi
- Unapenda sana stori za waganga, mitishamba na unaamini ramli ndo njia nzuri ya kumjua mmbaya wako
- Unapenda kutembelea na kujipumzisha karibu na makaruburi au miti mikubwa kama mbuyu