Ukiona Redflags hizi, usioe

No 90 izingatiwe zaidi

Mambo ya Sikupi mpaka ufanye hiki au sikupi mpaka unioe, ukiikubali utateseka huko ndoani
Mkuu, sidhani kwa namna ulivyoifafanua wewe ndiyo muktadha halisi wa mwandishi!

Ukiomba ukapewa kabla ya ndoa, ni kitu gani utachokuwa umebakiza kwake cha kukufanya usilale ukimuwaza yeye na kuharakisha kumuoa?

Hili sikuungi mkono.
 
Umepiga pale pale kwenye mshono. Miaka ya nyuma niliamua kuishi na mwanamke mmoja ambaye alikuwa karibu na hizi red flags zote ulizoziorodhesha..... hali ilikuwa mbaya. Utaomba dunia ikumeze. Yaani hizi dalili kila kijana wa kiume anatakiwa azijue na ahakikishe amezichunguza zote.
 
Vp ikiwa tayar ushazaa naye ila hujaoa ndo unagundua hizi tabia mbovu....
Hee... kwani hujui ukikutana na mnyama simba unafanya nini? Miguu ina kazi gani? Ndiyo... watoto wanaweza kuwa kikwazo ila njia nzuri sana ni kuwachukuwa wewe uishi nao. Ukimwachia watoto wanawake wa aina hiyo watakunyoosha.
 
Ndo maana watu wanashauri kuwa makini sana na mtu kuzaa naye na hii ni kote kote mwanaume au mwanamke
 
Ndo maana watu wanashauri kuwa makini sana na mtu kuzaa naye na hii ni kote kote mwanaume au mwanamke
Swala la mahusiano tena kufikia hatua ya kupata mtoto pamoja inatakiwa umakini coz unaweza kuzaa na shetani ukaishia kujuta maisha yako yote

Mi nasema ndoa sio ya kila mtu
Ukiona kabisa mahusiano yanakugalagaza Kifo cha mende ndoa ya nini sasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…