Ukiona mwanamke kanenepa, jua sababu ni hii…! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukiona mwanamke kanenepa, jua sababu ni hii…!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jul 4, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  african_woman_eating_salad_in_cafe_dbc01670.jpg

  Hivi sasa wataalamu wamegundua kwamba wanawake walio kwenye kusongeka kiakili hula sana kuliko wanaume. Katika kula huko, hujikuta wakinenepa kupindukia.

  Mwanasaikolojia Robert Jeffery anasema, mwanaume akiwa kwenye msongo hakimbilii kula kama ilivyo kwa mwanamke. Wanawake wengi wakiwa na mawazo mengi yenye kuwasonga hujitafutia nafuu kwa kula sana. Wanawake ambao wamesongeka hushindwa kujizuia kula kila wakati hasa pale wanapoingia kwenye kuwaza sana au hata wanapoona chakula kwenye televisheni au wanapoona chakula ambacho wanaweza kukipata.

  Inaelezwa kwamba matatizo ya ndoa au mahusiano ya kimapenzi huwafanya wanawake wengi kuwaza kupita kiasi na kupelekea kupata msongo wa mawazo. Ingawa kazi hususan kwa walioajiriwa inatajwa kama chanzo kizuri kinachowasababishia wanawake msongo wa mawazo lakini matatizo ya ndoa au mahusiano ya kimapenzi hutajwa sana kama chanzo kizuri kinachowasababishia msongo wa mawazo. Tatizo linakuja kwamba wanaponenepa na kujichukia kwa unene wao huongeza kiwango chao cha sononi na hivyo, hula zaidi.

  Siyo kwamba hakuna wanaume wanaokula sana kwa sababu ya kusongeka, wapo. Lakini wanawake wenye tatizo hilo ni wengi mara mbili zaidi kuliko wanaume. Kwa hiyo ukikutana na mwanamke ambaye ni mnene kutokana na kula unapaswa kujua kwamba, huyo amesongeka kiakili. Kwa wale wanawake wanene, ambao wanakula sana na wanashindwa kabisa kujizuia kula sana, inabidi wajue kwamba, labda wamesongeka. Ili kujitoa kwenye mashaka hayo, inabidi wapate tiba ya kusongeka ambayo ni pamoja na ushauri na dawa.

  Sikuandiki utafiti huu ili kuwakera wanawake wanene, hapana. Lengo ni kuwasaidia kujua kinachowakabili ili waweze kujisaidia. Unene wa ziada ni hatari kwa maisha ya mhusika, bila kujali kama unene huo unakupendeza au unasifiwa kwamba, una fedha, jua tu kwamba, ni hatari tena hatari sana.
   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Sikubaliani na wewe katika hili, hata kidogo!
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mkuu Invisible kwanza heshima yako............
  Nakubali kutokubaliana lakini ukweli ndio huo, kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalamu wa saikolojia....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  nilifikiri msongo wa mawazo unachangia mtu kupoteza appetite na possibly ku-lose weight...vipi mchango wa hormonal imbalance unaosababishwa na contraceptives, hii nadhani inachangia zaidi kwenye kunenepa bila mpango...
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  kuna ka ukweli
   
 6. roby2006

  roby2006 JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 399
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kwa utafiti wangu binafsi kuna kaukweli ndani yake
   
 7. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #7
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [FONT=&amp]Depression Leads to Overeating for Women, But Not Men

  [/FONT]
  That is according to University of Minnesota psychologist Robert Jeffery. His year-long study of 1,800 obese men and women looked at gender differences in the eating behavior of overweight adults. "Moods don't seem to be driving men's eating, but depression is a key driver for women," said Jeffrey, speaking at the American Psychosomatic Society meeting in Barcelona.

  At the start, everyone rated how difficult they found it to resist food in varied situations -- at parties, when watching TV, etc. -- or while experiencing certain emotions. Participants also took a depression test and were asked about their medical histories. Women were nearly twice as likely as men to have a history of depression. "Body weight is not a big issue for men," Jeffery says, "but a lot of these women might be depressed because they're overweight, and the social consequences of this for women are much greater."

  Women's depression around weight apparently prompts even more weight gain. For women, depression was strongly tied to trouble controlling eating behavior. Depression correlated with the women's inability to resist foods even more than their body weight did. For men, the heavier they were, the less confident they felt about controlling their weight; depression had no bearing on that confidence.

  But could men just be denying that food is a crutch for them? Jeffery thinks not, because the relatively lighter men voiced more confidence about resisting food, and the heavier men said they had more trouble. A year later, after receiving counselling in a weight-loss program, women who weren't depressed lost more than twice as many pounds as the depressed women who said they had trouble resisting food. For men, neither mental health nor confidence about controlling eating predicted weight loss.

  Men usually have to be much more overweight than women before they'll enter weight-loss programs, Jeffery says. Women dominate group programs, "and programs with a lot of women ought to be addressing depression." Men, he says, "tend to be a lot more naive than women" about what puts on the pounds. "Eating is kind of a knee-jerk thing for them." An informational approach might work best for men, he says.


  Health News Special Edition on Depression
   
 8. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Sio kweli Mtambuzi , labda useme baadhi ya wanawake........uwe na msongo afu upate hamu ya kula mpaka unenepe?.....kama wako wa aina hiyo basi jua watu tunatofautiana sana.....nijuavyo mimi ugomvi haswa unaohusu mahusiano hufanya mtu kupoteza hamu ya kula kabisa.......misongo hukondesha bana!.....ila sijui labda wapo unaowasema wewe ila sio wanawake wote!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,047
  Likes Received: 24,047
  Trophy Points: 280
  Kumbe.....kwa kauli hii leo nimethibitisha kumbe Invisible ni mwanamke! Mtambuzi, sweetlady, Kongosho cacico, gfsonwin, Kaizer na wote wenye mapenzi mema. Nikilambwa ban kwa kauli hii, msisite kuandamana mpaka kieleweke. Pipooooz....!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #10
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,250
  Trophy Points: 280
  Mie nakubaliana na wewe. Na kuna wanawake na wanaume ambao ni emotional eaters. These usually use food to drown their sorrows. Ofcoz wanaume wengi watatumia pombe.

  I for one, nikiwa stressed a nice yummy meal will make me feel better. I dress up well, feel good and eat out. Kama hujajijua ama u are in denial about this like most people, utashindwa kula healthy. So najua nikiwa stressed I hit the gym really hard, then eat later while being careful.

  Let's be frank ladies, ukiwa na a hard stressful day kazini ama nyumbani, kitimoto ama pizza won't soothe u and give u energy to kick the day?
   
 11. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  King'asti, bora wee umekubali.

  Kuna ka ukweli sana hapa, na unahakikisha hukosi icecream and the like home.

  Tena siku kama hizo hata kupika hutaki apike dada unapika mwenyewe.

  Tena mtu akipitia depression ya muda mrefu anaweza hata kujikuta amepata eating disorder.

  Japo eating disoder kuna wengine wanakula sana, wengine wanashindwa kula au wanakula kidogo sana.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #12
  Jul 4, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Aisee mke mwenza mie niko tofauti , nikiwa na stress ya ukweli siwezagi kula chochote !
  Afu umempeleka wapi wifi kipenzi?.....umeona mpaka gfsonwin kamuopoa Kaizer mbele ya macho yetu?....akija wifi tutamjibu nini?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hapo red nimetabasamu manake nikicheka ntalambwa ban..... we we we na athubutu huyo asiyejipenda kumlamba ban.... babu kipenzi cha wajukuu wote wa kike jf aka ODM aka Asprin ...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,333
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  mtambuzi acha kutoa povu, weka source ya huo utafiti tujue then tukusifie kwa kujisomea. leta source kaka vinginevyo sema kazi yako imepitia kwa academician/wataalamu gani
   
 15. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Hiyo ina ukweli asilimia 150 hasa kwa watu ambao chakula kwao si tatizo.
  Nina hakika huo utafiti ni wa kimagharibi ambako umasikini unaendana na vyakula vya hovyo kama machips na frozen food, na cookies.

  Kwa hapa Tz watu wananenepa kwa kuwa bado kuna baadhi ya watu hawajagundua kuwa unene ni ugonjwa regardless mtu anaonekana ana mvuto au hapana. Kwa hiyo inaweza isiwe sababu ya stress ila sababu ya ignorance na bado kuendelea kuamini kuwa na uwezo wa kupata chakula ni utajiri hivyo mkeo akinenepa basi unauwezo wa kulisha. Lol.

  Lakini kwa sasa wengi wamekuwa wahelewa na wanapima uzito na urefu wao kujihepusha na magonjwa ya kisukari na moyo.

  Juzi kati nilikuwa na shangazi wa rafiki yangu ambaye ni std seven nilishangaa ananambia siku hizi unene siyo dili na ametokea kijijini. Anajua akinenepa sana ana chance ya kupata magonjwa na hali vyakula vyenye mafuta.

  Kuna watu sababu ya umasiki wakipata chakula wanakula in advance na cha akiba, cha jana leo na kesho kwa sababu hana hakika kama kesho atakula.
   
 16. petrinamwana

  petrinamwana JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 877
  Likes Received: 258
  Trophy Points: 80
  Mhhh ya kweli haya??
   
 17. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #17
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mkuu HAZOLE haya kwa mara nyingine source hii hapa mkuu.....................
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #18
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Nafikiri utafiti ni wa kimagharibi zaidi, nenda vijijini kama utawaona hao wanawake wanene, labda vibibi. Ina maana huko hakuna stress?

  Mimi nikiwa depressed hata hamu ya kula sina!
   
 19. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #19
  Jul 4, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,973
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mkuu, hii nayo kali. Pipoooooz............ na maandamano mpaka kwenye unene wa wanawake?!
   
 20. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #20
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kaunga nawewe umezidi sasa, ilimradi ubishe tu...............LOL
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...