Ukiona mwanamke kanenepa, jua sababu ni hii…!

Hapa mnanikumbusha kale kausemi kwamba 'kwa kila uongo unaoongelewa, ukweli haukosekni ndani yake' au kinyume chake.
 
Ahaaaaaaaaaaaaa! Kumbe ndo maana ktk ndoa zenye matatizo utakuta mke ananenepeana halafu mume kimbaumbau!
 
Mmmh utafiti wako huu Mtambuzi nasita kuuamini hasa nikikumbuka dada yangu alivyonyooka ghafla kwa sababu ya msongo wa mawazo ya ndoa yake!
 
hua wanakula bt not the right food. mfano kuna some girls hua wakiwa na stress wanakula ice cream or chocolate na hizo ndio zinanenepesha or atakua ana crave kitu ambacho sio kizuri kwa afya yake. Huwezi kua na stress ukawa na hamu ya kula wali maharage..
 
Mimi ni mmoja wapo ninae kula sana nikiwa na msongo wa mawazo kama mtambuzi alivyoelekeza. Hajakosea kabisaa ni kweli tupu hiyo.
florence mie sijakataa alichokisema Mtambuzi ila tu nimesema sio wanawake wote wanaoweza kula wakiwa kwenye msongo wa mawazo mie mmoja wapo....siwezagi kula!
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi kakangu, kwa mara ya kwanza napingana na wewe hususani katika hili, haiwezekani uwe na msongo wa mawzo halafu uapte hamu ya kula, haipo! tena stress za mapenzi? Wanawake wengi wanokuwa na stress especially za mapenzi wanakongongoroka sana, hana muda wa kula, muda wote ni kuwaza na kulia atakula saa ngapi, kwanza hata chakula huwa hakina ladha tena
 
Nafikiri utafiti ni wa kimagharibi zaidi, nenda vijijini kama utawaona hao wanawake wanene, labda vibibi. Ina maana huko hakuna stress?

Mimi nikiwa depressed hata hamu ya kula sina!

Vijijini hawana stress hata kidogo, stress inatokana na uparanganaji wa kimaisha. Unamkuta mama ana zaidi ya watoto sita, mme wake akitoka asubuhi anaingia ziwani anakuja na samaki, wanauza baadhi wanaobaki wanakula aisha yanaenda. Nyumba wanayoishi hawawazii kuikarabati, kununua nguo ni mpaka mwisho wa mwaka, tiba ni miti shamba, na zaidi wanaamini kwenye mambo ya kiasili. PUSHNEY
 
Back
Top Bottom