Ukiona mtu wa hivi JF ujue anatafuta kiki

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,668
1. Post haihusu mapenzi wala mahusiano anaipeleka jukwaa la MMU. Basi tu ili mradi watu waisome na wamuone.

2. Anapenda kuzua ubishi kwenye thread za watu kwa jambo lisilo na ubishi ili mradi aonekane na yeye basi yupo na watu wamjue.

3. They always go against the trend. Unakuta thread inahusu maloveee anatokea mwehu ana comment "JK FISADI" ili mradi watu wa pay attention.

4. Wanapenda kujidai wanawafaham na wanamazoea na wale members ambao ni ma pro. Utaona tu kaandika comment halafu anajidai kum tag Nyani Ngabu, The Boss, lara 1, Bitoz, Valentina, miss chagga, faiza Fox..... Ndugu yangu wewe Id yako yenyewe ya juzi halafu unajidai eti unawafaham ma pro wa JF... unatafuta kiki.

5 Kila thread lazima acomment hata kama hana cha maana cha kuandika na haimuhusu.

6 Kama ni mwanaume basi atataka aonekane yeye Handsome boy matawi ya juu na kama ni ke basi atatafuta namna tu kwenye comment zake ajioneshe yeye wa moto na ni girl wa ukweeee, kumbe hamna kitu.

Embu ongezeeni nyingine tuwanange watafuta kiki wote wa JF....
 
Back
Top Bottom