Ukiona dalili hii ujue kuna jambo

cj21125

JF-Expert Member
May 12, 2013
3,016
2,445
Habari wandugu.
Kuna ishara nyingi ambazo mtu yeyote awe ndugu, unayemdai au mchumba/mke/mume akikuonyesha ujue mahusiano ndio yameisha. Hauhitaji hata kuuliza kwa nini.
Mfano ukiwa unampigia simu hapokei, ukimtumia meseji hajibu au kabadilisha namba ya simu ujue huna chako tena.

Binafsi kuna jamaa nilikuwa namdai akawa hapokei simu wala kujibu meseji zangu baada ya kutafakari nikajua nishazulumiwa.

Ongeza dalili nyingine kama zipo...
 
Ukiwa na miadi na Manzi leo badala ya kuja akakupigia simu na kukuambia amepata shida kidogo anaomba kwanza umtumie pesa fulani akasolve hiyo shida ila kesho ndo atakuja kwako....Tingisha kichwa sana wewe kabla ya kufanya uamuzi wowote..
 
Ukiona anampa mtu simu yake apokee akwambie mwenye simu katoka jua imekula kwako....

Huyu bint 0676243350 yupo moro alinambia amenipatia dada wa kazi nimtumie nauli amsafirishe Kilimanjaro. Alitafuna pesa yote na nkipiga simu hapokei au anampa mtu apokee.
 
Ukiona anampa mtu simu yake apokee akwambie mwenye simu katoka jua imekula kwako....

Huyu bint 0676243350 yupo moro alinambia amenipatia dada wa kazi nimtumie nauli amsafirishe Kilimanjaro. Alitafuna pesa yote na nkipiga simu hapokei au anampa mtu apokee.
Mkuu, usifadhaike nafsini mwako, Mkwere alishasema, 'ukitaka kula, lazima uliwe kwanza'... Pole mwaya.
 
Ukiwa unamuona mtu online meseji zako hajibu anasoma na kuzikaushia, jua hapo umekuwa gumzo la kijiwe chase, anasoma na kushare na wenzake
Ukiwa na ahadi na msichana siku ya tukio akakwambia kaona siku zake hivyo hawezi kuja, jua imekula kwako kuna men mwenigine amechukua nafasi
 
ukimpigia anajifanya hakusikii eti haloo halooo mtandao unasumbua anakata ukija mtafuta hapatikani inakera
 
Ukiona we ndio unaye mtafuta hewani daily but ye hana habari mpaka akuone sehemu au anashida jua lashilaga...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom