Ukioa mwanamke unaempenda sana ni hatari? Wewe unasemaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukioa mwanamke unaempenda sana ni hatari? Wewe unasemaje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by emmanuel katamba, Jun 12, 2012.

 1. emmanuel katamba

  emmanuel katamba Member

  #1
  Jun 12, 2012
  Joined: Jun 8, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika hali ya kawaida mtu huweza kushangaa hoja hii. Ukweli ni kuwa watu wengi wanafikiri wakioa au kuolewa na watu wanaowapenda sana maisha huwa ya furaha sana lakini wengi wamekuwa wakilazimika kufanya mambo hata nafsi zao hazipendi kwa kuwa tu wanaogopa wampendae atachukia au atamwacha. Ni vyema basi mtu kuoa au kuolewa na mtu umpendae wastani ili kuwa na kuambiana tunavyopenda na tusivyopenda vinginevyo tutaogopa kuwaudhi watu tunaowapenda kupita kiasi.
  WEWE UNAONAJE? NI VYEMA AU SI VYEMA KUOA AU KUOLEWA NA MTU UMPENDAE KUPIATA KIASI?
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Jun 12, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  ndoa sio kitu cha mchezo wala majaribio..... Unapaswa kuoa/olewa na mtu unayempenda......

  Unadhani kuishi na mtu ambaye huna mapenzi nae kivile ni mchezo?
   
 3. k

  kabye JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2012
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 355
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  balance
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  mmmh, ngoja waje wajuzi
   
 5. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  jamani naipenda hii forum! natangaza rasmi leo kha! uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii umuoe ambaye unampenda wastani! hii kubwa kuliko!
   
 6. wahida

  wahida JF-Expert Member

  #6
  Jun 12, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bora kuoa au kuolewa na unaempenda , kwani ukiolewa na usie mpenda utafanya visa na hapo haitokuwa sawa utamuonea tu mtu kwani yy atakuwa ktk hard situation ,na ww ulieoa au kuolewa hutoishi nae na kwa raha .
   
 7. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #7
  Jun 12, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  fallacious
   
 8. blea

  blea JF-Expert Member

  #8
  Jun 12, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Chochote kinachozidi kiasi ni hatari hivyo basi ni hatari pia kumwoa au kuolewa na mtu unaempenda kupita kiasi kwa hayo sio mapenzi tena kwani yameshazidi kiasi hayo yatakuwa na jina lake lingine
   
 9. K

  KASIANI Member

  #9
  Jun 12, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mtizamo wangu ni kwamba oa au olewa na m2 anayekupenda kwa sababu ni rahis kujlazmisha kumpenda m2 usiyemfeel kuliko kumbadilisha acyekupenda akupende.
   
 10. DERICK2000

  DERICK2000 JF-Expert Member

  #10
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 204
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kujilazimisha..Not willingly.hiyo hapo ni tatizo p4a,u wil always think of da one u love.
   
 11. DERICK2000

  DERICK2000 JF-Expert Member

  #11
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 204
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakuna kupenda kiasi,oa unaempenda na anakupenda pia.
   
 12. CUTE

  CUTE JF-Expert Member

  #12
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 1,237
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  bora kuolewa na umpendaye kwa dhati kuliko usiye mpenda jamani mana ni ngumu sana kuishi ndani na mtu usiyempenda
   
 13. m

  mkizungo JF-Expert Member

  #13
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 247
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wanawake huwa hawapindi,,,wanashawishika na kutii tu,,,,hivyo ukimpenda mwanamke saaana,,akishawishiwa na mwingine akamtii utakufa ka bp,,,,,ndo mana wengine wanaoa kwa mikataba,,,,hakuna kupendana,,ni mume anapenda,,,,,wanawake aweza tii sana kwa maslahi tarajali au vile ameridhika,,nje ya hapo utaisoma number za kirumi,,,,,,
   
 14. Ronn M

  Ronn M JF-Expert Member

  #14
  Jun 12, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 1,283
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sasa hapo inabidi tujue upendo wa wastani ukoje! Halafu mkikosana unawmwacha haraka! You have Ann, u lover her so much! You have Jane, 'unampenda wastani'(ingawa siielewi dhani hii). Then u go for Jane! Something must be wrong upstairs
   
 15. Jotojiwe

  Jotojiwe JF-Expert Member

  #15
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 325
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Ndugu hakuna hatari kama hiyo kuoana na mtu unayempenda kupindukia, tena inakuaga hv ww unampenda kuliko kifani alafu yeye anajifunza akupende vp kila siku ijayo katika mapenz yako na mfunzo yake.. Nakwambia utakufa umwache akidunda na wengine apendavyo. Nikama maji kukaa ndan ya ndoo na ndoo kuelea juu ya maji, ndoo haikai ktk maji.
   
 16. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #16
  Jun 12, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Bora kuoa mtu usiyempenda sana maana ukimpenda sana ata kusumbua sana.

  Ndio pale unapomkuta na mwanaume chumbani kwako na kumsamehe. Na anapo gundua anapendwa sana ana kutesa sana.
   
 17. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #17
  Jun 12, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  ni vyema
   
 18. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #18
  Jun 12, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,124
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  BadiliTabia...Sikubaliani nawe moja kwa moja kwa haya uyasemayo. Wasichana/wanawake wengi hapa Bongo siku hizi hawaolewi na mtu eti kwa sababu wanampenda; hapana, ila wanafuata material things. Haswa ukiangalia idadi kubwa ya wanawake wanao olewa na hawa vijana wa kuuza unga, unataka kuniambia they are there for the love? Heck no, but they'll do anything na watakubali kunyanyasika ili waonyeshe kuwa wako serious na ndoa zao. Mwanamke gani mwenye akili timamu anakubali kuwa a spare tyre? Nasema hivi kwa sababu vijana wengi wenye mahela machafu hapa Bongo, yaani asilimia 100 ni malaya na wake zao wanajua hivyo lakini wanavumilia because they are there for the ride. Kutoka kwenye ndoa zao hawawezi kwani walishatambia wenzao kabla ya kuolewa, na akitoka hapo ataenda wapi kwenye matanuzi kama aliyonayo? Binafsi, najua jamaa kama watatu hivi wameoa na wapigaji mademu hodari sana hapa jijini. Cha kusikitisha wake zao wote wanajua na mara nyingi huwa wanawambia waume zao mwenzangu tafadhali jichunge huko nje na kina mama, au utasikia shemeji tafadhali muonyeni rafiki yenu jamani kwani najuwa vitu vyake huko nje. Karne hii ya 21 hakuna love Bongo, kama wewe una mapenzi Mungu akubariki ila pia nakusitikia kwani kina mama wengi kama wewe ndio wanaopelekeshwa kwenye ndoa zao na huishia kujiua kwa kutovumilia manyanyaso ya ndoa. Pole sana yasije kukukuta dada yangu ila ukweli ndo huo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #19
  Jun 12, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,124
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280


  Si kweli, hujawahi kuona ndoo imezama kisimani au mtoni ikijaa maji? Ila umetoa point nzuri sana isipokuwa mfano tu ndiyo una utata.
   
 20. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #20
  Jun 12, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kupenda nusu nusu ni kupi huko? Unakusudia kuwa uwe hujali kwa analofanya mwenzio? usimshauri mwenzio anapokosa, au uwe na uhuru wa kumwambia chochote eti hujali nini itakuwa reaction yake?
  Na kupenda sana unakusudia ni kupi? yaani huwezi kumwambia chochote eti usimkere?
  Ndowa ni kitu kinachotarajiwa kuwa hatuwa ya mwanzo katika kujenga familia endelevu. Ndowa ndio jambo halali pekee kwa wawili kupata watoto na ndani ya ndowa watoto hawa wanataka walelewe hadi kufikia umri wa wao kujitegemea, sasa iwapo hamko tayari kusawazishana na kuunda msimamo wa pamoja ambao watoto wenu wataujuwa kuwa ndio msingi wa famila yenu, hapo hakutakuwa na ndowa wala familia mtakayoijenga haitokuwa na msimamo.
   
Loading...