Ukimya wa viongozi, kulikoni?

Ukimya wa viongozi, kulikoni?

Mkandara

Platinum Member
Joined
Mar 3, 2006
Posts
15,980
Reaction score
9,414
Nimejitahidi sana kutaka kuelewa sababu gani viongozi wote wa juu wamekaa kimya juu ya haya ya KIBAGUZI yanayoendelea nchini.

Na kibaya zaidi ukisikiliza maneno yanayozungumzwa utagundua sii hoja ya NCHI wala MUUNGANO isipokuwa watu wake. (Wazanzibar vs Watanganyika)

Aidha utasikia wakitaja wazi wazi Watanganyika hivi na vile ama viashria vinavyoshabihiana na Watanganyika! Na sasa Watanganyika nao wanafunguka kuwazungumzia Wazanzibar wazi wazi! Halafu viongozi wameufyata kimyaaa, sijasikia kiongozi hata mmoja akikemea haya yanayoendelea!

Niseme tu kwamba hata katika Ndoa watu hutarakiana sii kwa sababu na Nikah (ndoa yenyewe) bali wanandoa wenyewe hawana mapenzi tena. Hivi kweli tumefikia hatua hii? na kama tutauvunja Muungano wetu katika hali hii mnadhani kuna AMANI tena?

Maasalaam.
 
Ibara ya 20(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Ibara hiyo inasema:

"Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani..."

Hii ndiyo ibara inayotambuliwa kama msingi wa kikatiba wa uhuru wa kukusanyika na kuandamana kwa amani nchini Tanzania.
 
Msukuma na Waitara wameonesha kuchukizwa na matamshi ya wabunge wanzanzibar kiasi cha kumtaka rais wa Zanzibar awachukulie hatua za kinidhamu hao wabunge. Wabunge wa bara wameanza kuchachamaa dhidi ya ubaguzi wa Wazanzibar
 
Samahani mbona mnatumia Katiba pasipo husika? Ibara hiyo inaruhusu UBAGUZI?
 
Msukuma na Waitara wameonesha kuchukizwa na matamshi ya wabunge wanzanzibar kiasi cha kumtaka rais wa Zanzibar awachukulie hatua za kinidhamu hao wabunge. Wabunge wa bara wameanza kuchachamaa dhidi ya ubaguzi wa Wazanzibar
Hawa ni Wabunge wa JMT lakini ajabu Viongozi wote wa juu wa SEREKALI ya Zanzibar na JMT wamekaa kimyaa kama kwamba hawasikii ama wanaunga mkono kinachoendelea.
 
Back
Top Bottom