PreGE2025 Ukimya wa Mbowe; Je, yupo nyuma ya G55? Kwanini haungi mkono harakati za Lissu na Chadema hivi sasa?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Wakuu

Je, Mbowe yupo nyuma ya yanayoendelea kati ya wagombea na watiania wa ubunge 55 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa 2020 na 2025 maarufu G55 wanaowakilisha zaidi ya watiania 200, wakiwemo viongozi wa juu wa chama hicho dhidi ya uongozi wa sasa chini ya mwenyekiti wao Tundu Lissu ambaye anaongoza harakati za kuzia uchaguzi kama hakutafanyika mabadiliko (no reforms, no election).

Soma, Pia: Waraka wa wagombea 2020 na watia nia wa ubunge 55 wa CHADEMA

Tangu kukubali kushindwa uchaguzi wa ndani wa chama hicho na kusema anaenda kusaka Mafekeche, Mbowe aliamua kukaa kimya na kutoshiriki wazi wazi shughuli za chama hali ambayo inazua maswali mengi kwani wengi wanaoonyesha kwenda tofauti na harakati za chama chini ya Lissu ni wale waliokuwa timu Mbowe.

Mbowe ni mjumbe wakudumu wa Kamati Kuu ya chama lakini hayaonekani kwenye vikao kazi vya chama wala kuzunguka mikoani kueneza ajenda ya kutaka mabadiliko kwenye mfumo wa uchaguzi.

Kama Mbowe angekuwa bega kwa bega na Lissu, haya yanayoendelea hivi sasa ya Lembrus Mchome, John Mrema na wengine Je, tungeyashuhudia?
 
Mbowe hawezi kuwa fala kama Lisu,yaani ammdaririshe wakati wa Kampeni harafu amuunge mkono? 😁😁

Mlisahau kukwambia hiyo Lisu kwamba Kuna maisha baada ya Uchaguzi harafu mkono matupu na maneno hayalambwi ila hela .

Mtajua hamjui 😆😆👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DIBcjows1om/?igsh=MXZkZjVrOHQ1aHMyZQ==
 
Lissu ni dikteta hapaswi kusaidiwa
 
Tunayaandika haya kwa nia jema. Bado kuna njia ya kunusuru chadema.
1. Kila askari ni muhimu chadema. Kupishana kimawazo, matokeo ya uchaguzi should be handled with LOVE and not enemity!
2. Lisu kazi yako kubwa iwe kuponya majeraha.
3. Short of that unajidanganya!
 
Nyie huwa mna msifu lema kua ni kiongozi ana wadhihirishia sasa kukosa kwake hekima!
 
Na yule dada wa Nairobi na anawakoroga balaa!! Tuliona mbali sana uwezo wa kuongoza taasisi kubwa kama CHADEMA lissu hana na hakua tayari. Muda ni hakimu wa yote.
 
In fact Mbowe kesharudisha yote alopoteza wakati wa JPM kupitia Fedha za Abdul.

Heche hamna namna ambayo ataweza mrejesha mdogo wake.

LISSU Hana namna ya kurejesha mwili wake kabla ya ulemavu ulotokana na Risasi 16.

Hivo LISSU NA HECHE WASOMGE MBELE, WANANCHI TUNAWAELEWA.

G-55 wangekua wakushinda, wangemshinda LISSU wakati wa Uchaguzi.


Kwa Sasa wanajua wameshindwa, wanajaribu tu kuleta vijivurugu ili waonekane.

G 55 wamekataliwa na Mkutano Mkuu, wakakataliwa na Wanachama, na wamekataliwa na Wananchi.
 
Baada ya uchaguzi mkuu wa 2015 niliapa kujiweka mbali na siasa kwa namna yoyote ile,,,, ! Watu wapo kujishibisha matumbo tu na kimaslai zaidi !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…