Mariangonyani
Member
- Mar 31, 2013
- 39
- 59
Pole sana....ila nachelewa kuamini kama ni kweli ama ni utapeli mpya wa mitandaoni,....samahani wakuu msinipige mawe ni katika hali ya kuwaza na kuwazua kwa kina.Nawashukuru sana jamani mmenitia moyo hadi machozi yamenitoka. Mungu ananipigania ila naanza kukata tamaa, niliupata 2008 na sijaanza kutumia dawa; bado Mungu ananiongoza.
Tatizo maisha yamekuwa magumu sana kwa sasa kiasi hadi nashindwa kula, yote ni woga wa kuwashirikisha marafiki na familia ila naamin Mungu atajibu maombi yangu
Siwezi kuwa tapeli maana sijaomba hela ya mtu.Pole sana....ila nachelewa kuamini kama ni kweli ama ni utapeli mpya wa mitandaoni,....samahani wakuu msinipige mawe ni katika hali ya kuwaza na kuwazua kwa kina.
My bad_i draw it back,...pole sana dada.Siwezi kuwa tapeli maana sijaomba hela ya mtu.
unapitisha kapu la mpesa au?Kibarua hauna? AshaDii pls, kama unaweza fanya kama ya yule kijana ili tumsaidie mtaji ili aweze kujikwamua
Nina amini mashosti na mabro kama FP snowhite, Smile, Mentor, KIKUNGU, gfsonwin, Riwa, mwaJ, cacico, MwanajamiiOne, King'asti na wengine wengi wanaweza kusaidia mdada akaweza simama kwa miguu yake.
Amein ameinNimekugongea LIKE sio kwamba nimependa ulivyopata UKIMWI, ila ujasiri wako huo, Basi MUNGU wetu aonaye sirini na haja za mioyo yetu akakujibu siku ya shida yako, mtumaini yeye tu, usimwangalie mwanadamu awaye yeyote, kama yeye aliruhusu uwe hai hadi leo hii basi ataruhusu na MEMA yaje kwako.
Kuna wimbo wa Bukuku-Bahati naupenda sana una maneno yanasema hivi; wewe ni MUNIGU tena ni MUNGU, hivi leo nimejua wewe ni MUNGU, kama ulivyoruhusu mabaya yaje kwangu, ndivyo uruhusu na mema yanipate, kama ulivyoruhusu MAGONJWA yaje kwangu ndivyo uruhusu UZIMA uje kwangu........Ni wimbo ambao una ujumbe mzito sana sana, MUNGU wangu wa Mbinguni ninayemtumaini na kumtegemea akakujibu haja ya MOYO wako leo, akasikie kilio chako, akasikie ombi lako leo, umuitapo akujibu upesi tena Martha Mwaipaja nae anasema hivi, Jaribu kwa mtu si kwamba ni mtenda dhambi ila ni kikombe tu ambacho ni lazima apitie, usimwone mtu anapita kwenye jaribu........Muombe MUNGU aondoe kikombe hicho, hujatenda dhambi ndugu.
Abihudi Misholi kwenye latest CD aliyotoa ana wimbo pia unasema kuwa, hakuna kikombe kinachoponyesha UKIMWI, kikubwa ni TOBA na hii ndio itakuweka huru. Basi nakuombea toba ya kweli, uzidi kuwa huru katika Kristo YESU, sote tuseme AMen
Kaunga nashukuru kwa kunishtua...
Kwa mtazamo wangu hapa tatizo ni kubwa zaidi ya pesa Dear.
Ikiwa tu frustrations zingine za Kimaisha ambazo zinaweza kuwa solved in the long run huhitaji sana watu wa karibu kukufariji na kukupa moyo - Upande wa kujitambua kuwa ni mwathirika bila kuwa na mtu wa ku share, kuongea, kujadili na kufarijiana ndio worse.
Naamini kuwa hata ikitokea akapewa msaada wa pesa, haitakuwa msaada sana kama vile yeye kupata support ya familia na watu wake wa karibu kwa kutambua hali yake Ki afya na kumkubali jinsi alivyo. Imagine kakiri kapata virusi hivyo toka 2008 na bado afya yake ni nzuri na hajaanza kupata vidonge. Hiyo ni sababu tosha kabisa ya kuendelea kuwa na matumaini na pia kigezo kikubwa kutumia kuwashirikisha ndugu na jamaa. Si wote but kwa kuanzia na wale ambao ni watu wazima na wanaweza play positive part katika hili.
Hata hivyo ikitokea ikaonekana ni muhimu kwa sie kuhamasisha nitahusika kwa asilimia 100.