James Martin
JF-Expert Member
- Apr 2, 2016
- 1,206
- 1,509
Tundu Lissu ni mtu mmoja anayejua kujenga hoja sana. Amethibitisha kwamba yeye si mahiri ndani ya nchi tu, bali pia kwenye majukwaa ya kimataifa ambayo yanatisha kwa mtu asiye na uzoefu.
Tofauti na "waandishi" wa habari wa Tanzania ambao hawajui hata kuuliza maswali magumu, waandishi wa habari wa nchi za magharibi ni wazuri hasa. Ukiwaangalia waandishi mahiri kama Stephen Sackur, Andrew Marr au Chris Cuomo mpaka unaona raha! Nafikiri wanasiasa wengi wa Tanzania wakihojiwa na hao niliowataja wanaweza kuzimia kwenye mahojiano! Hata hao wanaojifanya madokta na maprofesa.
Nafikiri umahiri wa Lissu ndiyo sababu kubwa inayowafanya wapinzani wake wa kisiasa kumwogopa kwenye midahalo!!
Video: Chris Cuomo akimuhoji mgombea wa Senate Kris Kobach