Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,194
- 4,116
Kufanya maamuzi mabaya wakati wa uchaguzi kunawagharimu watu wengi sana, wengi hukubali kurubuniwa kwa rushwa au ahadi za madaraka, upendeleo au kumchagua mtu kisa ni wa chama chake hata kama hafai. Huuza haki yao ya msingi ya kufanya maamuzi yao binafsi na sahihi kwenye boksi la kura.
Wakati unapokuwa umeshindwa kufika kwenye shughuli zako kwa wakati kutokana na ubovu wa barabara, unateseka na kukosekana kwa huduma muhimu za kijamii au kupanda kwa gharama za maisha ile rushwa uliopewa ushakula imeisha au kile kitenge na tisheti vishachakaa na havifai tena ila una miaka 5 ya tabu kwa kumchagua kiongozi asiyefaa.
Wahenga walisema ningejua huja mwisho wa safari na majuto ni mjukuu, unaposema ningejua ushachelewa inabidi ujipange upyaaaa! Usikubali kuishi kwa majuto miaka 5 fanya maamuzi sahihi kumpata kiongozi bora.