Ukikutana na mtu kwa mara ya kwanza

Benny

JF-Expert Member
Jun 6, 2014
3,275
5,403
Habareee!

Nadhani mpo poa wakuu naomba kuona michango ya watu kidogo juu ya hili la socialization.

Hivi ukikutana na mtu kwa mara ya kwanza ni kipi unapenda agundue kutoka kwako labda ni mpenzi, rafiki au ukweni kwa mara ya kwanza au ndugu yako tu mliyepotezana kitamboo kikubwa unachopenda ajue kutoka kwako ni nini?

Binafsi mara ya kwanza sipendi kuonekana "kilaza" au mtu flan "mporipori" pia sipendi kuonekana "smart" sana.

Karibuni
 
Mkuu hao watu uliowataja sidhani kama ndo utakuwa unakutana nao for the first time..Mtu mpaka awe mpenzi,rafiki au ndugu it means u've met them before and u know your connection japo kidogo
Labda cha msingi ni
Kujiamini,stay positive,Acha maigizo unless kama utaweza kuyamaintain,Tabasamu nalo ni muhimu coz linampa mtu confidence/uhuru wa kuongea na ww
 
Ninapenda nionekane jinsi nilivyomtundu kwenye vifaa vya umeme kwa kutumia na kuvikarabati.
 
Ukikutana na mtu mara ya kwanza usinywe naye kinywaji!

Pia inategemea na mnakutana kwa sababu gani, nini malengo ya huo mkutano, nini unataka kiwe baada ya huo mkutano.

Mfano ukikutana na mtu kwa mara ya kwanza na ni interview ya kazi ni lazima ufunguke aujue uwezo wako katika fani husika.

Kukutana na mtu unayetaka awe mchepuko ni tofauti na mtu unayetaka awe njia kuu.

n.k
 
Back
Top Bottom