Ukikasirika huchukua uamuzi gani?

Ukikasirika huchukua uamuzi gani?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Kupigana, kuoporomosha maneno makali, kunyamaza, kununa, au kuondoka eneo la tukio? mimi huondoka sehemu ya tukio.
 
Inategemea!!!!!

Mtu kaja eneo lako la biashara analeta zogo!!!!!?????
 
Inategemeana na tukio wakati mwingne naondoka,wakati mwngine nakaa kimya,wakat mwingne nanuna,wakati mwingne nafoka,wakati mwngne nabaki kucheka tu,kupigana sipendi kabisa labda mtu anianze.
 
Inategemea na situation,but sipendi kuwa na hasira inaumiza...smtym namwaga chozi tu roho yangu nyeupee
 
Inategemea na situation, kama ni mpenzi wangu huwa nanyamaza na sinuni na ninamfanyia mema tena na zaidi hata kama yeye ana makosa. Baada ya siku 2 tukiwa katika hali ya furaha huwa namuuliza kwa upole na kama wakati wa tukio alinitukana au kuongea neno baya basi hapo chozi litashuka na unajua mpenzi akilia na kama mwapendana huwa ni nini kinafuata.... na kama ni mtu wa kawaida huwa nampuuza, sio jambo jema kutengeneza maadui bali kutengeneza marafiki. Unapompuuzia mtu na kuendelea kuwa kawaida huwa inamuumiza na kumtia aibu. Kurushiana maneno makali, matusi sio heshima bali ni kujishushia heshima. Huyo anayekutukana mchukulie kama ni kichaa vile, mpuuze.
 
Back
Top Bottom