Mbona kuna wanawake wameolewa wana miaka 40 na kuendelea na wamezaa watoto vizuri tu na ndoa zao zimedumu? Hapo ndipo jamii inapokosea kulazimisha nature ambayo haipo mbona wenzetu wazungu hawana hizi fikra potofu? Mimi ndo maana siku zote nawaambiaga watu wasikariri maisha
Msipende kuchukulia kila kitu in general kumbuka in every general rule there is always an exception maisha hayana kanuni moja ya kufikia malengo kuna watu wanaolewa wana miaka 20 na wanapofika miaka 40 wanaachika na hawaolewi tena na kuna watu wanaolewa wana miaka 40 na ndoa zinadumu hadi wanapofariki wakiwa na miaka 80
Jamani hii dunia kila mtu yupo kwenye safari yake ya maisha na kila mtu ana kusudi lake yaani kama ni mtihani kila mtu ana maswali yake tofauti na ya mwenzie ukijarubu kucopy tu kwa mwenzio umefeli ndoa anapanga Mungu na hakuna sehemu kwenye maandiko yametaja umri mahususi wa mwanaume kuoa au mwanamke kuolewa jamani hivi is it so hard for you guys to understand this?
Anyways endeleeni kuoa wanawake kwa sababu ya muonekano wao wa nje na kuwaona wenye umri mkubwa kuwa 'hawana jipya' and by the way sina any personal issues na wanaume ila huwa ninashangaa sijui kwanini inakuwa ngumu ninyi kuubali ukweli yaani mnang'ang'ania kile kilichopo kwa sababu mnaona kinawafaidisha hata kama kinatukandamiza sisi wanawake hilo hamjali