Ukiingia cha kike tarajia kuyaona ya kike

fakalava

JF-Expert Member
Jul 16, 2015
4,378
2,000
Amani iwe nanyi wadau,

Kuna uzi ulikuwa unaongelea jinsi gani magroup ya WhatsApp na mitandao mingine yanatumika vibaya kwa wanawake kufundishana tabia mbaya. Huu ni ukweli usiyopingika kuwa ndivyo ilivyo.

Ni dhahiri kuwa kila group hutengenezwa kwa kusudi maalumu likiwalenga watu maalumu, hivyo wahusika ujiunga kwa utashi wao japo kuna wachache ambao ushawishiwa.

Hapa mantiki yangu ni kuondoa mtazamo uliopo wa kuwaona kana kwamba ndiyo waovu kuliko wanaume.

Yapo magroup mengi ya wanaume kufundishana uhuni kama vile, jinsi ya kuchepuka, kuwa na wapenzi wengi bila kugundulika na mambo mengine kama hayo.

Kwa maana hiyo ukiingia huko tegemea kuyakuta mambo yafananayo na maudhui ya kundi husika, mara nyingine siyo wote kwenye kundi husika uyaishi maisha hayo ya kihuni. Katika makundi haya kuna watu wa aina tatu.
  1. Ambao ni halisi ndiyo maisha yao, hawa hiyo ndiyo ofisi.
  2. Wapweke: Hili ni kundi jingine ambalo hujikuta linaangukia huko kutafuta Kampani, hawa mara nyingi unaswa huko na kuwa watu hatari sana.
  3. Just for funny: Hawa wanapenda kujifurahisha kwa mambo yanayofanyika huko japo wao hawafanyi ila hutokea wachache kunaswa. Hili kundi wengi wao huwa ni wanandoa lakini hata masingo wamo.
  4. Experts/Retired Experts: Hili ndilo kundi hatali, hawa wameshakubuhu katika uhuni au wengine wameshastaafu, kazi yao ni kuwarubuni wengine waingie kwenye uhuni pengine hata kwa kuwachuuza. Janga hili huwaangukia wanawake wa uswahilini hasa ambao mitandao ni kitu kigeni kwao.

Mwisho: Jambo lingine linalowapotosha wanawake hasa wale fuata upepo, ni hivi vikundi vya kuchangiana.
 

kijani11

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
6,639
2,000
Katika maisha kuna watu wa kila aina. Na ndio hao hao tunaokutana na katika mitandao na magrupu ya mitandao.

Jua nini kinakufaa kisichokufaa achana nacho na kwa magrupu pia ukijua hilo mtu huwezi pata shida.

Yanini ukae grupu la watu wanazungumzia ulaji wa nyoka nawewe huli wala huna mpango wakula nyoka?!
 

fakalava

JF-Expert Member
Jul 16, 2015
4,378
2,000
Katika maisha kuna watu wa kila aina. Na ndio hao hao tunaokutana na katika mitandao na magrupu ya mitandao.

Jua nini kinakufaa kisichokufaa achana nacho na kwa magrupu pia ukijua hilo mtu huwezi pata shida.

Yanini ukae grupu la watu wanazungumzia ulaji wa nyoka nawewe huli wala huna mpango wakula nyoka?!
Ushauri mzuri Mkuu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom