Ukigomea sensa......utagomea na vitambulisho vya taifa?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukigomea sensa......utagomea na vitambulisho vya taifa?!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Anold, Jul 26, 2012.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,378
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Kuna watu wachache wanaofanya kampeni za kuhamasisha wananchi wasijitokeze kwenye sensa ya watu na makazi. kwangu mimi naona hiki ni kichekesho kingine, maana haiwezekeni ugomee sensa wakati tayari umeshajitokeza kwenye kujiandikisha kupata kitambulisho cha Taifa, watu watakwimu watakachokifanya ni kuoanisha takwimu na kufanya makadirio, hivyo hao wanaofanya kampeni za kukataza waumini wao nafikiri watafute mbinu nyingine inayoweza kuwasaidia kukwamisha zoezi hilo ila nijuavyo tayari chenga ya mwili washapigwa.

  Pili hata kwenye uandikishwaji wa vitambulisho vya Taifa kipengere cha dini hakimo vipi watu hawa wasiwahamasishe watu wao kugomea? maaana kitu wanachokifanya NIDA hakina Tofauti na zoezi la sensa, tena kama serikali ingejipanga vizuri ili kuepuka gharama zisizo na lazima wangeunganisha nguvu tu kwenye vitambulisho vya Taifa maana Tofauti za taarifa zilizopo kwenye dodoso la NIDA na sensa ni ndogo sana!!! Nafikiri kwa wale wanaogomea kuna tatizo la uelewa!!!!!

  Tatu dini ambayo itagomea sensa itapata hasara kubwa kwani idadi itakayopatikana ni dhahiri itasababisha dini ambayo haikugomea ione kuwa hiyo ndiyo idadi halisi ya waumini wao na hilo likitokea itakuwa ni hasara kubwa kwa dini iliyogomea!!!!!

  Nawatakia sensa njema kwa wale ambao hawatagoma!!
   
Loading...