Ukifanya hivi, hakika utafanikiwa

sylivesteralmas

New Member
Mar 4, 2019
2
1
Kwanza napenda kumshukuru Mungu kwa kunijalia uzima ambayo ni zawadi kubwa huku nikitumai kuwa hata wewe u mzima wa afya, pia nikushukuru wewe kwa kufanya kosa hili la kusoma thread hii kwani ukizingatia nakufanya, mafanikio ni yako.
Leo ningependa nikufundishe njia rahisi kabisa ya kufanikiwa katika unalo hitaji, haijalishi unataka uwe mwanasiasa mkubwa, msanii mkubwa. Photographer, mtangazaji, mwanasoka mkubwa na pengine unatamani kuwa tajiri mkubwa. Njia hii inaitwa " Tafuta alie fanikiwa kisha jaribu kufanya vitu vilivyo mpelekea afanikiwe "

Mfano 1: Unataka uwe Kama millardayo, Chunguza nini kinachofanya apige hatua zaidi katika kazi yake, mfano, anautumiaje muda, anaongeaje na watu, alianzaje na vitu vingine vingi utakavyoona vinakufaa.

Mfano 2: Unataka uwe tajiri, tafuta tajiri yoyote , fatilia kwa undani ,jinsi alivyo anza, ratiba yake kwa siku, mtazamo wake juu ya fursa na kazi, anahusiana vipi na watu na vingine vingi.

Mfano 3: Unataka uwe mwanasoka mkubwa, tafuta mwanasoka unaempenda na jaribu kufatilia alifanyaje na anafanyeje.

Nimatumaini yangu kuwa umepata kitu fulani cha kukusaidia ila kikubwa ni kutendea kazi, yaani " Information without execution is poverty "

GeItaGoLd blog. Soon karibu yako kukuelimisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilifatilia nikakuta ali lawitiwa akapata mafanikio
Nifatilia pia nikakuta mo alipewa mali na baba yake(urithi) akafanikiwa.
Nilifatilia nikakuta Alidhulumu wanyonge Akafanikiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilifuatilia nikakuta ni jambazi na muuaji

Sent using Jamii Forums mobile app
nimefatilia nikaja kugundua anauza unga
Nilifatilia nikakuta ni mshirikina balaa...
Hahahahaha,hizi coments zimenifurahisha sana.Yani ina maana hakuna muliyemfatilia mkakuta alianza kuuza genge la nyanya au kuuza nguo za mitumba mtaani?.Duuh,kweli mumempania mtoa mada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Timefatilia nimegundua Bwana SAIDI SALIMU (bakharesa) alianza kuokota makopo


Ngoja na mm nianze.....
 
Nilifatilia nikagundua sio mlipa koda kabisa ni mtu wa mishe za magumash magumash mda wote ila ndio anapesa mingi
 
Back
Top Bottom