Ukifanya haya jamii inaweza isikuelewe

Midavudavu

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
287
59
Kuna baadhi ya mambo ukiyafanya kutokana na hali na mazingira jamii inaweza isikuelewe je unalijua hilo?
1. Mchungaji kukutwa bar ukiwa mitungi kinoma
2. Kuvaa suti huku ukiwa na kandambili/yeboyebo
3. Kuingia katika eneo la ibada na suluari mlegezo au kimini
4. Kukutwa bar ukiwa umelewa huku umevaa kanzu na baraghashia
5. Kushangilia simba huku ukiwa umekaa katika jukwaa la yanga
6. Kundandia daladala huku ukiwa umevaa suti
7. Kuchuchumaa wakati wa kujisaidia haja ndogo wakati wewe ni mwanaume
8. Kujisaidia haja ndogo ukiwa umesimama wima wakati wewe ni mwanamke
9. .......................................................................:eek2:
 
1.kuanguka na kuzimia kwa sababu ya njaa mjini wakati mfukoni una msimbazi 50.
2.kufa kwa kiu wakati upo baharini.
3.kumchapa denti wa kike makalioni wakati huohuo ukipandisha sketi yake juu.
4.kulamba koni wakati wewe in mtu mkubwa kwa umri.
5.prezdaa kula 'lunch' kwa mama lishe.
 
Ukiwa mchungaji huku ukidai mganga anakusaidia sana kwenye mambo yako
 
No1 sio kihivyo sana.Ila 4 na 5 wanahasila hao balaa lazima ufe.Au piga mahesabu mwenyewe kitu tumepigwa mkono halafu upo jukwaa letu unashangilia lazima tuzae na wewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom