Ukifa, usijali kuhusu mwili wako...!

Somotimes sio kifo bali tunaowaach na wanaotuacha

Bab
Mam
Mke
Watoto
Jamaa zako


Very sad

Kifo chako binafs si issue
 
Very sad ni kwamba wote tutakufa[emoji22]

Kuna usiku mmoja nililala nikaota nimekufa, kwa kweli kuna upweke fulani niliuona ambao ulinikosesha amani, yani ni kwamba baada ya kuwa nimekufa nikawa nimetokea eneo fulani kama nyika hivi na nikatambua kuwa na mm nimekufa ,ila eneo hilo halina watu wengi ,ni kama eneo la watu wanao subiria kitu fulani, yani kila mtu yupo kivyake vyake.

Eneo hilo halina mwanga mkali kama wa mchana ,ni mwanga ambao upo kama inataka kunyesha mvua, au wakati jua limefunikwa na mawingu. Basi baada ya kujijua nimekufa nikaanza kuwaza mwenyewe kwamba, nilikuwa naambiwa kuna hukumu baada ya kufa sasa mimi itakuwaje kwa matendo yangu? ... Ila nikajipa moyo kwamba kama Mungu husamehe basi na mm nitasemehewa mana nilikumbuka kuwa kabla ya kulala usiku huo nilitubu. Nikawaida yangu kutubu na kuomba rehema kabla ya kulala kila mara,Hili nilifundishwa na mchungaji fulani.

Sasa eneo nililo fikia baada ya kugundua kuwa na mm ni miongoni mwa marehemu tayari, ni eneo ambalo linaupweke mno na zaidi ya yote kuna majuto fulani ya kuona ya kuwa maisha ya duniani si kitu, yaani unaona kabisa kama duniani ulikuwa unapoteza mda tu na kujilaumu baadhi ya mambo uliyokuwa ukiyafanya. Eneo hilo linarudisha picha nyuma ya maisha ya duniani harafu unaona hayakuwa na maana kabisa, kwa maana unajiona kabisa kuwa unaanza maisha mengine ambayo unakuwa haujui hatima yake.

Hii ndoto ilinishitua sana mana nilisituka usingizin ndo nikajua kumbe bado sijafa,ila hadi leo huwa najiiuliza ni nn maana ya ile ndoto.
 
Dah ee mola nisaidie kila nifanyalo nikumbuke napita maana nisipowaza hivyo nitajikweza bure

Rest easy my parents mliniacha imara japo i was too yangu japo mliniachia upweke baada ya ndugu wa pekee wa damu pia kuwafuata

Mshana Jr umenigusa sana na kunirudisha mbali sana be blessed kaka .[emoji120][emoji120]
 
Kaka umenipa tafakari nzito sanaa 🤦🏽‍♂️🤦🏽‍♂️

Ni vile binadamu tumeumbwa kufanya attachment kwa watu na vitu ila mwisho wa siku havitokuwa na maana kama hukuishi kwa furaha kwa kila sekunde

Kujijali na kujipenda kwanza ni muhimu zaidi kuliko kitu kingine chochote.. 🙏
 

Ayu 1:21​

"...Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe."
 
Mkuu una akili Sana ,ni wachache watakuelewa
 
Naogopa mauti, naogopa siku ambayo watu wataacha kuniita jina langu na kuniita marehemu....watanivua nguo zangu na kuniosha, huku siwezi kujitetea😭

Kinachonitisha naenda wapi? Nitakuwa Nani? Wakati huo sina huu mwili wangu mzuri nnaoupenda, sina Kazi, sina vyeti....vitachomwa Moto😭 sina familia wala kampani, nitakuwa wapi? Kama Nani? Nitapotea? Nitapoteaje?
 
Ndio maana tunatakiwa tusiwekeze kwenye roho zaidi kuliko mwili uharibikao..

Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…