Ukibahatika kuwa Kiongozi wa watu, jitahidi kujiepusha na majivuno

"Remembering that you are going to die is the best way I know to avoid the trap of thinking you have something to lose. You are already naked. There is no reason not to follow your heart.
========
=Steve Jobs
 
Nawasihi wale wote waliobahatika kuwa viongozi Wa watu, wadhamirie kuwa kuanzia 2018 hii watajiepusha na majivuno kwa kadiri watakavyoweza. Ni vyema kabla ya kuamua kufanya ama kutofanya chochote usikilize kwa makini sauti itokayo ndani yako na kujiridhisha juu matokeo ya lile utakalo kulifanya.

Mpaka kati ya uimara na udhaifu Wa mwanadamu ni mwembamba sana. Ni viungo kadhaa dhaifu sana ambavyo humfanya mwanadamu aweze kuendelea kuishi na kimoja tu kikifeli ndio basi tena. Mwanadamu anaweza kuinuliwa na akawa na heshima kubwa mbele ya wengine ndani ya muda mfupi tu, lakini pia Mungu anaweza kumshusha na kuwa dhalili ndani ya sekunde. Aidha, hata, mwanadamu awe na heshima kiasi gani katika dunia, anapoondoka waliobaki hawachukui muda kumsahau kana kwamba hakuwahi kuwepo.

Dunia ina watu mabilioni, kila Siku wengine wanazaliwa na wengine wanakufa. Pamoja na binadamu: dunia ina viumbe wengine mabilioni kwa mabilioni. Tunaamini dunia ni kubwa sana.

Hata hivyo dunia ni kakitu kadogo tu kwenye mfumo Wa jua. Humo kuna masayari makubwa zaidi ya dunia, kuna jua ambalo ukubwa wake ni Mara milioni ya dunia, kuna mwezi na nyota ambazo ni kubwa Mara milioni ya dunia n.k. Sasa tunaweza kudhani mfumo Wa jua ni mkubwa sana na bila shaka ndio hivyo.

Sasa mfumo Wa jua na makorokocho yake, uko ndani ya inayoitwa milk way galaxy ambayo ina madude mabilioni kwa mabilioni na mengi ni makubwa zaidi ya dunia.Hivyo mfumo Wa jua na na kasehemu kadogo tu kwenye milky way.

Nje ya hapo kuna ma galaxes mabilioni ambayo ndani yake kuna madubwana makubwa kama dunia au zaidi na yako kwa mabilioni.

Nje ya hapo, katika eneo ambalo halionekani hata kwa darubini Kali, inasadikika kuna galaxies nyingine zinaendelea kutokea kwa kasi ya mwanga.

Sasa jiulize Mwanadamu ni kitu gani!? Ndio maana katika vitabu vitukufu tumesisitizwa tusitembee juu ya dunia kwa kiburi na majivuno bila kujali karama wala bahati tulizonazo kwani sisi si imara vya kutosha!?

Ni kwa mantiki hiyo sasa, nawasihi viongozi wajiridhishe na dhamira zao kabla ya kuamua kufanya maamuzi ya aina Fulani yenye matokeo Fulani kwa wale wanaowaongoza.Hata ukibahatika kuwa na utajiri mkubwa au mafanikio yoyote, kuwa na tahadhali katika hili.

Naomba kumu acknowledge mdau alieleta Uzi Wa hapo chini kwani ndie alienisaidia kuweza kulifikiri jambo hili.
Kwa picha: Ufahamu kuhusu Ulimwengu


Kweli mkuu,hapo umenena,uongozi wa majivuno huwa haufai hata kidogo,wanaofanya hivi ni wale ambao hawajiamini katika nafasi hizo,wanachokitaa ni kuogopeka na wala siyo kuheshimka kwa matendo yao
 
Baada ya kila kitu kushindwa mmehamia kwenye misemo, na bado Raisi wetu hatikiswi na Mafisadi na wapiga Dili!
Raisi Magufuli hapo hapo usipinde hata mm 1 mpaka Mafisadi waishe!
Mwambie farao.......
 
Back
Top Bottom