Ni Mtawala asiyejielewa pekee anaweza kukubali kuwa raifiki wa chawa

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,559
41,078
Katika lugha ya picha, hutumika vitu au hata baadhi ya viumbe au wadudu kuelezea mahusiano ya mwanadamu na wanadamu wenzake:

Ndiyo maana huwa kuna misemo kama, 'pete na kidole', kuelezea urafiki ulioshibana baina ya watu wawili. Misemo mingine ni kama vile, 'kushambulia kama nyuki', kuonesha umoja wa wahusika katika kupambana kwa nguvu zote na kwa umoja dhidi ya adui. Mingineyo ni kama, 'usiwe kupe', maana yake usiishi kwa kuwanyonya wenzako.

Siku zote uhusiano wa mwanadamu na chawa, ni uhusiano wa uadui. Chawa akimwingia mwanadamu kwanza humdanganya kwa kuleta muwasho wa kuvutia, huku yeye akizidi kupata nafasi ya kunyonya damu ya mwanadamu. Mwanadamu akigundua chawa wameingia kwenye mavazi yake au kwenye nywele, hufanya kila jitihada kuwaangamiza kwa sababu anajua madhara ya chawa.

Leo hii kuna watu wamewahi kutangaza wazi tena hadharani kuwa wao ni chawa wa Rais. Sijui ni kwa kukosa akili au maarifa, watu hao wanaamini kuwa kwa kutangaza hivyo wamejiweka karibu na Rais. Na Rais naye, kwa kuzisikia kauli kama hizo, sijui kama anaona hiyo ni sifa au anaona ameletewa ujumbe wa wazi kuwa watu hao ni maadui zake yeye Rais.

Kama Rais atakubali kuwa rafiki wa MACHAWA, basi lazima atakuwa na hitilafu kichwani, kwa sababu tangu kale chawa, kama alivyo funza, kunguni, papasi au kupe, hajawahi kuwa rafiki wa mwanadamu. Mwanadamu ametafuta kila mbinu ya kumwangamiza chawa kwa sababu ni adui wa afya ya mwanadamu.

Machawa, hakika jina lao limeakisi uhakisia wao. Wote wanaojiita au wanaojulikana ni machawa, ni maadui wa Taifa letu. Na ni maadui wa kila kiongozi anayejitambua.
 
Siku zote uhusiano wa mwanadamu na chawa, ni uhusiano wa uadui. Chawa akimwingia mwanadamu kwanza humdanganya kwa kuleta muwasho wa kuvutia, huku yeye akizidi kupata nafasi ya kunyonya damu ya mwanadamu. Mwanadamu akigundua chawa wameingia kwenye mavazi yake au kwenye nywele, hufanya kila jitihada kuwaangamiza kwa sababu anajua madhara ya chawa.
Hi falsafa imefichua siri nyingi
 
Katika lugha ya picha, hutumika vitu au hata baadhi ya viumbe au wadudu kuelezea mahusiano ya mwanadamu na wanadamu wenzake:

Ndiyo maana huwa kuna misemo kama, 'pete na kidole', kuelezea urafiki ulioshibana baina ya watu wawili. Misemo mingine ni kama vile, 'kushambulia kama nyuki', kuonesha umoja wa wahusika katika kupambana kwa nguvu zote na kwa umoja dhidi ya adui. Mingineyo ni kama, 'usiwe kupe', maana yake usiishi kwa kuwanyonya wenzako.

Siku zote uhusiano wa mwanadamu na chawa, ni uhusiano wa uadui. Chawa akimwingia mwanadamu kwanza humdanganya kwa kuleta muwasho wa kuvutia, huku yeye akizidi kupata nafasi ya kunyonya damu ya mwanadamu. Mwanadamu akigundua chawa wameingia kwenye mavazi yake au kwenye nywele, hufanya kila jitihada kuwaangamiza kwa sababu anajua madhara ya chawa.

Leo hii kuna watu wamewahi kutangaza wazi tena hadharani kuwa wao ni chawa wa Rais. Sijui ni kwa kukosa akili au maarifa, watu hao wanaamini kuwa kwa kutangaza hivyo wamejiweka karibu na Rais. Na Rais naye, kwa kuzisikia kauli kama hizo, sijui kama anaona hiyo ni sifa au anaona ameletewa ujumbe wa wazi kuwa watu hao ni maadui zake yeye Rais. Kama Rais atakubali kuwa rafiki wa MACHAWA, basi lazima atakuwa na hitilafu kichwani, kwa sababu tangu kale chawa, kama alivyo funza, kunguni, papasi au kupe, hajawahi kuwa rafiki wa mwanadamu. Mwanadamu ametafuta kila mbinu ya kumwangamiza chawa kwa sababu ni adui wa afya ya mwanadamu.

Machawa, hakika jina lao limeakisi uhakisia wao. Wote wanaojiita au wanaojulikana ni machawa, ni maadui wa Taifa letu. Na ni maadui wa kila kiongozi anayejitambua.
Suala hili si rahisi kulielezea ila linafikirisha. Katika historia kuna maswali kama kwa nini Wajerumani na akili zao waliruhusu Hitler akaua binadamu wengi kiasi hicho? Jibu ni kwamba katika kila jamii huwa kunatokea wakati ambao sehemu kubwa ya jamii inarubuniwa na viongozi wachache waovu na kuifanya jamii ikubali mambo maovu kuwa ndiyo utaratibu wa kawaida! Mfano wa Tanzania si tofauti au Israel ya sasa ambayo haijali kumwaga damu ya mtu mwingine. Huchukua muda jamii ya namna hiyo kurudi kwenye mstari unaolingana na viwango vya dunia. Kuna waandishi wa historia ambao wameelezea hali ya namna hiyo hutokeaje.
 
Taasisi ya urais siku hizi imekuwa ya kijinga sana.Ikulu imekuwa kama sehemu ya kucheza mpira wa miguu na nyumba ya biashara ya Soko huria.
 
Back
Top Bottom