Ukibahatika kuwa Kiongozi wa watu, jitahidi kujiepusha na majivuno

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,427
Nawasihi wale wote waliobahatika kuwa viongozi Wa watu, wadhamirie kuwa kuanzia 2018 hii watajiepusha na majivuno kwa kadiri watakavyoweza. Ni vyema kabla ya kuamua kufanya ama kutofanya chochote usikilize kwa makini sauti itokayo ndani yako na kujiridhisha juu matokeo ya lile utakalo kulifanya.

Mpaka kati ya uimara na udhaifu Wa mwanadamu ni mwembamba sana. Ni viungo kadhaa dhaifu sana ambavyo humfanya mwanadamu aweze kuendelea kuishi na kimoja tu kikifeli ndio basi tena. Mwanadamu anaweza kuinuliwa na akawa na heshima kubwa mbele ya wengine ndani ya muda mfupi tu, lakini pia Mungu anaweza kumshusha na kuwa dhalili ndani ya sekunde. Aidha, hata, mwanadamu awe na heshima kiasi gani katika dunia, anapoondoka waliobaki hawachukui muda kumsahau kana kwamba hakuwahi kuwepo.

Dunia ina watu mabilioni, kila Siku wengine wanazaliwa na wengine wanakufa. Pamoja na binadamu: dunia ina viumbe wengine mabilioni kwa mabilioni. Tunaamini dunia ni kubwa sana.

Hata hivyo dunia ni kakitu kadogo tu kwenye mfumo Wa jua. Humo kuna masayari makubwa zaidi ya dunia, kuna jua ambalo ukubwa wake ni Mara milioni ya dunia, kuna mwezi na nyota ambazo ni kubwa Mara milioni ya dunia n.k. Sasa tunaweza kudhani mfumo Wa jua ni mkubwa sana na bila shaka ndio hivyo.

Sasa mfumo Wa jua na makorokocho yake, uko ndani ya inayoitwa milk way galaxy ambayo ina madude mabilioni kwa mabilioni na mengi ni makubwa zaidi ya dunia.Hivyo mfumo Wa jua na na kasehemu kadogo tu kwenye milky way.

Nje ya hapo kuna ma galaxes mabilioni ambayo ndani yake kuna madubwana makubwa kama dunia au zaidi na yako kwa mabilioni.

Nje ya hapo, katika eneo ambalo halionekani hata kwa darubini Kali, inasadikika kuna galaxies nyingine zinaendelea kutokea kwa kasi ya mwanga.

Sasa jiulize Mwanadamu ni kitu gani!? Ndio maana katika vitabu vitukufu tumesisitizwa tusitembee juu ya dunia kwa kiburi na majivuno bila kujali karama wala bahati tulizonazo kwani sisi si imara vya kutosha!?

Ni kwa mantiki hiyo sasa, nawasihi viongozi wajiridhishe na dhamira zao kabla ya kuamua kufanya maamuzi ya aina Fulani yenye matokeo Fulani kwa wale wanaowaongoza.Hata ukibahatika kuwa na utajiri mkubwa au mafanikio yoyote, kuwa na tahadhali katika hili.

Naomba kumu acknowledge mdau alieleta Uzi Wa hapo chini kwani ndie alienisaidia kuweza kulifikiri jambo hili.
Kwa picha: Ufahamu kuhusu Ulimwengu
 
Na hiyo ndio tafasiri sahihi ya ULEVI WA MADARAKA.
 
Akiwa na afya njema bas binaadamu hujisahau na kudhan kana kwamba ataishi milele lakin wap.wamepita wengi wenye nguvu na vituko bas hata cc tutapita na history itabaki kuwa walikuwepo
 
Nawasihi wale wote waliobahatika kuwa viongozi Wa watu, wadhamirie kuwa kuanzia 2018 hii watajiepusha na majivuno kwa kadiri watakavyoweza. Ni vyema kabla ya kuamua kufanya ama kutofanya chochote usikilize kwa makini sauti itokayo ndani yako na kujiridhisha juu matokeo ya lile utakalo kulifanya.

Mpaka kati ya uimara na udhaifu Wa mwanadamu ni mwembamba sana. Ni viungo kadhaa dhaifu sana ambavyo humfanya mwanadamu aweze kuendelea kuishi na kimoja tu kikifeli ndio basi tena. Mwanadamu anaweza kuinuliwa na akawa na heshima kubwa mbele ya wengine ndani ya muda mfupi tu, lakini pia Mungu anaweza kumshusha na kuwa dhalili ndani ya sekunde. Aidha, hata, mwanadamu awe na heshima kiasi gani katika dunia, anapoondoka waliobaki hawachukui muda kumsahau kana kwamba hakuwahi kuwepo.

Dunia ina watu mabilioni, kila Siku wengine wanazaliwa na wengine wanakufa. Pamoja na binadamu: dunia ina viumbe wengine mabilioni kwa mabilioni. Tunaamini dunia ni kubwa sana.

Hata hivyo dunia ni kakitu kadogo tu kwenye mfumo Wa jua. Humo kuna masayari makubwa zaidi ya dunia, kuna jua ambalo ukubwa wake ni Mara milioni ya dunia, kuna mwezi na nyota ambazo ni kubwa Mara milioni ya dunia n.k. Sasa tunaweza kudhani mfumo Wa jua ni mkubwa sana na bila shaka ndio hivyo.

Sasa mfumo Wa jua na makorokocho yake, uko ndani ya inayoitwa milk way galaxy ambayo ina madude mabilioni kwa mabilioni na mengi ni makubwa zaidi ya dunia.Hivyo mfumo Wa jua na na kasehemu kadogo tu kwenye milky way.

Nje ya hapo kuna ma galaxes mabilioni ambayo ndani yake kuna madubwana makubwa kama dunia au zaidi na yako kwa mabilioni.

Nje ya hapo, katika eneo ambalo halionekani hata kwa darubini Kali, inasadikika kuna galaxies nyingine zinaendelea kutokea kwa kasi ya mwanga.

Sasa jiulize Mwanadamu ni kitu gani!? Ndio maana katika vitabu vitukufu tumesisitizwa tusitembee juu ya dunia kwa kiburi na majivuno bila kujali karama wala bahati tulizonazo kwani sisi si imara vya kutosha!?

Ni kwa mantiki hiyo sasa, nawasihi viongozi wajiridhishe na dhamira zao kabla ya kuamua kufanya maamuzi ya aina Fulani yenye matokeo Fulani kwa wale wanaowaongoza.

Naomba kumu acknowledge mdau alieleta Uzi Wa hapo chini kwani ndie alienisaidia kuweza kulifikiri jambo hili.
Kwa picha: Ufahamu kuhusu Ulimwengu

Baada ya kila kitu kushindwa mmehamia kwenye misemo, na bado Raisi wetu hatikiswi na Mafisadi na wapiga Dili!
Raisi Magufuli hapo hapo usipinde hata mm 1 mpaka Mafisadi waishe!
 
Mkuu, mada hii haihusiani kabisa na Rais. Sijui wewe umeihusishaje na Rais? Mada hii inakuhusu wewe hapo ulipo. Jenga tabia ya kusoma vitu uelewe kabla ya kuchangia na uache ushabiki usio Wa lazima. Hatuwezi kufanikiwa kwa kuendekeza ushabiki hata kusikostahili.

Raisi wetu hatishiwi nyau!
 
Natamani hekima iwepo na idumu katika kuifanya Tanzania bora. Vihoja na hoja viwe sawia kiwepo na upendo na ukuaji Wa uchumi Imara. Natumaini hili la bwana Aziz halimgusa MTU yeyote ni tafakuri ya ujumla. Ahsanteni.
 
Na kumbuka uongozi ni kama koti la kuazima. Ukilingangania utanyanganywa na kuumbuka juu
 
Usisahau kuwa pana jamii zingine kama wewe ni kiongozi bila kuwa na majivuno kamwe hutaweza kuwa kiongozi kwenye hizo jamii/ nchi.

Pride in leadership its a subjective and not objective matter...in administration, management or governing.
 
Baada ya kila kitu kushindwa mmehamia kwenye misemo, na bado Raisi wetu hatikiswi na Mafisadi na wapiga Dili!
Raisi Magufuli hapo hapo usipinde hata mm 1 mpaka Mafisadi waishe!

Ukivua hirizi kiuononi utaacha kukurupukia mambo.KATUBU KWANZA.
 
Raisi wetu hatishiwi nyau!
Usitegemee sana hayo mahirizi viunoni , mengi yamefungwa bangi , mkaa na mfupa wa nguruwe tu .

Unajua kwanini waganga wa kienyeji hawaagizi mchicha na matembele na badala yake wanaagiza kuku na mbuzi ?
 
Nawasihi wale wote waliobahatika kuwa viongozi Wa watu, wadhamirie kuwa kuanzia 2018 hii watajiepusha na majivuno kwa kadiri watakavyoweza. Ni vyema kabla ya kuamua kufanya ama kutofanya chochote usikilize kwa makini sauti itokayo ndani yako na kujiridhisha juu matokeo ya lile utakalo kulifanya.

Mpaka kati ya uimara na udhaifu Wa mwanadamu ni mwembamba sana. Ni viungo kadhaa dhaifu sana ambavyo humfanya mwanadamu aweze kuendelea kuishi na kimoja tu kikifeli ndio basi tena. Mwanadamu anaweza kuinuliwa na akawa na heshima kubwa mbele ya wengine ndani ya muda mfupi tu, lakini pia Mungu anaweza kumshusha na kuwa dhalili ndani ya sekunde. Aidha, hata, mwanadamu awe na heshima kiasi gani katika dunia, anapoondoka waliobaki hawachukui muda kumsahau kana kwamba hakuwahi kuwepo.

Dunia ina watu mabilioni, kila Siku wengine wanazaliwa na wengine wanakufa. Pamoja na binadamu: dunia ina viumbe wengine mabilioni kwa mabilioni. Tunaamini dunia ni kubwa sana.

Hata hivyo dunia ni kakitu kadogo tu kwenye mfumo Wa jua. Humo kuna masayari makubwa zaidi ya dunia, kuna jua ambalo ukubwa wake ni Mara milioni ya dunia, kuna mwezi na nyota ambazo ni kubwa Mara milioni ya dunia n.k. Sasa tunaweza kudhani mfumo Wa jua ni mkubwa sana na bila shaka ndio hivyo.

Sasa mfumo Wa jua na makorokocho yake, uko ndani ya inayoitwa milk way galaxy ambayo ina madude mabilioni kwa mabilioni na mengi ni makubwa zaidi ya dunia.Hivyo mfumo Wa jua na na kasehemu kadogo tu kwenye milky way.

Nje ya hapo kuna ma galaxes mabilioni ambayo ndani yake kuna madubwana makubwa kama dunia au zaidi na yako kwa mabilioni.

Nje ya hapo, katika eneo ambalo halionekani hata kwa darubini Kali, inasadikika kuna galaxies nyingine zinaendelea kutokea kwa kasi ya mwanga.

Sasa jiulize Mwanadamu ni kitu gani!? Ndio maana katika vitabu vitukufu tumesisitizwa tusitembee juu ya dunia kwa kiburi na majivuno bila kujali karama wala bahati tulizonazo kwani sisi si imara vya kutosha!?

Ni kwa mantiki hiyo sasa, nawasihi viongozi wajiridhishe na dhamira zao kabla ya kuamua kufanya maamuzi ya aina Fulani yenye matokeo Fulani kwa wale wanaowaongoza.Hata ukibahatika kuwa na utajiri mkubwa au mafanikio yoyote, kuwa na tahadhali katika hili.

Naomba kumu acknowledge mdau alieleta Uzi Wa hapo chini kwani ndie alienisaidia kuweza kulifikiri jambo hili.
Kwa picha: Ufahamu kuhusu Ulimwengu
Kwani majivuno maana yake nini?
 
Baada ya kila kitu kushindwa mmehamia kwenye misemo, na bado Raisi wetu hatikiswi na Mafisadi na wapiga Dili!
Raisi Magufuli hapo hapo usipinde hata mm 1 mpaka Mafisadi waishe!
Kwanini nyie misikule hamzungumziagi ufidadi wake akiwa waziri kama MV dar na uporaji wa nyumba za uma?
 
Angalia kwenye kamusi ya kiswahili.
Nilitaka unavyoielewa wewe sio tafsiri ya kamusi!Ningetaka ya amusi ningeitafuta.Mtu mwingine akiona mwenzie kanunua gari zuri,kajenga nyumba nzuri,anavaa vizuri basi anaringa,kumbe hiyo siyo maana ya kuringa.
Ila ngoja nikusaidie,majivuno ni ile hali ya kujiona bora kuliko wengine.Sasa uliyemkusudia ana majivuno?
 
Nilitaka unavyoielewa wewe sio tafsiri ya kamusi!Ningetaka ya amusi ningeitafuta.Mtu mwingine akiona mwenzie kanunua gari zuri,kajenga nyumba nzuri,anavaa vizuri basi anaringa,kumbe hiyo siyo maana ya kuringa.
Wewe kama hukuelewa mada ndio ulipaswa kusema wapi hukuelewa na kwa nini! Suala la Mimi naelewaje, naelewa kama mada ya msingi inavyojipambanua.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom