Joseverest
JF-Expert Member
- Sep 25, 2013
- 52,470
- 70,588
Habari za muda huu wana MMU,
Nimefanya 'kautafiti kangu kasicho rasmi' nikagundua maneno haya kutoka kwa wanawake wakikwambia usiwaamini hata kidogo..
Karibuni mchangie mada, ukiwa na la kuongezea ongezea ili tujifunze.
1.Ungejua wala sina haraka ya kuolewa!
Hakuna mwanamke ambaye yuko tayari kuona umri unamkimbia, ameshahudhuria harusi za marafiki zake, pengine ameshaliona mpaka gauni litakalompendeza harusini halafu eti akuambie hana haraka ya kuolewa!
2. Ngoja Nikavae, nipe dakika tano tu!
Ukiambiwa hivi, basi Kama hujanywa soda muda mrefu huu ndo muda muafaka! Tafuta sehemu yenye utulivu upate kinywaji chako maana hizo dakika tano ni dakika hamsini!
3.Wala sioni wivu ukiwa unawaangalia wanawake wengine
Akikuambia hivi, anataka tu akuonyeshe ni jinsi gani amekua kiakili, na ni mtu muelewa saana.. lakini moyoni mwake anatamani kukupiga makofi unapomuangalia msichana mwingine huku akijiuliza moyoni, kwani huyo anaemuangalia amenishinda nini?
4.Hata kama unapata mshahara mdogo, mi nimeridhika kabisa.. (mmmh Kweli?)
5.Mbona dada yako hajaja kututembelea muda mrefu? Nime”mmiss” sana!
Mara chache sana kutakuwepo na upendo kati ya mpenzi wako na dada yako au hata mama. Kwa mwanamke ni bora umletee wadogo zako wa kiume kumi nyumbani atawalea ila sio dada yako mmoja!
6.Napenda kila kitu kutoka kwako
Unadanganywa! lazima kuna kitu angalau kimoja angependa ubadilike au anapanga kukubadilisha.. mara nyingine atataka hata uwe kama Yule kaka anayemuona kwenye tamthilia!
7.Sihitaji kuwa na mwanaume kwa sasa.
Niko “busy” sana! Au utaambiwa nimeumizwa sana hata kama yeye ndiye mgonvi namba moja!
8.Wala sina njaa, mi nikila kidogo tu nashiba!
9.Niko sawa tu, hamna shida!
Ukweli ni kwamba anataka uongeze juhudi kumbembeleza ili akuambie ni nini shida.
10.Simuambii yeyote!
Hapo imekula kwako usitegemee atakaa nalo moyoni!