Ukiachwa achika!!

Ukiachwa achika!!

Huu ni ungese aiseeeh, ukisikia ukichaa ndo huu. Ila kwa upande mwingine kama mtu anaona nimemkosea sana na anataka kunikera, bora avunje hivyo ila aniachie mwili wangu, maana ntapambana nipate pesa nyingine na niendelee mbele bila yeye.

Poleni wahanga wa hilo tukio, ukute bidada alikuwa anajinunulisha vyombo na kupendezesha geto la mwanaume halafu anasikia anaolewa mwingine. Ila hata kama anaolewa mwingine ukifanya hivo ndo unazidi kujiharibia.

Acha niendelee na Mahaba yangu Mia Mia na Dadii aka Nonsense.
Wee mimi hata sivunji. Kama nilinyunua mimi nabeba naenda navyo
 
Hiyo ni busara na kupevuka akili, kama bvitu ulighara mia unavibeba tuu. Ila kama ulimpa zawadi ni hiari kuvichukua au kumuachia.

Umenikumbusha case moja binti wakati anaolewa kafanyiwa house party maana ile haikuwa kichen party. Alipewa zawadi na familia yake vitu vya kuanzia maisha vya kujaza nyumba nzima, kitanda godoro vyombo friji makochi dining table washing machine jiko la mkaa na umeme deep frizer makabati ya nguo makapeti picha za ukutani hadi nguo za kuvaa mumewe pia liletewa kama zawadi.

Baada ya harusi binti kaleta fuso kwa mumewe na mizawadi aliyopewa kwenye house party (kitchen party) akamshawishi mumewe vile vitu vyake (alivyomkuta navyo mwanaume) avipeleke kijijini kwao au avigawe au aviuze ili nyumba ijazwe na zawadi alizopewa binti.
Mume bila kuwaza mara mbili kasema sawa fuso likashusha mzigo utasema Orca Deco imehamia nyumbani kwao. Baada ya miaka 2 ya ndoa binti akaanza kuona kekundu kekundu kila akiongea na mwezie anajibiwa nyodoo..... akasema huyu hanijui, siku ya siku kachukua kichanga chake kakipeleka kwao (kwa wazazi wa binti), alishatafuta nyumba ya kupanga wilaya nyingine na waliyokuwa wakiishi na mumewe, akaita fuso akasafisha nyumba nzima akaacha funguo kwa majirani.

Mwanaume kurudi usiku wa manane yuko tips, piga honi piga na wewe, piga simu ya mkewe piga an wewe ikabidi alale kwenye gari nje ya nyumba yao. Asubuhi majirani wanamgongea kwenye gari wakampa funguo za nyumba yake. Kuingia ndani anakutana na mwangi hakuna hata nguo zake za ndani maana alinunuliwa hadi boksa hadi soksi. Zile za kwake za zamani zote aliziondoa kwa kuzitupa na vitu vingine aligawa......

Jamaa kupiga mahesabu ya haraka haraka hadi aje ajipange kukaa sawa akaenda kuomba msamaha mjkewe arudi akajishusha kama mtumwa, mke alirudi ila alinyanyasika hadi ukawa unaona huzuni.

Moral of the story; kwenye mahusiano chochote chaweza kutokea, kila mmoja asiishi maisha ya kumtegemea mwnzake saanaa kiasi cha kunyanyasika. Mnaishi kwa kusaidiana ila kila mmoja aishi au awe kwenye nafasi ya iwapo mmoja wapo hatokuwepo tena kwenye maisha yake haitakuwa mwisho wa maisha ya huyo aliyebaki maana maisha yanatakiwa kuendelea kama kawaida.

Kasie Matata.
 
Hahaha aisee dawa ya jeuri kiburi. Nimependa hapo kwenye funzo

inanikumbusha juzi kati jirani yangu alipokuja amekimbia kwangu na kunikabidhi funguo za gari na kuniambia nilipeleke nikalifiche popote ninapojua maana mke wake alikuwa ameshaanza kupasua vitu ndani hivyo angetoka nje na kumalizia kupasua gari.nikamwambia si umpige kichwa azimie akija kushituka ajikute mochwari.
 
Na yeye anajua hana ticket ya kurudi. Mtu hawezi kufanya mambo ya kizwazwa namna hiyo alafu awe na wazo la kurudi humo ndani. Halafu wakati anafanya hayo yote mwenye nyumba alikuwa wapi? Huyo mwanaume atakuwa kaka yetu hapa Dar
Akisema naomba funguo nikachukue vitu vyangu utamnyima!?
 
Hiyo ni busara na kupevuka akili, kama bvitu ulighara mia unavibeba tuu. Ila kama ulimpa zawadi ni hiari kuvichukua au kumuachia.

Umenikumbusha case moja binti wakati anaolewa kafanyiwa house party maana ile haikuwa kichen party. Alipewa zawadi na familia yake vitu vya kuanzia maisha vya kujaza nyumba nzima, kitanda godoro vyombo friji makochi dining table washing machine jiko la mkaa na umeme deep frizer makabati ya nguo makapeti picha za ukutani hadi nguo za kuvaa mumewe pia liletewa kama zawadi.

Baada ya harusi binti kaleta fuso kwa mumewe na mizawadi aliyopewa kwenye house party (kitchen party) akamshawishi mumewe vile vitu vyake (alivyomkuta navyo mwanaume) avipeleke kijijini kwao au avigawe au aviuze ili nyumba ijazwe na zawadi alizopewa binti.
Mume bila kuwaza mara mbili kasema sawa fuso likashusha mzigo utasema Orca Deco imehamia nyumbani kwao. Baada ya miaka 2 ya ndoa binti akaanza kuona kekundu kekundu kila akiongea na mwezie anajibiwa nyodoo..... akasema huyu hanijui, siku ya siku kachukua kichanga chake kakipeleka kwao (kwa wazazi wa binti), alishatafuta nyumba ya kupanga wilaya nyingine na waliyokuwa wakiishi na mumewe, akaita fuso akasafisha nyumba nzima akaacha funguo kwa majirani.

Mwanaume kurudi usiku wa manane yuko tips, piga honi piga na wewe, piga simu ya mkewe piga an wewe ikabidi alale kwenye gari nje ya nyumba yao. Asubuhi majirani wanamgongea kwenye gari wakampa funguo za nyumba yake. Kuingia ndani anakutana na mwangi hakuna hata nguo zake za ndani maana alinunuliwa hadi boksa hadi soksi. Zile za kwake za zamani zote aliziondoa kwa kuzitupa na vitu vingine aligawa......

Jamaa kupiga mahesabu ya haraka haraka hadi aje ajipange kukaa sawa akaenda kuomba msamaha mjkewe arudi akajishusha kama mtumwa, mke alirudi ila alinyanyasika hadi ukawa unaona huzuni.

Moral of the story; kwenye mahusiano chochote chaweza kutokea, kila mmoja asiishi maisha ya kumtegemea mwnzake saanaa kiasi cha kunyanyasika. Mnaishi kwa kusaidiana ila kila mmoja aishi au awe kwenye nafasi ya iwapo mmoja wapo hatokuwepo tena kwenye maisha yake haitakuwa mwisho wa maisha ya huyo aliyebaki maana maisha yanatakiwa kuendelea kama kawaida.

Kasie Matata.
Hivi hii jeuri miaka hii inatokea wapi mbona kipindi hicho mama zetu hawakuwa nayo !?!
 
Unajua nini, sio tu zama zimebadilika ulimwengu unakwenda kwa kasi sana na mambo yake yamekuwa vululu vululu. Ni jamii chache sana sasa hivi duniani ambazo bado zinaishi kwa misingi ya kuheshimu familia. Namaanisha kuna kizazi kiliacha kuafanya majukumu yake ndio maana unayaona haya yanayotokea kipindi hiki tunachoishi sasa hivi.

Kwanza turudi nyuma kizazi ambacho harusi ilikuwa inaishia kwenye kiwango cha familia na majirani hapo hata makwaruzano ya hiyo ndoa wataojua ni familia tena watu wa karibu na majirani. Siku hizi unaweza ukaenda kwenye harusi au ukajikuta unashiriki harusi ila bibi harusi humjui hujawahi kumuona, wazazi wake huwajui wala hujawahi kuwaona ila unajikuta na wewe ni mwanakamati kisa mtu unayejuana nae ni binamu wa wazazi wa bibi harusi na ndie aliyekuomba mchango na ukajikuta ni mwanakamati.

Sasa mtu ambaye sio ndugu wa karibu na maharusi mkijikuta familia wanamuachia huyo mwanakamati kuleta mapendekezo bila kujali baadae yataleta athari kwa wanandoa hao. Ndo mtu utasikia jamani bibi harusi asiende kunyanyasika huko anakoolewa akingie kwenye familia wajue kuwa binti ametoka familia ambayo iko vizuri, tuhakikishe kamati tutoe michango ya kutosha bibi harusi aende kwake na zawadi kibao ili mumewe na ndugu zake wamuheshimu..... hapo ndo makosa huanza.

Simemi binti au vijana wasipewe zawadi siku ya harusi ila kila kitu kiwe na kiasi, mkiwanunulia maharusi kila kitu kwenye nyumba yao wao watafanya juhudi gani kwwnye maisha?? ni sawa na mtoto unampeleka shule unamlipia ada unamlipia tuition na bado ikifika mtihani wa taifa unamnunulia feki ili afaulu......( huyu mzazi wa hivi unajiuliza akili yake iko sawa..... kama na yeye huyo mzazi alifanyiowa hivyo na wazazi wake basi kosa lilianzia huko nyuma).

Malezi yamebadilika sana na yanaleta athari nyingi sana kwenye familia / ndoa za leo....

Ni mambo mengi sana ambayo yamesababisha wasichana au wamama wa leo kuwa na kiburi hiko ambacho mama zatu / bibi zetu wa zamani hawakuwa navyo.

Swali nini kifanyike??!!...... suluhisho ni nini?

Je ile elimu iliyokuwa inatolewa kipindi kile tunasoma middle school na baadae ikaja elimu ya ujamaa na kujitegemea ilisaidia kuweka familia imara na kila mmoja kutimiza wajibu wake? kwanini ile elimu imeachwa? au bado inafundishwa? je watu wanafundishwa na kukuzwa kujitegemea an kuwa na ujamaa?

Je wanajua ujamaa ni nini? wanajua kujitegemea ni nini?

Watoto wa leo hadi wako na miaka 40 bado wanategemea support za wazazi wao, mzazi alipwe pension ndo amsaidie mwane wa kiume kujenga nyumba au kusomesha wanae.....

Kila mahali vurugu vululu na tunaona huko mitaani...

Eeeehh nimeandika mengi sana acha niishie hapa.
 
Back
Top Bottom