Ukiacha matumizi ya Mapambo, nini Kipo nyuma ya uthaman wa Dhahabu?

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,651
14,318
Nmekuwa nikijiuliza hili swali muda mrefu. Ukiacha kuwa dhahabu inatumika kutengenezea mapambo au kuonesha utajiri nini kingine kinachoipa dhahabu uthaman?

Wazo nililo nalo ni kuwa uthaman wa dhahab kwa kiasi kikubwa umesababishwa na binadamu wenyewe na si matumizi yake. Mfano dhahabu ingekuwa ni dawa ya kutibu cancer hapo tungesema inaokoa uhai wa mtu. Dhahabu ingekuwa inatumika kuungia mifupa hapo pia tungesema hilo ni jambo la kipekee la dhahabu.

Lakini kama ni mapambo, kama ni kuonesha tu utajiri wa mtu basi ni waz thaman hii ilipachikwa na binadamu. Kama ambavyo tuchukulie glass ingekuwa ni madini yanayochimbwa ardhin na yanapatikana kwa nadra basi glass ingekuwa na thaman sana.

Kama ingekuwa kioo ni aina flan ya madin ukichimba sehem unayapata yakiwa katika hali hiyo ya ukioo basi ingekuwa ni issue kubwa sana na wenye vioo wangekuwa wanaonekana wana utajiri sana.

Naombeni mnisaidie mbali na kutumika kama mapambo dhahabu inatumikaje zaidi. Na je kuna uhusiano gani wa dhahabu na ulimwengu wa roho? Almas wanasema ni moja ya madini yenye thaman kubwa lakini naona kama dhahab inaongoza hata tukizungumzia ulimwengu mzuri tunaoujenga kichwan tutasema kuna majumba ya dhahabu au vyombo vya dhahabu. Na hapo ukiniuliza tofaut ya anayekunywa juice kwenye kikombe cha udongo na anayekunywa kwenye kikombe cha dhahabu ni nini.

Bado utagundua dhahab kama dhahab haina thaman kama haijapewa uthaman na binadamu. Maji yana thaman kubwa sana kuliko dhahabu. Sema kwa vile maji ni mengi basi yamepoteza uthaman. Lakini ikiwa umetupwa katikat ya pori kubwa upo peke yako ukaambiwa uchague kilo 20 za dhahabu na lita 20 za maji kipi kitakuwa na thaman kwako?

Uthaman wa dhahabu ni wa kupandikizwa na binadamu. Dhahab kama dhahabu haina thaman. Isipokuwa binadamu waliamua kuipatia thaman hiyo.

Dhahabu haina thamana ya kiasili. Yaani toka inapoonekana na mtu wa kwanza ikawa na dhaman. Kwa mfano adam na eva dhahabu wao wangefanyia nini?ingewafaa nini?matumizi mengine ambayo tumekuja kuya ambatanisha na dhahabu nayo si ya kipekee. Kwa maana ya kuwa hakuna mbadala. Unakuwepo mbadala. Nini mahitaji ya asili ya dhahabu ambayo ni pekee hayajaambatanishwa na binadamu au kama yameambatanishwa na binadamu basi hamna mbadala wake na hivyo kuifanya dhahabu kuwa kitu cha kipekee.
 
Wazo na swali lenye mantiki kubwa. Ninachoweza kuongeza ni kwamba binadamu tunatumia sehemu kibwa ya uchumi/mali (fedha) kwa vitu vinavyombulisha utajiri tulio nao badala ya afya zetu. Vitu hivyo tunavipa thamani kubwa kuliko vinavyoongeza afya au uchumi.

Kwa mfano kilo ya nyama ni ghali kuliko ya mboga za majani. Glass ya mvinyo ni ghali kuliko ya maji. Lakini athari ya nyama au mvinyo kwa afya ya binadamu ni kubwa maradufu.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Niliwahi kuwa na fikra hizo pia, dhahabu imepewa.thaman hiyo lakini kiuhalisia sio sawa
 
Badala ya kutunza mapesa mengi taasisi kubwa kama Roman Catholic hununua dhahabu na kuihifadhi kama mbadala wa kuweka pesa.
Kwahyo kazi nyingine ya dhahabu ni kama hiyo kwa mataasisi flani yenye fedha kuzihifadhi kupitia madini hayo.
 
Wazo na swali lenye mantiki kubwa. Ninachoweza kuongeza ni kwamba binadamu tunatumia sehemu kibwa ya uchumi/mali (fedha) kwa vitu vinavyombulisha utajiri tulio nao badala ya afya zetu. Vitu hivyo tunavipa thamani kubwa kuliko vinavyoongeza afya au uchumi.

Kwa mfano kilo ya nyama ni ghali kuliko ya mboga za majani. Glass ya mvinyo ni ghali kuliko ya maji. Lakini athari ya nyama au mvinyo kwa afya ya binadamu ni kubwa maradufu.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
Haki elimu.....
 
Mkuu mvinyo kuwa ghali kuliko maji ni kwasababu processes zinazotumika had kupata mvinyo ni nyng na za gharama ukilinganisha na maji ambayo tunapata naturally kutoka ktk Chemchem , mito,bahar na maziwa..... Inachukua muda mrefu zaid na gharama nyng kumtunza na kumhudumia ng'ombe had afikie ubora wa kuchinjwa na kutumika kama kitoweo tofaut na mchicha ambao haumalizi hata mwez mmoja ili uitwe mboga.... Hvyo uthamani wa kitu unasababishwa na gharama znazotumika kukipata kitu chenyewe pasipo kuangalia madhara ya kitu chenyewe ktk matumizi ya mwanadam Ndio maana hata bom la nyuklia linauzwa ghali ingawaje madhara yake ni kuangamiza na kuharib uhai pamoja na mali
 
Hata materials zinazotumika kutengeneza noti ya 1000 na ile ya 10,000 ni yaleyale. Kinachotofautisha u thamani wa hizi noti ni yale masifuri yanayowekwa. Yenye masifuri mengi Ndo yenye thamani zaidi, kwa mujibu wa ubinadamu.
Umefikiria mbali mkuu
 
Sababu kuu Gold kuwa ghali ni moja tu tena rahisi.

Demand and Supply.

Watu wanaotaka gold ni wengi (demand) lakini upatikanaji wake (supply) ni ndogo sasa hapa kinachotokea ni kuuzwa kwa bei ghali.

Kama watu leo wataacha kuhitaji gold kwa sababu yoyote ile basi thamani yake itashuka tu.

Pia kama leo gold itakuwa inapatikana kwa wingi na urahisi kama aluminium basi thamani yake itaashuka.

Ukitaka uelewe kwanini vitu vinakuwa na thamani wewe elewe tu nadharia ya DEMAND AND SUPPLY
 
Hata fedha haina thamani kama binadamu anavyoitukuza.
Fikiria karatasi au cheti chako cha shule kina tofauti gani na box LA kuwekea Sabuni?
Hii in dhahania tu. Usiwaze sana.
Wewe embu kaa bila pesa na huna hata pa kupata mlo mmoja kwa cku uone kama utakua na thamani pesa na uhai ni vitu vinavyotegemeana sana!.. Na ukitaka kujua thamani ya vyeti muulize bashite
 
Nmekuwa nikijiuliza hili swali muda mrefu. Ukiacha kuwa dhahabu inatumika kutengenezea mapambo au kuonesha utajiri nini kingine kinachoipa dhahabu uthaman?

Wazo nililo nalo ni kuwa uthaman wa dhahab kwa kiasi kikubwa umesababishwa na binadamu wenyewe na si matumizi yake. Mfano dhahabu ingekuwa ni dawa ya kutibu cancer hapo tungesema inaokoa uhai wa mtu. Dhahabu ingekuwa inatumika kuungia mifupa hapo pia tungesema hilo ni jambo la kipekee la dhahabu.

Lakini kama ni mapambo, kama ni kuonesha tu utajiri wa mtu basi ni waz thaman hii ilipachikwa na binadamu. Kama ambavyo tuchukulie glass ingekuwa ni madini yanayochimbwa ardhin na yanapatikana kwa nadra basi glass ingekuwa na thaman sana.

Kama ingekuwa kioo ni aina flan ya madin ukichimba sehem unayapata yakiwa katika hali hiyo ya ukioo basi ingekuwa ni issue kubwa sana na wenye vioo wangekuwa wanaonekana wana utajiri sana.

Naombeni mnisaidie mbali na kutumika kama mapambo dhahabu inatumikaje zaidi. Na je kuna uhusiano gani wa dhahabu na ulimwengu wa roho? Almas wanasema ni moja ya madini yenye thaman kubwa lakini naona kama dhahab inaongoza hata tukizungumzia ulimwengu mzuri tunaoujenga kichwan tutasema kuna majumba ya dhahabu au vyombo vya dhahabu. Na hapo ukiniuliza tofaut ya anayekunywa juice kwenye kikombe cha udongo na anayekunywa kwenye kikombe cha dhahabu ni nini.
Kwa kifupi sana.
Moja ya kazi ya Dhahabu ni msingi wa hazina.
Kwa mfano leo Tanzania ikitaka kuchapisha noti zake na sarafu ...malipo yake ni kilo kadhaa za dhahabu.
 
Bado utagundua dhahab kama dhahab haina thaman kama haijapewa uthaman na binadamu. Maji yana thaman kubwa sana kuliko dhahabu. Sema kwa vile maji ni mengi basi yamepoteza uthaman. Lakini ikiwa umetupwa katikat ya pori kubwa upo peke yako ukaambiwa uchague kilo 20 za dhahabu na lita 20 za maji kipi kitakuwa na thaman kwako?

Uthaman wa dhahabu ni wa kupandikizwa na binadamu. Dhahab kama dhahabu haina thaman. Isipokuwa binadamu waliamua kuipatia thaman hiyo.
 
Jet engines,rocket engines waya zake zote zinatengenezwa na dhahabu,ndomana miradi ya kurusha vyombo angani ni garama sana...nchi kama tanzania hatuwezi kupeleka satelite angani mpaka labda miaka 1000 ijayo
 
Back
Top Bottom