Ukiacha kazi, ukistaafu au kufukuzwa, kwanini unapoteza marafiki?

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,804
8,797
Waungwana wazima?

Nimejaribu kuwaza na kuona jinsi gani jamii yetu kubwa ilivyokuwa na unafiki wa hali ya juu. Kuna maisha ya hapa duniani hasa ukiwa na kipato kitokanacho na ajira ya ofisi za Umma pindi unapostafu ama kuachishwa kazi au kuamua mwenyewe kujiajiri kunatokea kutengwa na jamii uliyoishi nayo muda mwingi sehemu moja ambapo utaona hakuna ukaribu tena na hata ukisema utafute kuongea nao na kubadilishana mawazo wanakukimbia.

Hii tabia inasababishwa na nini hasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa hawakimbii ila wewe mwenyewe ulieacha kazi ukiwa unajishitukia shitukia maana mara nyingi mtu kipato kikipungua kama hajiamini ubongo wake unatafsiri kinyume na hali halisi, ukikuta watu wanacheka unahisi wanakucheka wewe au bahati mbaya mtu mnajibishana nae ulimi ukamteleza akatoa kauli ambayo sio nzuri (mtu atahusisha kwa kuwa tu hana ajira ndio anapewa kejeli)

Acha kazi alafu jichanganye na watu alafu usilielie kwa mtu kila mtu ajue huna kazi yaani namaanisha yaani hata kama unamwambia mtu huna kazi ila unaitoa kauli ya kawaida (sio ya kinyonge), hakuna mtu ataekukimbia sana sana watakuwa wanakushangaa jinsi unavyo survive wakati ugumu wa maisha unaujua mwenyewe
 
Mara nyingi ni suala ambalo lipo automatic. Kutokana na kubadili "industry" basi amini kuwa wale ulikowa nao zamani (kwenye industry nyingine) wengi utawapoteza.

Mfano mimi niliwahi kuwa fundi katika kampuni fulani na wakandarasi wengi walikuwa mabest zangu simu kila mara kwakuwa nilikuwa nawasaidia kazi zao lakini nilipoacha mawasiliano yakakata. Hii ni kutokana na sababu kuwa kwao sikuwa ni connection tena na hivyo imewabidi watafute connection mpya ili mambo yao yaende sawa. Wala mimi sijachukizwa kwasababu naelewa uhalisia wa mambo. Hata hivyo nilipo sasa na mimi nina connection mpya ambazo sikuwa nazo zamani.

Mbaya ni pale rafiki zako wa karibu zaidi pamoja na ndugu na jamaa wanapokutenga ukiwa huna kitu wakati ulipokuwa na kitu walikuwa karibu sana na wewe.

Hili ni funzo kuwa kumbe sio kila mtu unaemuona yupo karibu yako ni kwasababu anakupenda. Wengi wapo kimaslahi. Hivyo wakati umedondoka ndio muda muafaka kwako kupitisha chujio lako ili kubaini rafiki wa kweli kwako ni yupi ili utakapoinuka tena wale waliokuwa nawe kwenye shida ndio wabaki kwenye marafiki zako. Watakaotaka kujikomba na kujirudisha wachijilie baharini.

Undugu na urafiki wa kweli hudhihirika wakati wa shida.
 
Jifunze kujua wakati wa kuachana na wengine unapofika,sio kila mtu utadumu naye kwa Muda wote:
1)Kuna watu wataanza na wewe wanakusaidia kufika mahali fulani Kisha wanaondoka kwa ajili ya kwenda kuwasaidia wengine.Wape Fursa ya kuwasaidia wengine pia,usiwe mbinafsi kuwang’ang’ania.
.
2)Kuna watu walikuja ili uwasaidie,wakishaimarika wanaendelea na Safari,na wewe endelea na Safari.Usinung’unike kuwa hawako na wewe tena,Furahia mafanikio yao.Mungu alikutumia kuwasogeza hatua,usitake kuwamiliki.
.
3)Kuna watu walikuja kukufundisha Kitu fulani,ukishapata somo,wanaondoka.Inaweza kuwa kupitia maumivu ama furaha,ila somo utalipata.Wanakusaidia kukuongezea umakini katika maisha.
.
4)Kuna wengine walikuja ili wakuunganishe na watu wengine,wakishamaliza wanaondoka.Wanaweza wasikupe Kitu ila wakakuunganisha na Mtu/Fursa itakayokufanikisha.
.
5)Kuna wengine walikuja kukuharibia mwelekeo,wakishakutoa kwenye mstari,wanaondoka.Furaha yao na ushindi wao ni kuona umepoteza mwelekeo.
.
6)Kuna watu wamekuja kwa sababu kuna msimu mpya wa maisha yako,msimu huo ukishapita na wao wanakuwa wamemaliza kazi.Ni marafiki wa msimu.
.
7)Kuna watu walikuja kwa sababu kuna Kitu walitarajia kupata kutoka kwako,wakishakipata tu,wanaondoka.Hawana cha kukupa hawa,usijaribu kutarajia kutoka kwao.

*TIMIZA MALENGO YAKO*
*TENDA WEMA NENDA ZAKO*
c-m

Hii ni c&p

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii Mada Ni nzuri sana, fikirishi inayohitaji sana tafakuri na ina funzo kubwa sana.Katika maisha Watu wengi wanakuangalia una nini na kina hadhi gani??

Kama uko Serikalini Heshima yako hupimwa kwa nguvu na madaraka na ofisi unayofanyia kazi..mara nyingi watu husahau kwamba mambo hayo yote hupita na hilo ndilo huwaumiza wakistaafu au kufukuzwa.Kumbuka fukuza fukuza haukuapo sana nyuma huko awamu 4 zote haikua kubwa kama leo awamu hii.

Awamu hii kwa maoni yangu chuki tu na mtu mwingine ofisni inaweza kukuweka matatizoni ukaumia hivyo chances za kuonewa pia zipo sana kwasasa.Hii pekee ni mada ya kujitegemea.

Cha msingi jenga imani moyoni kazi ya Umma sio yako ndio mana inaitwa public service ujenge moyo uwe na amani ili ukiondoka usikonde na kuumia.

Unapokua kazini network unazopata tumia kufungua milango ya kujiajiri mbeleni.Sio ukae tu kufurahia simu kuita kila mara ukitolewa uanze kukonda na mawazo.

Kazi ya Umma sio yako usiwatendee Wengine roho mbaya malipo ni hapa hapa.Mifano ni Mingi.
 
Rufiji dam, Hapa kwetu hamnaga marafiki wa dhati wengi wako kimasirahi wakiona hamna kitu tena hawana mda nawewe ...Mimi nilishawahi kukaa na DC (mkuu wa wilaya) msitaafu nilishinda nae wiki nzima tukiwa kwenye shughuri fulani simu yake hamna alio ipinga wiki nzima isipo kua mara moja tu wakati mkewe anamuulizia anageuza lini?

......marafiki wa kiswahili 90% ni wanafiki sana ukipata shida kubwa wanafurahi ki mwoyomwoyo na watasambaza habari kwa wengine, rafiki yako ni mtoto wako wazazi wako ndugu zako kwa 40% mkeo kwa 50% , mimi sinaga mkumbo wa marafiki wala sitaki kabisa nahitaji business partner tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jifunze kujua wakati wa kuachana na wengine unapofika,sio kila mtu utadumu naye kwa Muda wote:
1)Kuna watu wataanza na wewe wanakusaidia kufika mahali fulani Kisha wanaondoka kwa ajili ya kwenda kuwasaidia wengine.Wape Fursa ya kuwasaidia wengine pia,usiwe mbinafsi kuwang’ang’ania.
.
2)Kuna watu walikuja ili uwasaidie,wakishaimarika wanaendelea na Safari,na wewe endelea na Safari.Usinung’unike kuwa hawako na wewe tena,Furahia mafanikio yao.Mungu alikutumia kuwasogeza hatua,usitake kuwamiliki.
.
3)Kuna watu walikuja kukufundisha Kitu fulani,ukishapata somo,wanaondoka.Inaweza kuwa kupitia maumivu ama furaha,ila somo utalipata.Wanakusaidia kukuongezea umakini katika maisha.
.
4)Kuna wengine walikuja ili wakuunganishe na watu wengine,wakishamaliza wanaondoka.Wanaweza wasikupe Kitu ila wakakuunganisha na Mtu/Fursa itakayokufanikisha.
.
5)Kuna wengine walikuja kukuharibia mwelekeo,wakishakutoa kwenye mstari,wanaondoka.Furaha yao na ushindi wao ni kuona umepoteza mwelekeo.
.
6)Kuna watu wamekuja kwa sababu kuna msimu mpya wa maisha yako,msimu huo ukishapita na wao wanakuwa wamemaliza kazi.Ni marafiki wa msimu.
.
7)Kuna watu walikuja kwa sababu kuna Kitu walitarajia kupata kutoka kwako,wakishakipata tu,wanaondoka.Hawana cha kukupa hawa,usijaribu kutarajia kutoka kwao.

*TIMIZA MALENGO YAKO*
*TENDA WEMA NENDA ZAKO*
c-m

Hii ni c&p

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu umewaza kwa kutuliza akili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waungwana wazima?

Nimejaribu kuwaza na kuona jinsi gani jamii yetu kubwa ilivyokuwa na unafiki wa hali ya juu. Kuna maisha ya hapa duniani hasa ukiwa na kipato kitokanacho na ajira ya ofisi za Umma pindi unapostafu ama kuachishwa kazi au kuamua mwenyewe kujiajiri kunatokea kutengwa na jamii uliyoishi nayo muda mwingi sehemu moja ambapo utaona hakuna ukaribu tena na hata ukisema utafute kuongea nao na kubadilishana mawazo wanakukimbia.

Hii tabia inasababishwa na nini hasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni nature ili urafiki uwepo ni lzm kuwe na kitu kinachowaunganisha, ukiwa mkulima utakutana na marafiki wakulima,hivo hivo wafanyakazi,wafanyabiashara,wanafunzi marafiki uendana na mazingira pia
 
Mkuu pole na hongera kwa kuleta mada hii hapa jukwaani. ukweli ni kwamba kila jaribu ni mpango wa Mungu kukufundisha namna ya kubadili maisha yako au jinsi ya kuishi na watu waliokuzunguka. mimi binafsi nilishakumbwa na tatizo hilo niliachishwa kazi kwenye taasisi ya umma nikakimbiwa na marafiki zangu wote ambao nilikuwa nakula nao nakunywa nao.

lakini baada ya kuachishwa kazi nilikuwa kila nikimpigia rafiki yangu yeyote yule wananikatia simu na nikienda kwenye eneo la kazini hawataki hata kuniona ili mkuu wao asiwaondoe na wao. baada ya kufukuzwa nilifungua kesi na nikapambana kurudi kazini.

Mungu alivyo mwema baada ya miaka 7 mahakama kuu ikatoa hukumu kwamba sina hatia hivyo nirudi kazini na nilipwe mishahara yangu yote. kwa kweli nimerudi kazini kwa amri ya mahakama na nimelipwa mabilioni hivi ninavyoongea nina magari mawili moja la biashara na moja la familia na nimejenga nyumba kubwa nzuri ya gorofa 2 huwezi amini maadui wameaibika hawana raha kabisa na maisha yangu.

Leo hii mimi ni tajiri kuliko wao nilichokifanya ni kwenda kanisani kutoa shukrani ya siri kumuambia Mungu wangu asante unafanya mambo ambayo mwanadamu hawezi kufanya. leo nipo kazini na mshahara umepanda Mungu ni mwema kwangu sana. Hivyo nimegundua kwamba Mungua alinipa hilo jaribu ili anionyeshe marafiki zangu wa kweli ni wapi kumbe nilizungukwa sana na maadui sasa nimejua namna ya kuishi na watu.

Endeleeni kumuomba mungu na ukipata lolote baya shukuru sio kila jaribu ni mkosi majaribu mengine ni ya kukupeleka kwenye daraja la mafanikio.siku njema
 
tapatalk_1583756529009.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waungwana wazima?

Nimejaribu kuwaza na kuona jinsi gani jamii yetu kubwa ilivyokuwa na unafiki wa hali ya juu. Kuna maisha ya hapa duniani hasa ukiwa na kipato kitokanacho na ajira ya ofisi za Umma pindi unapostafu ama kuachishwa kazi au kuamua mwenyewe kujiajiri kunatokea kutengwa na jamii uliyoishi nayo muda mwingi sehemu moja ambapo utaona hakuna ukaribu tena na hata ukisema utafute kuongea nao na kubadilishana mawazo wanakukimbia.

Hii tabia inasababishwa na nini hasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukipoteza jua hao hawakua marafiki zako bali ni contacts tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom