Maserati
JF-Expert Member
- Jun 15, 2014
- 11,602
- 20,098
Ubaya wa roho yake ni nini??
Sasa anavotaka mwenzie aende huko akakatwe
Ubaya wa roho yake ni nini??
Habari wana MMU
Tuna binti wetu wa kazi ambae sasa ni kama miezi 6 tangia tumeanza kuishi nae.Ni mwenyeji wa mkoa wa Dodoma.
Huyu binti historia yake hakuwahi kupelekwa shule na kwa maana hiyo hawezi kusoma wala kuandika.Alifanyiwa mpango hapa nyumbani akapelekwa sehemu ili ajifunze kusoma na kuandika then utaratibu mwingine ufuate.
Amekuwa ni rafiki kwangu ingawa me nimempita kiumri ila ananiambia vitu vingi sana.Na huwa na mshauri pale inapobidi...
Juzi mama yake alipiga cm kwa wazazi wangu wakiomba tumrudishe binti yao.Home walikubali na baadae wakampigia tena aongee na binti yao....
Waliongea nae kwa kilugha na hatukujua walichoongea
Sasa leo huyu binti amenifuata chumbani na kuniambia kuwa mama yake atakuwa anamuitia kumkeketa tu maana kabla yakuja huku dar alimwambia akamsalimie bibi yake kijijini (mvumi) akahisi zoez hilo lingekamilishwa lakin hakwenda.
Namuonea huruma sana na nimemwambia kuwa akirudi nyumbani asikubali lakin sasa kaniambia haiwezekani kwani huwa wanawakamatia ndani.
Roho inauma sijajua jinsi yakumsaidia jamani.....nisaidieni ushauri!!!
Yeah kes coz watamfanyia ktu ambacho hayupo willing nacho.ts violation of human rights
Mkuu, mahsuri asiende---ukeketaji ni mbaya sana kwa watoto wa kike. Lakini sijakupata vizuri hapo kwenye red mkuu.
Ha ha ha ha ha h haa.eti jukwaaa.jukwa la nn??
Huyu kaanza kuelimika baada yakuona baadhi ya vipind kwenye tv vinavyopinga ukeketaji na kusema madhara yake.
Kuhusu kukaririshwa ni kweli coz kasema wanaotoka kukeketwa ukiwauliza habari za huko wanasema yaani huko ni raha sana.
Duuuhh huyu mama yake anatafuta matatizo maana hata shule mtoto hakumpeleka na bado analeta balaa lingine.
interesting....Dodoma kabila gani?
Muache mwenzio akakate antenna,atatumia dish
Umejarbu kuwashrksha wazaz wako kwa hl???
Huwa napenda kujieleza kwa vitendo, hao watasema na ng'ombe 40! Nadhani hiyo itakuwa zaidi a maelezo. Mkono mtupu haulambwi mama.
Tutaangalia kama una qualify.....
Hilo tu, ondoa shaka, wasiwasi wangu nisije ku-overqualify.
mwambie tuhuyo binti asijaribu kwenda serikali imepiga marufuku.....atakamatwa atafungwa