miss strong
JF-Expert Member
- Jul 4, 2012
- 7,012
- 3,694
Habari wana MMU
Tuna binti wetu wa kazi ambae sasa ni kama miezi 6 tangia tumeanza kuishi nae.Ni mwenyeji wa mkoa wa Dodoma.
Huyu binti historia yake hakuwahi kupelekwa shule na kwa maana hiyo hawezi kusoma wala kuandika.Alifanyiwa mpango hapa nyumbani akapelekwa sehemu ili ajifunze kusoma na kuandika then utaratibu mwingine ufuate.
Amekuwa ni rafiki kwangu ingawa me nimempita kiumri ila ananiambia vitu vingi sana.Na huwa na mshauri pale inapobidi...
Juzi mama yake alipiga cm kwa wazazi wangu wakiomba tumrudishe binti yao.Home walikubali na baadae wakampigia tena aongee na binti yao....
Waliongea nae kwa kilugha na hatukujua walichoongea
Sasa leo huyu binti amenifuata chumbani na kuniambia kuwa mama yake atakuwa anamuitia kumkeketa tu maana kabla yakuja huku dar alimwambia akamsalimie bibi yake kijijini (mvumi) akahisi zoez hilo lingekamilishwa lakin hakwenda.
Namuonea huruma sana na nimemwambia kuwa akirudi nyumbani asikubali lakin sasa kaniambia haiwezekani kwani huwa wanawakamatia ndani.
Roho inauma sijajua jinsi yakumsaidia jamani.....nisaidieni ushauri!!!