UKAWA yasambaratika Arusha, CCM washangilia

UKAWA yasambaratika Arusha, CCM washangilia

Ule usemi kuwa UKAWA ni wasaka tonge unaanza kukamilika taratibu.

UKAWA wangekuwa wasaka tonge mnaposikia porojo za kusambaratika msingekuwa mnashangilia,kushangilia kwenu ni jibu tosha kuwa UKAWA imewakalia kooni.
 
Mbona ma-ccm mnajitetemesha na hoja za ajabu ajabu! Nani kasema Cuf wamemwachia Chadema jimbo huko Unguja!?! Jimbo linalozungumziwa hapa Cuf hajawahi kushinda tangu kuanzishwa kwake!

Hata katika uchaguzi mkuu uliopita Chadema walishika nafasi ya pili! katika hali hiyo inawezekanaje cuf awe amemwachia mwenzie jimbo?

Tatizo lililopo kwenye Ukawa kwa sasa ni kwamba baadhi ya vyama havifanyi jitihada kuyapata majimbo ambayo yamekuwa ngome ya ccm kwa muda mrefu, wameng'ang'ana na majimbo ambayo tayari yapo kwa upinzani (ukawa).
 
Ule usemi wa adui muombee njaa, umetimilika Arusha baada ya CCM kushangilia kuvunjika kwa UKAWA.

Arusha mumetupa aibu wapenda demokrasia.

Imekuwaje G.Lema na Nassari washindwe kuafikiana na wenzao? hii inanifanya niamini maneno ya mbatia kwamba ndani ya UKAWA kuna umimi.

Inasikitisha sana mnavo jitetea kwamba hata Serikali za mitaa kila chama kilisimamisha mgombea wake. Mimi nliamini baada ya Uchaguzi Serikali za Mitaa, ilikua ni wakati wa kufanyia kazi tofauti zenu.

Aibu zaidi ni pale Moja ya chama kinachounda UKAWA, kuandika barua eti hawatambui UKAWA Arusha. Hii ni aibu.
Kwanini watu wa Arusha Mnang'ang'ania Madaraka?

Mkajifunze Zanzibar ambapo CUF wamewachia CHADEMA Jimbo moja kwa ajili ya Salum Mwalimu. CUF hawajasimamisha mtu jimbo hilo la Mwalimu.

Arusha aibu yenu!

Wewe kwa akili yako hapa ndio umeandika kitu cha watu wachangie kweli?
 
Haahaaaa adui muombee njaa, lakini isijekuwa unamuombea njaa kipindi ambacho ni cha ukame itakuwa haina maana, UKAWA imewafanya watu wachanganyikiwe huu ni muungano tu fitina kila kona poleni, subirini matokeo ya uchaguzi UKAWA itawafanya watu wasielewane lugha nsani ya CCM.

Ukawa itaifanya ccm ifutike ktk ulimwengu wa siasa kabisa.
 
Hakuna ukweli wowote wa suala hilo..huu ni uzushi kama mwingine wowote.

Ni wazi kuwa mleta uzi anawasilisha hisia na ndoto za wana-CCM wengi juu ya UKAWA.

Kweli kwa mwana ccm,anaichukulia ukawa kama adui yake namba moja hivyo atazusha kila baya juu ya ukawa.
 
Rudi ukalale wewe, inaelekea ndoto yako haijafikia mwosho ukakurupuka.

Teeeeh,teeeeh,teeeeh,alikuwa anatoa juu ya ukawa.wataugua maradhi mengi mwaka huu juu ya ukawa.
 
Wacha waje wenye UKAWA wakusasambue, UKAWA itasambaratika kirais hivyo, CCM ndiyo imesambaratika Arusha na aliye isambaratisha ni Merry Chatanda

Huyo alikuwa ndotoni
 
UKAWA wangekuwa wasaka tonge mnaposikia porojo za kusambaratika msingekuwa mnashangilia,kushangilia kwenu ni jibu tosha kuwa UKAWA imewakalia kooni.

Sana kiongozi,ccm sasa hivi wameingiwa na hofu kubwa kiasi wanataka kumuuwa sisimizi kwa bunduki
 
Kwa ambao hawako Arusha mnaweza mkaongopewa na huyu, ila Arusha haturudi nyuma, tushafanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi. Period.

Hongereni sana wana wa Arusha kwa kujitambua na kuwafuta hawa wanyonyaji.
 
Figganigga kwanza kaulize ile Tume ya Mkude Simba,maana mpaka imebidi watoe onyo kwa UKAWA.

Pili sioni sababu ya vyama vingine kukimbilia kwenye maeneo ambayo ina wabunge tayari wa upinzani?Kwanini wasiende kwenye majimbo ya CCM wakafanya kampeni?

Ninawasiwasi na waliyekupa taarifa yawezekana aliwekwa ili kuleta tafrani huko.Mpe pole mwambie ameshindwa arudishe fedha za MAFISADI walizompa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom