UKAWA yasambaratika Arusha, CCM washangilia

UKAWA yasambaratika Arusha, CCM washangilia

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,812
Reaction score
63,268
Ule usemi wa adui muombee njaa, umetimilika Arusha baada ya CCM kushangilia kuvunjika kwa UKAWA.

Arusha mumetupa aibu wapenda demokrasia.

Imekuwaje G.Lema na Nassari washindwe kuafikiana na wenzao? hii inanifanya niamini maneno ya mbatia kwamba ndani ya UKAWA kuna umimi.

Inasikitisha sana mnavo jitetea kwamba hata Serikali za mitaa kila chama kilisimamisha mgombea wake. Mimi nliamini baada ya Uchaguzi Serikali za Mitaa, ilikua ni wakati wa kufanyia kazi tofauti zenu.

Aibu zaidi ni pale Moja ya chama kinachounda UKAWA, kuandika barua eti hawatambui UKAWA Arusha. Hii ni aibu.
Kwanini watu wa Arusha Mnang'ang'ania Madaraka?

Mkajifunze Zanzibar ambapo CUF wamewachia CHADEMA Jimbo moja kwa ajili ya Salum Mwalimu. CUF hawajasimamisha mtu jimbo hilo la Mwalimu.

Arusha aibu yenu!
 
Atakayevuruga muungano huu wa kuiondoa CCM atalaaniwa na vizazi vyote Tanzania.
 
cuf zanzibar wameachia jimbo moja tena ngome ya ccm, bado tunaita ukawa?
 
Wacha waje wenye UKAWA. UKAWA itasambaratika kirais hivyo, CCM ndiyo imesambaratika Arusha na aliyeisambaratisha ni Merry Chatanda
 
Kama ni kweli imetokea, litakuwa ni pigo kwa wapenda mabadiliko.
Chief figganigga hebu tupe chanzo cha hizi taarifa?

mia.
 
Last edited by a moderator:
figganigga unagombea nini mkuu? Wamegoma kukuachia? Kwani Cuf kuachia jimbo moja kati ya mamia zenji nayo ni sifa? Tena ngome ya magamba
 
Last edited by a moderator:
Rudi ukalale wewe, inaelekea ndoto yako haijafikia mwosho ukakurupuka.
 
Hakuna ukweli wowote wa suala hilo..huu ni uzushi kama mwingine wowote.

Ni wazi kuwa mleta uzi anawasilisha hisia na ndoto za wana-CCM wengi juu ya UKAWA.
 
Ule usemi kuwa UKAWA ni wasaka tonge unaanza kukamilika taratibu.
 
Haahaaaa adui muombee njaa, lakini isijekuwa unamuombea njaa kipindi ambacho ni cha ukame itakuwa haina maana, UKAWA imewafanya watu wachanganyikiwe huu ni muungano tu fitina kila kona poleni, subirini matokeo ya uchaguzi UKAWA itawafanya watu wasielewane lugha nsani ya CCM.
 
Ukawa wako imara sana tusidanganyane hapa, ccm msipo tulia kwenye behewa lenu la kwenda ikulu mkampitisha kibaka nchi inakwenda ukawa october saa 4 asubuhi
 
Hivi magamba mmekuwaje? Kama wagaganga wa kienyeji. Mwaka huu lazima choo laini iwatoke
 
Hivi ccm wanadhani kuwa ngome ya upinzani Arusha wataweza hata kusogeza pua wajaribu mwaka huu waone kikumbo?
 
Kwa ambao hawako Arusha mnaweza mkaongopewa na huyu, ila Arusha haturudi nyuma, tushafanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi. Period.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom