MWAKATA KWETU
JF-Expert Member
- Mar 25, 2015
- 560
- 320
Vyama vinavyounda ukawa leo vimefanya mkutano wao wa kwanza mjini kahama na kuhudhuriwa na halaiki kubwa ya watu ambao wakati wote walionekana wakiwa na nyuso za ukombozi....mweshimiwa lema amewaasa wananchi kuwaunga mkono ukawa pamoja na kuepuka vibaraka wa ccm wanaotaka kuwagawa watanzania ili ccm iendelee kutawala.amesema,"ccm wanatumia fedha nyingi sana kuanzisha vyama vipya vya siasa lengo na madhumuni kuwagawa watanzania ili waweze kuendelea kutawala"pia mheshimiwa kafulila amesema kuwa watanzania tuiunge mkono ukawa kwani ukawa ndio tumaini la watanzania kwa sasa....amesema,"ataendelea kuwaelimisha watanzania kwa gharama yoyote na bunge lijalo anaenda kumbana waziri mkuu aweke hadharani ripoti ya takukuru kuhusu escrow.pia mheshimiwa kafulila amesimikwa kuwa mtemi wa kahama na kupewa jina kishimba ishara ya kumkumbuka mpiganaji wa utemi wa kahama mtemi kishimba.