David Kafulila ni hazina kwa Taifa letu, anapaswa kutumiwa vyema kwa maslahi mapana ya nchi

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
19,241
13,548
Ndugu zangu Watanzania,

Nimeendelea kumfuatilia na kufuatilia mahojiano mbalimbali ambayo amekuwa akifanya na ambayo amefanya kupitia vyombo vya habari kuelezea mambo mbalimbali kuanzia uchumi, uwekezaji, biashara na mengine mengi. Kila mtu pasipo kujali itikadi yake ya Kiasia au chama chake anakili kuwa Mheshimiwa David Kafulila Ni Hazina kubwa kwa Taifa letu na anapaswa kutumiwa vyema kwa maslahi mapana kwa Taifa letu.

Nimeona namna anavyoitetea na kuisemea vyema serikali yetu chini ya Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan kwa ufasaha, hoja, takwimu na ushahidi wa kiutafiti na wa ukweli. Anaeleza kwa lugha nyepesi ambayo watu wanamuelewa vyema sana huku mitaani na kuielewa vyema sana serikali yetu kupitia ufafanuzi wake anao utoa.

Anaeleza kwa utulivu,upole na unyenyekevu mkubwa sana. Angalia namna alivyoelezea juu ya Deni la Taifa,ongezeko la watalii hapa nchini ,suala la ajira na ukuaji wa uchumi wetu. Akaeleza kuwa pamoja na kwamba watu wanasema Deni limekuwa lakini uchumi wetu umekuwa zaidi ndani ya Muda mfupi wa Rais Samia kutoka Dolla Billioni 66 mpaka Dolla Billion 85. Akaeleza pia kuwa kukopa siyo dhambi bali inategemea unakopa kwa ajili ya nini.akasema kama unakopa kwa ajili ya kulipa mishahara hapo ndio inakuwa tatizo.

Mheshimiwa Kafulila amekuwa mtetezi mkubwa sana wa Rais Samia na serikali yake kupitia vyombo vya habari na mitandao. Anaifanya kazi hiyo kwa weledi na uzalendo mkubwa sana, anawafumbua macho watu wengi sana ambao wengi walikuwa wamepofushwa akili na macho na upotoshaji wa baadhi ya watu wenye nia mbaya na chuki binafsi na Mheshimiwa Rais na Serikali yake.

Mheshimiwa David Kafulila amefanikiwa kwa hoja nzito na kwa lugha rahisi na kwa takwimu kuzizima na kuzisambaratisha kabisa kama mvuke hoja za upinzani walizokuwa wanazitumia kupotosha wananchi hususan wale wasio na uelewa wa baadhi ya mambo hususani ya kiuchumi.

Mheshimiwa David Kafulila mbali na usomi wake mkubwa lakini unamuona ni mtu mnyenyekevu na mzalendo wa kweli kwa Taifa letu. Ni mtu na kiongozi aliye nyooka kama rula. Hanaga kupinda pinda. Ni mtu ambaye kwake nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi. Hata umshambulie kwa lugha kali utaona yeye amebakia katika utulivu na kujibu kwa hoja. Katika hili mnaweza kurejea mapambano ya hoja bungeni wakati wa sakata la Escrow namna alivyokuwa mtulivu katika kutoa hoja na kutetea hoja zake.

Mheshimiwa David Kafulila Ni chuma na kiongoz anayekubalika kwa hoja zake na watu wa vyama vyote iwe upinzani na ndani ya chama chetu cha CCM.kwa sababu yeye wakati wote husimama katika hoja na kuitetea hoja kwa takwimu.

Mheshimiwa Rais Aendelee kumtumia Mheshimiwa Kafulila kwa sababu ana mapenzi mema na Taifa letu na ni mzalendo na amekuwa mtetezi wake kwa yote ayafanyayo. wakati unakuta wengine wamejikausha tu pale serikali inaposhambuliwa kwa hoja za upotoshaji.

Mheshimiwa Kafulila amekataa kabisa kivitendo kukaa kimya pale anapoona kuna watu wanapotosha mambo kwa lengo la kuichongaisha serikali na wananchi au kuifanya serikali ichukiwe na wananchi.amekuwa akitoka hadharani na kujibu mapigo kwa hoja na takwimu na kusambaratisha kabisa mijadala ya kiuopotoshaji.

Mheshimiwa David Kafulila Ni Hazina kwa Taifa letu tunayepaswa kumtumia kwa maslahi mapana ya Taifa letu. Ni mtu safi, mzalendo na mchapa kazi kwelikweli. Ndio maana huwezi ukamkuta na doa la rushwa au ufisadi au matumizi mabaya ya madaraka katika maeneo mbalimbali aliyoitumikia Taifa letu. Zaidi utakuta alama njema za kiutendaji alizoziacha katika maeneo aliyopita na kukumbukwa kwa uchapakazi wake ulioleta matokeo chanya.

Watanzania tunapaswa kuwatia moyo na kuwaunga mkono wazalendo aina ya Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan na David Kafulila. Tukikaa kimya tukaacha wakashambuliwa na wenye maslahi yao binafsi tutakuwa tunawakatisha tamaa na kuwapa ushindi mafisadi na wenye kulinyonya Taifa letu kwa mirija.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Anapambana sana
Anapambana sana na anatakiwa kupewa nguvu ,kutiwa moyo na kuungwa mkono. Ikumbukwe siyo wote wanaofurahia kazi nzuri na ya kizalendo anayoifanya kuisemea serikali ya Rais Samia. Wengine wanapenda sana kuona serikali yetu na Rais wetu wakishambuliwa kwa nguvu bila kupata watetezi. Kwa hiyo wanapojitokeza watetezi aina ya David Kafulila wanakuwa wanaonekana kama maadui na wakwamishaji wa ajenda mbaya za siri Kwa Rais Samia na Serikali yake.
 
Shida system haitaki akili za Kafulila, inahitaji akili za Babu Tale. No Offence.
Rais wetu ni mzalendo na anayependa na kuwapenda sana wachapa kazi na WAZALENDO aina ya Mheshimiwa David Kafulila.kwa hiyo naamini hata Mheshimiwa Rais anaona kazi nzuri anayoendelea kuifanya Mheshimiwa Mheshimiwa Kafulila na atajuwa amuweke wapi ili atumike vyema zaidi kwa maslahi ya Taifa letu.

Lakini naona itapendeza sana ikiwa mwakani akiungwa mkono ili aingie Bungeni na kupewa nafasi yakuwa ndani ya Baraza la Mawaziri. Naamini atapiga kazi mpaka Dunia itashangaa. Na wala Mheshimiwa Rais hatajuta kumpa nafasi ya kutumika katika baraza lake la Mawaziri.
 
Cha kufanya kwa sasa ni kutafuta jukwaa la kafulila.Tumeshindwa kulinda mali zetu zinaibiwa na mabeberu tuje kulinda mtu ana nn cha ajabu huyo nchi hii inahitaji kufumuliwa yote tuanza upya
 
Cha kufanya kwa sasa ni kutafuta jukwaa la kafulila.Tumeshindwa kulinda mali zetu zinaibiwa na mabeberu tuje kulinda mtu ana nn cha ajabu huyo nchi hii inahitaji kufumuliwa yote tuanza upya
Nchi ipo katika mikono salama ya Mzalendo wa kweli na dhati Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan. Kikubwa ni kuendelea kuwaunga mkono WAZALENDO wengine aina ya Mheshimiwa David Kafulila walioamua kujitoa na kujitolea kumsaidia kazi Mheshimiwa Rais.
 
Nchi ipo katika mikono salama ya Mzalendo wa kweli na dhati Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan. Kikubwa ni kuendelea kuwaunga mkono WAZALENDO wengine aina ya Mheshimiwa David Kafulila walioamua kujitoa na kujitolea kumsaidia kazi Mheshimiwa Rais.
Hebu niambie ww km mtanzania gas ya mtwara ina msaada gani kwako?Nimekuuliza dogo tu hilo..
 
Anapambana sana na anatakiwa kupewa nguvu ,kutiwa moyo na kuungwa mkono. Ikumbukwe siyo wote wanaofurahia kazi nzuri na ya kizalendo anayoifanya kuisemea serikali ya Rais Samia. Wengine wanapenda sana kuona serikali yetu na Rais wetu wakishambuliwa kwa nguvu bila kupata watetezi. Kwa hiyo wanapojitokeza watetezi aina ya David Kafulila wanakuwa wanaonekana kama maadui na wakwamishaji wa ajenda mbaya za siri Kwa Rais Samia na Serikali yake.
Anatafuta tu cheo kikubwa zaidi ya hicho. Akipata atatulia.
 
Anatafuta tu cheo kikubwa zaidi ya hicho. Akipata atatulia.
Mheshimiwa Kafulila hajawahi kutafuta vyeo wala kuwa na uchu wa madaraka na hajawahi kuwa na dhamira hiyo .Kiu yake kubwa ni kuona taifa letu likistawi na kusonga mbele kimaendeleo. Anastahili kupewa nafasi zaidi ya kutumika kwa Taifa letu.
 
Back
Top Bottom