UKAWA wanamvizia Lowassa atoswe CCM wamchukue

UKAWA wanamvizia Lowassa atoswe CCM wamchukue

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,618
Wenye macho ya mbali wanaamini kusua sua kwa zoezi la kumteua mgombea uraisi UKAWA ni njia ya kumngojea Lowassa achujwe CCM kisha wao wamchukue kama mgombea wao wa uraisi kwani ameshajijenga na wakimchukua Lowassa watakuwa na uhakika wa kura nyingi toka ndani ya CCM.

Posted by: MCHUNGUZI HURU (Associate Professor)
 
Last edited by a moderator:
wenye macho ya mbali wanaamini kusua sua kwa zoezi la kumteua mgombea uraisi ukawa ni njia ya kumngojea lowassa achujwe ccm kisha wao wamchukue kama mgombea wao wa uraisi kwani ameshajijenga na wakimchukua lowassa watakuwa na uhakika wa kura nyingi toka ndani ya ccm.

Posted by: Mchunguzi huru (associate professor)

mchunguzi feki
 
unachunguza nini iwapo unaandika pumba kiasi hiki??? kuvizia ni kosa au sio kosa?
 
Sifa kuu ya mwanasiasa ni tamaa ya madaraka na si juwahudumia wananchi kama wanavyodai
 
Ka akili za viongozi wa UKAWA, hili linawezekana. Hawana kabisa mgombea Urais. Wanasubiri makapi toka CCM
 
Lowassa ni history hana mvuto,hana sera,hana usafi na baya zaidi ni mgonjwa.
 
nitajie faida 2 tu ulizozipata tangu uanze kuandika uongo .
 
Lowassa ni history hana mvuto,hana sera,hana usafi na baya zaidi ni mgonjwa.
Mkuu, Pole sana.
Naomba nikujulishe tu. Lile zoezi.la uandikishwaji lilokuwa lianze kesho limeahirishwa tutajulishwa tena baadaye.
Lowassa wa kwetu tu. Hakwepeki.
 
Ukawa wameshasema hawapokei makapi huelewi tu? Hilo gunia lenu la misumari mtakoma nalo safari hii, malizaneni wenyewe tu msituhusishe sisi. Na nguli lazima atawatokeeni puani .
 
Kwanini zoezi limesitishwa au kwakuwa kuna chama kulipita mitaani kuhamasisha wanachi hasa vijana wajiandikishe.

Mkuu, Pole sana.
Naomba nikujulishe tu. Lile zoezi.la uandikishwaji lilokuwa lianze kesho limeahirishwa tutajulishwa tena baadaye.
Lowassa wa kwetu tu. Hakwepeki.
 
Ka akili za viongozi wa UKAWA, hili linawezekana. Hawana kabisa mgombea Urais. Wanasubiri makapi toka CCM
Unadai kuwa Ukawa hawana mgombea Urais?

Hata kama watakosa mgombea kihivyo, lakini haiwezekani wafikie wamchukue 'kapi' tena fisadi wa kutisha mzee wa mamvi halafu wamfanye mgombea Urais wao.

Unategemea hapo watajielezaje.kwa wananchi, wakati ajenda yao no. 1 kwa wananchi ni kupambana na ufisadi, halafu wao wambebe 'fisadi' kuwa ndiye mgombea wao!
 
Huyu lazima ni MChunguzi wa kambi ya Lowassa anapima upepo. Hatumtaki huyo jamaa
 
amiri jeshi mkuu EL.!!!!!ivi anaweza kagua gwaride kwelii
 
Back
Top Bottom