Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,976
Wakuu.
Mahakama Kuu katika kesi ya kihistoria ya Saed Kubenea v. Attorney General, Misc. Civil Cause No. 28 of 2014 ilitamka wazi kwamba Bunge Maalum la Katiba halikufungwa na RASIMU YA WARIOBA na wala hawakulazimika kufuata yaliyokuwa ndani ya RASIMU hiyo, lakini ndugu zetu wa UKAWA bado hilo hawalioni! Wamekuwa wanatoa comments (hata humu JF) as if Bunge Maalum la Katiba lilifungwa na RASIMU YA WARIOBA! Hiyo si sahihi hata kidogo.
Sisemi kwamba Bunge Maalum la Katiba halipaswi kukosolewa lakini pale ambapo chombo pekee cha utoaji haki kinapotoa tafsiri ya kisheria lazima tafsiri hiyo iheshimiwe hadi hapo chombo hicho hicho kitakapotoa tafsiri nyingineyo! Ni vizuri hata namna upigaji kura ulivyofanyika na hata kura zilivyopatikana vikahojiwe Mahakamani na Mahakama hiyo ikitoa tafsiri basi tuiheshimu, hata kama itakuwa ni kinyume na maoni yetu.
Kinyume chake ni kudharau (contempt) chombo hicho hicho ambacho wao wenyewe walikimbilia kwenda kuwasilisha malalamiko yao.
Nawasilisha kwa mjadala zaidi.