Mkuu Jabulani,Najaribu kutafuta hayo uliyosema kwamba mahakama iliyatamka:
![]()
![]()
1.Kuna mgongano mkubwa kati ya toleo la Kiswahili na Toleo la Kiingereza la kifungu cha 25 (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
2. Kwamba pamoja na mgongano huo, Sheria imekusudia kwamba Madaraka ya Bunge Maalum la Katiba yatatekelezwa kupitia Rasimu ya Tume ya M.y.K kama ilivyowasilishwa kwake.
3. Kwamba mamlaka ya BMK yana mipaka, na kwamba madaraka yake yanaongozwa na na kutekelezwa kupitia Rasimu. BMK linaweza kubadili na kuboresha mapendekezo yaliyomo katika Rasimu mradi tu maboresho yasiende kinyume na misingi iliyowekwa na kifungu cha 9 (2) cha Sheria ya M.y.K, kama ilivyokuwa pia kwa Tume.
4.Mahakama Kuu haina Mamlaka ya kuamua ni kiwango gani BMK inaweza kuboresha Rasimu kwani hilo ni suala la kisiasa, ingawa BMK inafungwa na kifungu cha 9 (2) cha Sheria ya M.y.K.
Hapana Mkuu Buchanan, sikuja kwa moto wa mabua. Mimi ni mhandisi, huwa nazingatia sana efficiency ya kila activity. Wakati mwingine huwa najitoa katika mjadala iwapo naona ninatumia nguvu nyingi (input) kuhoji kitu lakini kila jibu linalokuja (output) linakuwa halijatoa hasa mwangaza wa ninachohoji.Mkuu Jabulani,
Ulikuja na mbwembwe kibao kumbe ulikuwa moto wa mabua?Wakuu.
Mahakama Kuu katika kesi ya kihistoria ya Saed Kubenea v. Attorney General, Misc. Civil Cause No. 28 of 2014 ilitamka wazi kwamba Bunge Maalum la Katiba halikufungwa na RASIMU YA WARIOBA na wala hawakulazimika kufuata yaliyokuwa ndani ya RASIMU hiyo, ...
Okay, mkuu kama unapata efficient ndogo kutoka kwangu nisikulazimishe kujadiliana na mimi! Kila lakheri na shughuli za uhandisi!Hapana Mkuu Buchanan, sikuja kwa moto wa mabua. Mimi ni mhandisi, huwa nazingatia sana efficiency ya kila activity. Wakati mwingine huwa najitoa katika mjadala iwapo naona ninatumia nguvu nyingi (input) kuhoji kitu lakini kila jibu linalokuja (output) linakuwa halijatoa hasa mwangaza wa ninachohoji.
Ninachosema ni hiki, hukulitendea haki swali langu, nikaona utakuwa umefika mwisho wa uelewa wa hoja yangu, sasa badala ya kulazimisha nipewe majibu, nikaona niachane na mambo ya kurudia rudia maswali. Ulileta hukumu ya Kubenea vs Mwanasheria, nikakuhoji tafsiri ya hukumu, ukarudi kusema kwamba thread yako haijazingatia hukumu bali sababu za hukumu, sasa nikawa najiuliza, kama ni sababu, ina maana mahakama 'imetamka' sababu, na sio hukumu? Angalia hapo nimekuquote ulichosema kwamba mahakama 'ilitamka wazi'. Sasa kama ilitamka, itakuwa iltamka kwenye nini kama sio kwenye hukumu? Kwa nini nakuomba unitafsirie hukumu unakuja kusema hutaki hukumu ila 'sababu za hukumu'? Nikagundua either hautaki kutafsiri hukumu au hauwezi kutafsiri hukumu. Nikaona natumia input kubwa kupata output ndogo and hence low efficiency. Nikaamua kuachana na thread hiyo kwani inawezekana tukawa tunajaza space ya server yetu bila kupata tunachotaka.
Na wewe utajisifu kwamba umechangia mada?
Kinacho-matter kuhusu Majaji ni "Security of Tenure" na sio namna wanavyoteuliwa!Kwani majaji wanateuliwa na nani, unatagemea nini lazima walipe fadhila, tatizo mfumo mbovu na tumelalamika sana mfumo ubadilishwe kupitia katiba, tulifurahi sana baada ya warioba kutuletea rasimu ambayo watu wengi waliikubali lakini ccm wameturudisha nyuma sijaona tofauti ya kimfumo kati ya katiba ya 77 na hii katba pendekezwa
Mkuu,
Kwa nini wewe usiiambie Mahakama iwaamuru wana-UKAWA waache kudharau maamuzi yake?
1. Kwa nini usiseme Bunge Maalum limeboresha maoni ya Wananchi badala ya kusema CCM wamedharau maoni ya wananchi? Pia kwa nini usiseme kuwa Rasimu ya Warioba ilikuwa hailifungi Bunge Maalum la Katiba?
2. Kwa nini usiseme Serikali imeweka msingi wa kupata Katiba Bora kwa kuwashirikisha wananchi wote kutunga Katiba Bora badala ya kusema kuwa CCM imevuruga misingi?
3. Kwa nini usiseme kuwa Katiba inayopendekezwa itapata uhalali wakati wa Kura za maoni badala ya sasa?
Na kama unadai Mahakama ni ya kipuuzi nashauri UKAWA muunde Mahakama zenu ambapo Jaji Mkuu atakuwa ni Tundu Lissu na Majaji wengine ni akina Kibatala, Marando, nk! Hapo nafikiri "haki" itakuwa inatendeka mkuu!