Prof. Malcom Shaw
Member
- Aug 16, 2014
- 14
- 6
Wadau,
Hili kundi linalojiita ukawa liligoma kushiriki katika kutunga katiba ya nchi kwa maslahi ya nchi likidai kwamba lenyewe ndio linalotetea maslahi ya nchi na watanzania kama lilivyo jina lake "UKAWA'. kundi hili, wakati wote limekuwa likisisitiza kwamba liko kwa maslahi ya watanzania wote na wala si vinginevyo.Kundi hili hili ndilo limekuwa likisisitiza kwamba mchakato wa katiba si wa vyama vya siasa, hivyo si sahihi kuhodhiwa na vyama vya siasa kwa maslahi ya vyama. kawaida njia ya mwongo ni fupi , huchukua muda kidogo tu hujitokeza katika sura yake halisi.
Swali; Ni kwa nini mambo ambayo hawa jamaa wamependekeza yabadilishwe katika katiba ya sasa iliwao (ukawa ) wawe radhi, ni yale tu yanayohusiana na madaraka? Au matokeo ya rais kupingwa mahakamani ndilo jambo lenye maslahi kwa watanzania wote kuliko mambo mengine yote? kwa nini mapendekezo ya marekebisho ya katiba ya sasa yote yaliyotolewa yanahusu uchaguzi?
Kwa haya machache tu, kwa wale wenye kuona mbali lakini bado walikuwa hawajalielewa genge hili la UKAWA, na watafakari.